warumi
R I P
- May 6, 2013
- 16,218
- 18,440
Wakati habari ya mjini ikiwa ni kuhusiana na nyumba yake kupigwa mnada , staa wa Bongo Fleva , Judith Wambura ' Lady Jaydee ' au ' Jide ' yupo bize jijini Hong Kong , China akila bata.
Mwishoni mwa wiki iliyopita , Kampuni ya Udalali ya MEM Auctioneers and General Brokers ilipewa jukumu la kupiga mnada nyumba ya mwanamuziki huyo iliyopo Mivumoni , Kinondoni jijini Dar baada ya Jide kushindwa kulipa deni alilokopa kutoka taasisi ya fedha ya EFC Tanzania Limited .
Wanahabari wetu waliokuwa na kibarua cha kumtafuta Jide ili kujua anazungumziaje kuhusu nyumba hiyo kupigwa mnada , walizunguka kwenye viunga lukuki vya Dar ambavyo mwanamuziki huyo huwa anapatikana lakini jitihada hazikuzaa matunda , achilia mbali simu yake ya mkononi kutopatikana.
Wakati gazeti hili likielekea mitamboni, chanzo kimoja kilipenyeza habari kuwa staa huyo wa Wimbo wa Yahaya yupo nchini China ' anakula ujana'.
"Kwa taarifa yenu Jide hayupo Bongo , ametimka zake China kula raha kama vipi fuatilieni kwa mbinu zenu mtabaini hiki ninachowaeleza, " kilinyetisha chanzo chetu , Jumamosi iliyopita .
Kabla ya kuwadadisi wadau wengine wa karibu wa Jide , Ijumaa Wikienda liliingia kwenye ' peji' ya Instagram ya mwanamuziki huyo na kukutana na posti iliyoonesha kuwa yupo Dubai akielekea nchini China kuinjoi maisha.
"Dubai - Hong Kong leo nimetoa ushamba sikujua mpaka ndege ikipaa kuna WiFi (huduma ya intaneti) tembea ujionee , " aliandika Jide.
Alipotafutwa Gardner G. Habash ambaye alikuwa mume wa Jide alisema kwa kifupi kuwa hana taarifa zozote kuhusiana na nyumba hiyo kupigwa mnada.
Chanzo: GPL