Wakati matajiri duniani wakitoa misaada kukabiliana na COVID-19, Mo Dewji yeye anauza vitakasa mikono

Swali la awali ni kwa nini atoe kwa sasa?Na serikali inasemaje kuhusu corona...inasema ipo under control,na je pesa za majanga zinatumikaje?Za tetemeko na misiba kama ule wa wanafunzi Arusha ilikuwaje?
Kuna kutoa kwa lengo la kujipatia umàarufu...Mo umaarufu anao wa kutosha,kuna kutoa msaada kwa malengo lukuki,mbali na umaarufu kuna kutoa huku ukijua inarudi vipi.
Ulaya(sijafika) naskia wananchi wanazingatia sana reciprocity japo sio lazima,yani baadae huwa wanakupa sapoti katika masuala yako iwe biashara au lolote unalofanya kama vile political will.
Jamii yetu hii kama kinyonga....watu yalishawapata wakaona wawe wagumu tu.Haujui kupatikana kwake labda kuliambatana na "makato ya fweza na maumivu kibao" huenda anawaza zile alizotoa ndio watumie😃😃😃.
Thats why hata wewe unaweza kuwa na "buku la haraka" kijana wa mtaani kwako usimfadhili barakoa akikwama kwa sababu ya mahusiano yenu.
Hali ikiwa tete atatoa sanitizer kwa bei nafuu labda janga bado halijaisha .... Mwanetu Adebayor kasema tu simple and clear hatatoa.Asalaam Aleykum
 
Ndo ujue bongo hamna matajiri.. Unaowaita matajiri nao wanapambana kutoka!!!
tusiishike mioyo ya watu mkononi,tutaishi kwa amani.hata hivyo alivyoamua kuwekeza kwenye sanitizer pia amejitolea pia,kumbuka hii bidhaa watu walivyokuwa wanainunua kwa wingi halafu wanailangua.ilipanda sana bei sababu ilikuwa chache
 
Kweli kabisa mkuu! Cha kuongezea tu ni kwamba serikali imewapunguzia kodi!
Maana kwa kufanya hivo na wao wanapata unafuu ambao watauelekeza kwa wahitaji moja kwa moja! Tusiwalaumu sana maana na wao wanapitia ktk kipindi kigumu wakuu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
4. Mark Zuckerberg huyu ni mmiliki wa Facebook yeye katoa 231,440,000,000 kwa wafanyabiashara wadogowadogo
Nimesoma uzi wote, ila hebu weka sawa hapa kwa mark Zuckerberg, je hizo pesa alizotoa pesa ya wapi..?
TZS
USA
EURO
POUND
 
Hujataka kupepesa macho hata kidogo, Umemaliza Mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo ni muongoza jahazi, hana nature ya kuweka watu Karibu. Na pia kwa sababu hatuna lockdown na watu bado wanachapa kazi na kujiingizia kipato mimi naona ni sawa tu kutuuzia hizo sanitizer maana shughuli za uchumi bado zinaendelea tofauti na wenzetu walioko lockdown.
 
Usimpangie mtu aina ya msaada wa kutoa.
Kuna misaada ya aina mbalimbali, kama fedha taslimu,vyakula mbalimbali,vifaa tiba, (mashine za Hospitali,vitanda,mavazi ya watumishi wa afya,magari ya wagonjwa).
Vile vile siyo lazima unapotoa ujitangaze(INGAWA Ina hasara sana kwa walengwa isiwafikie ,sababu kuna mchwa wa fursa hapo kati).
 
una hakika na unachokiandika?unawajua wangapi waliotoa misaada hapa Bongo?ulitaka akitoa akupigie simu?au akitoa inamnyima haki ya kuuza?MSD wanavyo hizo sabuni,wanatoa bure?
 
Hawaamini matumizi sahihi ya fedha yao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kwamo kwani hiyo list ya baadhi ya mabillionea wanaotoa msaada kwa jamii hawalipi kodi katika serikali yao

sema Mo anamatatizo ndo maana ata wafanyakazi wake anawapa mishahara midogo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kwamokwani hiyo list ya baadhi ya mabillionea wanaotoa msaada kwa jamii hawalipi kodi katika serikali yao

sema Mo anamatatizo ndo maana ata wafanyakazi wake anawapa mishahara midogo

Sent using Jamii Forums mobile app
Mabillionea gani?! Akina Rostam Azizi ambao watu tunachora tu nyendo zake kuangalia what's he up to!!

Kwamba analipa mishahara midogo... Inalipa tofauti na kima kinachopangwa na serikali, au?!

Kama jibu NDIYO, serikali ipo wapi?!

Btw, ni kampuni ipi inayolipa vizuri wafanyakazi wake?! Hiyo serikali yenyewe inalipa vizuri wafanyakazi wake?!

Again, serikali ina mipango ipi ya dharula kuhakikisha sekta binafsi haiathiriki kipindi hiki kigumu badala ya kusubiria kukusanya kodi na kuomba misaada?!
 
Hayo ni mawazo ya kimaskini! We we kazi yako iwe ni kumjaza mimba mkeo halafu utegemee mo aje kukisaidia?
Huu ujinga ndio uliojaa kichwani kwa Watanzania wengi. Tupambane kuzihudumia familia zetu...
Mwanaume ni kubeba majukumu ya familiar yako...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…