Eric Kabendera ameandika mengi ya kustaajabisha kuhusu hayati John Magufuli aliyekuwa rais wa awamu ya 5 Tanzania. Ukweli kuhusu walipo akina Ben Saanane na Azorly Gwanda umewekwa wazi katika kitabu hicho. Wakati umma ukiwa na taarifa pengine za kuweza kuaminini kwa kiasi kikubwa, inashangaza na kuumiza zaidi kuwa wanaharakati hawa walivyoishia, na hasa uhusika kwa utawala wa awamu ya 5 na hasa aliyekuwa rais wa awamu hiyo.
Samia Suluhu Hassani alikuwa makamu wa rais katika awamu ya 5, mtu wa karibu kabisa na rais Magufuli na kwa namna yoyote ile hawezi kutenganishwa na yalikuwa yakitokea kipindi cha Magufuli, yawe mazuri au mabaya hawezi kutenganishwa nayo!
Mwanzoni rais Samia alionesha adhma ya dhati ya kutaka maridhiano kati ya serikali yake, chama na vyama vya upinzani. Pengine alitaka maridhiano ya upinzani kwani upinzani upo karibu na wanaharakati waliopoteza maisha yao.
Lakini siku za karibuni nguvu ya maridhiano imepungua na ile hulka ya kukosa uvumilivu imeonekana kurudi tena. Suala la Tume Huru ya Uchaguzi na Katiba Mpya vilionekana kama njia ya kuleta maridhiano lakini imeonekana wazi kuwa mambo hayo hayakuzingatiwa. Bado wapinzani wameendelea kukosa haki yao ya kuandamana hata kama katiba iliyopo inaruhusu maandamano.
Freeman Mbowe anajulikana kwa diplomasia yake na weledi mkubwa katika masuala ya kisiasa. Mbowe pia anajulikana kwa uvumilivu mkubwa aliouonesha katika matukio mbalimbali ambapo upinzani ulinyang'anywa haki yake wazi wazi bila kificho. Busara hizi zimeangaliwa na baadhi ya wanaharakati kama upole uliozidi au hata kuwa udhaifu.
Kitabu cha Eric Kabendera kimefunua ukurasa mpya wa ukweli kuhusu awamu ya 5. Kitabu hiki kimeeleza mambo ya kutisha hasa kuhusu hayati Magufuli na uhusika wake kwenye maisha ya baadhi ya watu waliopotea katika mazingira ya kutatanisha. Haya yote na mengine mengi ndio kwanza yanaibua hisia kali zaidi pengine kuwahi kutokea kuhusu awamu ya 5 ambayo rais Samia alikuwa nguzo ya pili.
Bila shaka yataibuka mengi mno na pia wataibuka watu wengi mno baada ya Kabendera kufungua njia. Nionavyo mimi siku za usoni patahitajika maridhiano. Maridhiano kati ya walioumizwa na serikali ya awamu ya 5 ambayo rais Samia alikuwa sehemu muhimu sana.
Kwa muktadha huu Freeman Mbowe ndiye mtu sahihi wa kuwezesha maridhiano hayo kwani tayari amekuwa sehemu ya maridhiano hayo. Freeman Mbowe ni mwanadiplomasia, lakini pia ni mtu mwenye kuthubutu. Tumeona jinsi aliyohatarisha maisha yake mara kadhaa akitetea demokrasia na haki. Hiyo Mbowe apewe nafasi kama lengo ni kutafuta muafaka wa kitaifa. Rais Samia ana kazi kubwa ya kuwa mkweli na mwenye utashi wa kisiasa kuliponya taifa letu la sivyo na yeye anakumbana na lawama ambazo siku zijazo zinaweza kumlazimisha kusimama mbele ya sheria kujibu maswali mengi ya upotevu wa haki za watu wakati wa utawala wa awamu ya 5.