Wakati nchi za EAC zikiunga mkono Azimio la Baraza la Usalama UN kuitaja Urusi kuondoka Ukraine, Tanzania ili-dodge kikao

Wakati nchi za EAC zikiunga mkono Azimio la Baraza la Usalama UN kuitaja Urusi kuondoka Ukraine, Tanzania ili-dodge kikao

ChoiceVariable

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2017
Posts
66,537
Reaction score
75,687
Habari Wadau.

Wakati Nchi wanachama wa EAC Zikiunga Mkono azimio la Umoja la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuitaka Russia kuondoa Majeshi yake vamizi Nchini Ukraine,Tanzania imekimbia Kikao bila kutokea kwenye upigaji kura.

Kuliko Nchi yetu kuendelea kukimbia vikao vya UN mara kutopoga kura ni Bora ikatoka hadharani na kubainisha msimamo wake rasmi kwenye issue ya Ukraine kwamba inapendelea Russia hata kama haisemi kiuwazi wazi..

Dunia ya Sasa sio ya kuishi kwenye kifungo Cha Kihistoria Cha msimamo wa waasisi Bali ni Dunia ya kuangalia upande wa maslahi.

Viongozi Wetu kutwa kucha kujikomboa Kwa Wazungu na Marekani ila linapokuja suala la Kisiasa wanajificha na kuwa na kigugumizi ambacho ndani yake Kiko upande wa Russia.

Binafsi naona ni mambo ya ajabu kuegemea Russia ambayo Wala Haina Msaada wowote wa maaha hapa Tanzania kulinganisha na West,Sasa ni wakati wa kuwaunga mkono wale wenye maslahi na sisi.

 
20230224_102922.jpg
😜😜😜🤪
 
Habari Wadau.

Wakati Nchi wanachama wa EAC Zikiunga Mkono azimio la Umoja la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuitaka Russia kuondoa Majeshi yake vamizi Nchini Ukraine,Tanzania imekimbia Kikao bila kutokea kwenye upigaji kura...
Kwanini tuwatetee wanaoonewa wakati sisi tunawakandamiza wananchi wetu, haiingii akilini.
 
Habari Wadau.

Wakati Nchi wanachama wa EAC Zikiunga Mkono azimio la Umoja la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuitaka Russia kuondoa Majeshi yake vamizi Nchini Ukraine,Tanzania imekimbia Kikao bila kutokea kwenye upigaji kura...
Huna akili wewe chawa
 
Hata huyo Urussi ana hofu dhidi ya usalama wake kutoka kwa hao NATO hivyo anachukua hatua za kujikinga, Tanzania kuwa neutral kwenye mgogoro wa hao wababe ipo sahihi kabisa..........wapambane wenyewe hadi akili zitakapowakaa sawa wataacha.​
 
Rais Samia alisisitiza kwenye kikao Cha wakuu wa nchi wa Afrika mashariki kwamba sera ya mambo ya nje ya Tanzania inajulikana na Tanzania itasimama na waasisi.
Kuna maslahi gani kusimama na sera za kijima na utumwa?
 
Kuna maslahi gani kusimama na sera za kijima na utumwa?
Mkuu kwani tatizo ni nini!? kutokana na aina ya mahusiano ya kidiplomasia, siasa za kimataifa ambazo zinabeba maslahi ya aina mbalimbali na hivyo kuleta migongano na migogoro ya hapa na pale hususani miongoni mwa mataifa makubwa, nchi imeona ni bora kuendelea na sera ya kutofungamana na upande wowote inapotokea mitifuano ya mataifa makubwa yenye mlengo wa dunia kuwa katika kambi mbili, wao wasuluhishe hayo mambo maisha yaendelee.......​
 
  • Thanks
Reactions: FPT
Back
Top Bottom