MK254
JF-Expert Member
- May 11, 2013
- 32,408
- 50,809
Kama kawaida yako huwa hutulii kuona kipi kinajadiliwa, hapa kinachojadiliwa sio utumiaji wa bandari ya Dar, kama ulisoma mleta huu uzi amesema Tanzania inaliteka soko la Burundi na DRC, hayo maonyesho yaliyofanyika Burundi ni kwa ajili ya kuzitambulisha bidhaa zinqzotengenezwa Tanzania, kama ambavyo Kenya inaenda kushiriki maonyesho ya biashara nchi mbalimbali, Kenya mnauza bidhaa zenu Rwanda, Burundi, Zambia, Sudan, na sasa hivi mnunuzi mkubwa wa bidhaa za Kenya ni Pakistan kuliko hata Uganda ambaye wlikua mnunuzi mkubwa wa bidhaa za Kenya, kwani biashara ni lazima muwe na ujirani, kwa utumiaji wa bandari hilo linaweza kuwa na maana, lakini sio katika kufanya biashara, leo china anauza bidhaa zake dunia nzima, kwani china imepakana na dunia nzima.
Ukweli ni kwamba, Kenya manufacturing sector imeathiriwa sana na vitu vifuatavyo
1)Bidhaa za china... ni cheap zaidi kuliko za Kenya hivyo kufanya wafanya biashara wengi kwenda kununua bidhaa china badala ya zile za Kenya
2)Viwanda vingi vya Kenya kufungwa kutokana na kushindwa kupambana na soko, vingi vinatumia tecknolojia ya kizamani sana
3)Gharama za uzalishaji Kenya kuwa juu ukilinganisha na Uganda na Tanzania
4)Uchumi wa Kenya kutetereka kutokana na sababu mbalimbali hivyo kufanya biashara nyingi kuhamia nchi zingine, hasa Tanzania
5)Manufacturing sector ya Tanzania na Uganda kukua kwa kasi, na kwasababu technologia inayotumika katika nchi hizi na kutoka china, bidhaa zinazozalishwa zinakua za bei nafuu sana
Tumia akili na kupanua uwezo wako wa kuelewa wacha kuwaza kama beberu anayefugwa kwenye zizi moja siku zote.
Nimetolea bandari kama mfano wa kuonyesha mlivyo mizembe maana majirani zenu wa hapo wanahangaika kukatiza nchi kadhaa hadi wafikie bandari ya Mombasa kisa nyie mumejaa uvivu na ukajanja mwingi.
Mrundi inabidi avuke mpaka aingie Rwanda na kukatiza nchi yote, avuke tena mpaka aingie Uganda na kukatza nchi yote, avuke tena Mpaka aingie Kenya na kukatiza nchi yote hadi afikie bandari ya Mombasa, ilhali hapo kwenu angevuka mpaka mmoja tu. Sasa hadi mwanabiashara afikie maamuzi mazito na ya gharama kiasi hicho, lazima utakua umemtamausha hadi hana lingine la kufanya.
Suala la uwekezaji, kwa nyie hapo kuingia DRC is a walking distance, lakini kwamba Mkenya anakuja kuwapa ushindani hadi huko inaonyesha mlivyo ovyo. Siku mkija kutupa ushindani Sudan Kusini nitaishia kuichukia nchi yangu.