Wakati Ripoti ya Mwakyembe bado gizani, Law School of Tanzania waendelea kunoa 'wembe'. Watangaza ratiba ya mitihani inayohusisha supp

sajo

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2010
Posts
3,474
Reaction score
6,195
Wakati umma ukiendelea kusubiri ripoti ya Kamati ya Mwakyembe baada ya muda iliopewa ile kamati hiyo kuchunguza nini kinachosababisha wanafunzi wa Shule ya Sheria Tanzania kufeli kwa kiwango cha kutisha kwisha toka tarehe 13 Novemba 2022, hakuna taarifa ni lini Kamati hiyo itasoma na kukabidhi ripoti kwa Waziri wa Sheria Dr. Ndumbaro tayari LST wametoa ratiba ya mitihani kwa wanafunzi waliopo darasani na wale zaidi ya 500 wanaotakiwa kurudia tena masomo waliyofeli. Ratiba inaonesha mitihani itaanza tarehe 02.12.2022.

Tafsiri ni kuwa wale waliofeli kwa matokeo yaliyopita ambayo yapo kwenye uchunguzi wa Kamati ya Mwakyembe maana yake wanahesabika wamefeli rasmi, hakuna uonevu wowote uliofanywa na LST kama wanafunzi wanavyolalamika.

Wembe tayari unanolewa kunyoa wanafunzi wa LST na kama ilivyozoeleka mtaani, Ngariba haogopi mkojo. Wanafunzi jiandaeni na msiache kumwomba Mungu awaongoze vyema na kuwajalia mfaulu.

Mwakyembe na Kamati yake waendelee kufanya compilation ya ripoti, wallet zinenepe. Watanganyika wamezoea kuona kamati zikiundwa ila hawajazoea kuziona zikitoa ripoti kwa wakati au zisitoe kabisa.

Tanzania ni kichwa cha mwendawazimu
 
Attachments

  • Screenshot_2022-11-18-20-57-27-262_com.google.android.apps.docs.jpg
    Screenshot_2022-11-18-20-57-27-262_com.google.android.apps.docs.jpg
    108.2 KB · Views: 12
Tuache siasa kwenye elimu.
Hao wakipita vilaza itasababisha ndugu, jamaa na marafiki kudhurumiwa haki zao. Kosa la wakili laweza kusababishia majuto maisha yako yote
Siasa inaingiaje hapo mkuu? Wanafunzi wamelalamika kuwa usahishaji hauko fair, LST wanasema usahishaji uko fair isipokuwa wanafunzi wanapata elimu duni kwenye vyuo vya sheria, wahadhiri wa vyuo vya sheria wanasema kuwa wanafundisha elimu kwa kiwango kinachokidhi - hapo maana yake kila upande unavutia kwake, ndipo uchunguzi unapohitajika kufanyika, waziri amekunda kamati haijulikani itatoa ripoti lini, LST wanaendelea na business as usual, wewe unasema wanafunzi 650 kati ya 700 ni vilaza, justification huna unawaza makosa ya wakili kilaza kumgharimu mteja ilhali kanuni zinasema wakili akifanya kazi chini ya kiwango mteja anaweza kumdai fidia ileile au zaidi ya ambayo alikuwa anadai mahakamani.
 
Wakati umma ukiendelea kusubiri ripoti ya Kamati ya Mwakyembe baada ya muda iliopewa ile kamati hiyo kuchunguza nini kinachosababisha wanafunzi wa Shule ya Sheria Tanzania kufeli kwa kiwango cha kutisha kwisha toka tarehe 13 Novemba 2022, hakuna taarifa ni lini Kamati hiyo itasoma na kukabidhi ripoti kwa Waziri wa Sheria Dr. Ndumbaro tayari LST wametoa ratiba ya mitihani kwa wanafunzi waliopo darasani na wale zaidi ya 500 wanaotakiwa kurudia tena masomo waliyofeli. Ratiba inaonesha mitihani itaanza tarehe 02.12.2022.

Tafsiri ni kuwa wale waliofeli kwa matokeo yaliyopita ambayo yapo kwenye uchunguzi wa Kamati ya Mwakyembe maana yake wanahesabika wamefeli rasmi, hakuna uonevu wowote uliofanywa na LST kama wanafunzi wanavyolalamika.

Wembe tayari unanolewa kunyoa wanafunzi wa LST na kama ilivyozoeleka mtaani, Ngariba haogopi mkojo. Wanafunzi jiandaeni na msiache kumwomba Mungu awaongoze vyema na kuwajalia mfaulu.

Mwakyembe na Kamati yake waendelee kufanya compilation ya ripoti, wallet zinenepe. Watanganyika wamezoea kuona kamati zikiundwa ila hawajazoea kuziona zikitoa ripoti kwa wakati au zisitoe kabisa.

Tanzania ni kichwa cha mwendawazimu
WASOMI WETU DEGREE FAKE ZINAWATESA SANA HATA MAKAZINI
"HONGERA LAW SCHOOL KWA KUSIMAMIA TAALUMA"
 
Kama wanasheria wanalia basi hakuna aliye salama
 
Pigeni Supp hakuna ushindi wa mezani. Zambia ali faulu 1 tu. Itakuwa Tz watu 26!
Wanasheria na taaluma ya sheria kwa jumla, migogoro hutatuliwa kwa hoja na sio nguvu. Hoja za wanafunzi ni kuwa wanaonewa, mitihani haisahishwi kabisa ama haisahishwi ipasavyo - wanataka kuona booklet zao mchawi ajulikane kama ni mwanafunzi au usahishaji - hakuna anayeomba kufaulishwa - kinachodaiwa ni haki. Unafanya supp kwa njia zilezile ulizoelekezwa naq, wasahishaji walewale na utegemee matokeo tofauti
 
NECTA uliwahi kuomba booklet?
 
