GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 7,189
- 10,375
Hope angelikuwa wapi leo kama asingeonwa na Mzungu kutoka Denmark?
Ilitokea huko Nigeria mwaka 2016.
Mzungu kutoka Denmark alimwokota mtoto wa kiume mitaani aliyekondeana sana kwa kukosa huduma muhimu.
Si kwamba huyo mtoto hakuwa na wazazi wa damu, bali alitelekezwa kutokana na shinikizo la Jamii yake ya Nigeria. Pamoja na kuwa alikuwa mtoto mdogo, alituhumiwa kuwa ni mchawi.
Wazazi wake hawakuwa na jinsi isipokuwa kumtupa mitaani akajifilie zake.
Kwa bahati nzuri, "Msamaria" Mwema wa Kizungu alimkuta akiwa amedhoofika sana, akaamua kumtendea kwa upendo.
Alimpa maji ya kunywa na chakula, na kisha kumpeleka hospitalini.
Alipopona, alimuhamishia kwenye makazi ya watoto aliyoyaanzisha mahsusi kwa ajili ya kuwalea watoto wa Nigeria wanaotupwa kwa kuhusishwa na uchawi. Inaonekana huo ni utamaduni wa kawaida kwenye hiyo Jamii.
Hebu fikiria jinsi Waafrika wa huo mji walivyo wakatili!
1. Waliona ni sahihi mtoto mdogo kufa kwa tabu mitaani kwa tuhuma za "kipuuzi?"
2. Hakukuweko na viongozi wa Serikali waliomwona huyo mtoto alkiteseka mitaani?
3. Hakuna viongozi wa dini walioweza kumwona huyo mtoto mitaani na kumwonea huruma?
4. Ingelikuwaje kama huyo Mzungu asingechukua uamuzi wa kumtendea "Hope" kwa upendo? ( Ni huyo Mzungu ndiye aliyempa hilo jina la Hope)
Siyo kila Mzungu ana "roho" nzuri, lakini kuna wengi walio wema kama huyo wa kutoka Denmark. Sasa hivi Hope ana afya nzuri na anaendelea na masomo.
Kwa hiyo, ni sahihi kusema "Mungu mbariki Mzungu aliyemsaidia Hope"