GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,660
- 121,325
Kama ulidhani ujio wa hili Janga Kubwa na baya Ulimwenguni la CORONA halina Faida kwa upande mwingine utakuwa umekosea sana na unajidanganya mno. Katika hali isiyokuwa ya Kawaida Serikali ya Afrika Kusini kupitia Waziri wa Polisi Bwana Bheki Cele amekishukuru kupita maelezo Kirusi kibaya cha CORONA kwa ujio wake hasa nchini humo kwani kimesaidia kwa kiasi kikubwa kabisa Kupunguza Uhalifu ambao umekuwa ukiharibu sana Sifa ya nchi hiyo Kimataifa.
" Kama kuna Kipindi ambacho Mimi, Wizara yangu na Watendaji wangu Mapolisi tunalala Usingizi mnono na wala hatuna Presha basi ni Kipindi hiki baada ya ujio huu wa Kirusi hiki cha CORONA kwani hata Wahalifu wenyewe nao wameshika Adabu na wanakiogopa hicho Kirusi CORONA kuliko hata Virungu vyetu na Risasi zetu kiasi kwamba hata Wao kwa Wao wanaogopana na hawataki Kusogeleana na Kushirikiana. Nilikuwa sijui kuwa kumbe hata Wahalifu nao Wanaogopa Kufa. Ningekuwa na uwezo ningekifanya hiki Kirusi CORONA kiwe hakikai sehemu ya Watu wema na wala Kisiwadhuru ila Kidumu kabisa katika yale Maeneo yote yanayokaliwa na Wahalifu na Magenge yao hapa nchini Afrika Kusini " alisema Cele.
Nami GENTAMYCINE nauliza je, ujio wa CORONA kwa huku Kwetu Afrika Mashariki ( hasa hii nchi niliyopo sasa ) umesaidia jambo gani ambalo hata kama huko baadae hiki Kirusi ' Kikitokomezwa ' na Wanasayansi wa Maabara tutakuja Kukikumbuka kama hata pia siyo Kukishukuru kwa namna moja au nyingine kama hivi ambavyo Wenzetu wa Afrika Kusini kupitia Waziri wa Serikali yao ambavyo pamoja na kwamba Kimewaambukiza Wananchi wake wengi na hata wengine Kupoteza Maisha lakini upande wa Pili wa Shilingi ameshukuru ujio wake Kirusi CORONA ( COVID-19 )
Kwa Habari Kamili juu ya hii Taarifa tembelea Gazeti Mtandao la The CITIZEN.