Wakati kelele za Katiba mpya zikikolea, Ni yapi makubaliano kwenye "Muundo wa muungano, Mahakama ya kadhi, Muundo wa Tume huru na Mamlaka ya Teuzi?

Wakati kelele za Katiba mpya zikikolea, Ni yapi makubaliano kwenye "Muundo wa muungano, Mahakama ya kadhi, Muundo wa Tume huru na Mamlaka ya Teuzi?

MoseKing

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2017
Posts
4,928
Reaction score
8,976
Bila makubaliano na haya. Tutegemee kukwama tena
 
Bila makubaliano na haya. Tutegemee kukwama tena
Mahakama ya Kadhi ipo BAKWATA,aina ya Muungano lazima itambue haki za waTanganyika ikiwemo kumiliki ardhi na haki ya kuchagua na kuchaguliwa huko Kibandamaiti.

WaZanzibar kurejeshwa kwao iwapo watakaidi haki za waTanganyika.

Majaji kuomba ajira,kufuta cheo cha ukuu wa Mkoa na Wilaya.

Kuondoa kinga ya kutoshitakuwa viongozi wote.

Ukomo wa uongozi ubunge,uwaziri na Rais.
 
Haya ni maoni yako au ndio makubaliano?
 
Mahakama ya kadhi ni mambo ya kidini
 
1. Tume huru ya uchaguzi ianze kuundwa na wananchi wenyewe kuanzia ngazi ya vijiji na mitaa hadi taifa na kamwe serikali wala chama chochote cha siasa kisihusike katika huu mchakato.

2. Tuendelee tu kuwa na serikali mbili ila wizara za muungano ziwe nne tu; Mambo ya nje, Mambo ya ndani, Ulinzi na Fedha.

3. Majaji wafanyiwe "Vetting" kabla ya kuteuliwa na wasifungamane na chama chochote cha siasa kama ilivyo sasa.

4. Tuwe na serikali ya majimbo (Federal System of Government) na magavana wachaguliwe na wananchi na wasitokane na chama chochote cha siasa na theluthi moja ya mapato ya jimbo yabakie majimboni na majimbo yasizidi 15 Tanganyika na 3 Zanzibar.

5. Viongozi wote wanaochaguliwa na wananchi wahudumu kwa mihula miwili tu na wabunge wasiwe mawaziri na wizara zisizidi 15.

6. Mtu yeyote asiwe juu ya katiba hivyo mtu yeyote anayetuhumiwa kuvunja sheria afikishwe mbele ya sheria bila kujali cheo chake tofauti na ilivyo sasa.

7. Mwenyekiti wa chama chochote cha siasa akigombea urais na kushinda lazima ajiuzulu uwenyekiti wa chama chake na kubaki rais tu.

8. Uraia pacha iruhusiwe na adhabu ya kifo ifutwe na adhabu ya juu iwe kifungo cha maisha jela.

9. Tuhuma zote ziwe na dhamana isipokuwa kama mahakama kwa busara yake itaona kwamba dhamana itahatarisha maisha ya mtuhumiwa.

10. Katiba iseme wazi kwamba ndoa halali itakuwa ni ya mume na mke wa jinsia tofauti tu na kinyume chake itakuwa ni kosa la jinai.

11. Spika wa bunge asitokane na chama chochote cha siasa na awe hajawahi kujihusisha na chama chochote cha siasa katika maisha yake.

12. Polisi iwe ni huduma kwa umma na wala isiwe jeshi na kamwe wasijihusishe na mambo ya siasa kama ilivyo sasa na wanajeshi wasiteuliwe katika nyadhifa za kiraia tofauti na ilivyo sasa.

13. Chama chochote cha siasa kisitumie rasilimali za umma katika kuendesha shughuli zake na hivyo ccm isalimishe mali zote za serikali ilizonyakua huko nyuma.

14. Uchaguzi wowote uweze kupingwa matokeo yake mahakamani endapo kuna wale watakao ona umuhimu wa kufanya hivyo.

15. Kuchagua na kuchaguliwa iwe ni haki ya kila raia mwenye sifa na iwe ni marufuku kumuengua mgombea yeyote kugombea wadhifa wowote kwa kisingizio chochote kile na sifa pekee ya kutokugombea iwe ni kutokuwa raia, umri chini ya miaka 18, kutumikia kifungo gerezani na kutokuwa na akili timamu.
 
Back
Top Bottom