Wakati mwingine tunakutana na watu wakiwa wameumizwa sana na mahusiano ya nyuma.

Wakati mwingine tunakutana na watu wakiwa wameumizwa sana na mahusiano ya nyuma.

Magical power

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2022
Posts
2,158
Reaction score
5,626
Wakati mwingine tunakutana na watu wakiwa wameumizwa sana na mahusiano ya nyuma
1732051356307.jpg

Tunalazimika kuzinyanyua nafsi na mioyo yao iliyojiinamia ndipo tuwapandikize upendo wetu

Huwezi kuupata upendo mkubwa toka kwa mtu mwenye mapito mazito kama hujamponya na maumivu yake ya nyuma ili awe mpya kwanza

Hauwezi kustawisha mche wa upendo penye udongo mkavu. Lazima upalowanishe kwanza ili mche wako utakapoupanda uchipue, umee na ustawi. Mponye kwanza, muinamie hisia za mapenzi na upendo kabla hujaupanda upendo

Mkimponya ni rahisi kuupanda upendo wako huo na ukaota, ukamea na ukastawi vyema na ukalipata lile pendo lake na lile PENZI MDAKO.
 
Usijipe jukumu la kumfix mtu mkuu..
Kuwa wewe katika uhalisia wako pasipo kufake au kutumia nguvu ya ziada kwa sababu kama ataona jinsi ulivyo ni sababu tosha ya kumfanya asahau aliyoyapitia na kuanza nawe upya. Amini atafanya hivyo lakini kama hauna uzito huo kwake, hata uongeze upendo kiasi gani HUTOWEZA
 
Kweli mkuu, be real usihamishe maumivu na hisia mbaya kwa mtu ambae ndio kwanza mnaanza kujuana.
 
Unajitahidi kumfix na kumrudisha awe kama zamani ili muanze mahusiano yenu, lile lijamaa lililomjeruhi na kumuumiza kihisia linamtumia txt mambo, ghafla Binti anakusahau na kurudi kwa lijamaa lake.

Be care broo jipende ww kwanza, piga na kusepa.
 
Yote hayo ya nini bro! Na muda huo unautoa wapi?
Pale unapo fanya hayo kujifanya unalowanisha udongo mkavu na ndiyo hapohapo na wewe unapo pigwa tukio na wewe kuungana kwenye ugonjwa wa maumivu kama yeye.
"Life is unfair" and "There's nothing you can do about it"
Laws za Mapenzi ya hivyo zilizama na meli ya titanic mwaka 1912 now hazifanyi kazi tena.
Why should we play fair in an unfair world?
Nipo nimekaa pale👉
 
Back
Top Bottom