NECTA uliwahi kuomba booklet?
NECTA ukikata Rufaa, mtihani wako unaposahishwa kwa mara ya pili unaitwa kushuhudia usahishaji huo swali kwa swali, unakuwa umepewa booklet yako impliedly.
 
Uongo mkubwa. Hata chuo tu huoneshwi booklet.
 
NECTA uliwahi kuomba booklet?
Halafu mkuu hii mambo ya kufananisha/kulinganisha ni ya kienyeji sana, kwamba zambia alifaulu 1 basi na huku ni sawa kufaulu 26 au hii ya wanafunzi kuomba booklet, uulize kama NECTA huwa wanatoa booklet au la - sio sawa. Kila jambo lina kanuni na taratibu zake, kanuni za LST zinaruhusu ukaguzi wa booklet, kwa hiyo bila kujali kama NECTA au chuo kikuu fulani wanatoa booklet au la, tunazingatia kanuni za mitihani na rufaa za LST.

Sasa ingawa kanuni zinaruhusu ukaguzi wa boolet, LST (uongozi na walimu) hawatekelezi takwa hilo, hawatoi booklet kwa ukaguzi.
 
Mkuu mm sikupingi sana. Ila ambacho binafsi sikipendi ni siasa kuingilia taasisi za Elimu. Tuta haribu Elimu yetu na baadae tutakuwa Taifa la hovyo sana.
 
Uongo mkubwa. Hata chuo tu huoneshwi booklet.
Hii tabia ya kulinganisha itakupoteza mkuu, jambo fulani haliwi halali sababu tu linafanywa na mwingine. Weka ukweli wako.
 
Mkuu mm sikupingi sana. Ila ambacho binafsi sikipendi ni siasa kuingilia taasisi za Elimu. Tuta haribu Elimu yetu na baadae tutakuwa Taifa la hovyo sana.
Siasa ndio hizo sasa zinazofanywa na LST kusema kuwa wanafunzi wanafeli kwa kuwa vyuo vikuu wanafundishwa kwa kiwango duni (ni mawazo tu pasi uthibitisho), wanafunzi hawataki mbeleko wala siasa wanataka kanuni zilizowekwa na haohao LST zifuatwe na kutekelezwa, wao LST hawataki zaidi ya kuleta maneno yasiyo ya kikanuni, sasa hapa nani anayeleta siasa?? Mamia ya watoto wa hali za kawaida kabisa kiuchumi ndoto zao zinakwamishiwa hapo LST sio kwa sababu wanafunzi ni wajinga bali kwa sababu wababe LST hawataki kutekeleza kanuni, kwa nini isiaminike kuwa wanafunzi wanaonewa?
 
Siasa ndio hizo sasa zinazosemwa na LST kuwa wanafunzi wanafundishwa kwa kiwango duni (ni mawazo tu pasi uthibitisho), wanafunzi hawataki mbeleko wala siasa wanataka kanuni zilizowekwa na haohao LST zifuatwe na kutekelezwa, wao LST hawataki zaidi ya kuleta maneno yasiyo ya kikanuni, sasa hapa nani anayeleta siasa?? Mamia ya watoto wa hali za kawaida kabisa kiuchumi ndoto zao zinakwamishiwa hapo LST sio kwa sababu wanafunzi ni wajinga bali kwa sababu wababe LST hawataki kutekeleza kanuni, kwa nini isiaminike kuwa wanafunzi wanaonewa?
Hapo sawa nime kuelewa ila isiwe kufaulishwa kama wale wa Form 4 miaka ya nyuma, matokeo yalifutwa na kuletwa mapya.
 
Hapana mkuu, hoja ni kuwa mitihani isahishwe kwa haki na haki ionekane ikitendeka. Hakuna kufaulishwa. Pia hizi pesa za supplementary ni mtaji kwa LST hazifanyi shughuli yoyote ya maana, wala hazina ukaguzi, LST wanapenda watu wasupp kila mara ili wao wapige hela, sasa kama ishu ni maslahi ya Taifa, hapo ni Taifa linalonufaika au wachache??
 
Wanafunzi hawako competent, Mwakyembe na tume yake ndio maana wako kimya
Wametumia pesa ya umma kufanya uchunguzi, ni lazima watamke hadharani hayo maneno kuwa "uchunguzi umebainisha kuwa wanafunzi hawapo competent". Kukaa kimya maana yake ni kuwa tumetupa hela ya umma kwa kazi isiyo na tija.
 
Hapana mkuu, hoja ni kuwa mitihani isahishwe kwa haki na haki ionekane ikitendeka. Hakuna kufaulishwa. Pia hizi pesa za supplementary ni mtaji kwa LST hazifanyi shughuli yoyote ya maana, wala hazina ukaguzi, LST wanapenda watu wasupp kila mara ili wao wapige hela, sasa kama ishu ni maslahi ya Taifa, hapo ni Taifa linalonufaika au wachache??
Hoja zako ni za msingi naona.
1. Ufundishwaji utoke Theory uwe practical
2. Fairness ya mitihani
3. Usahihishaji wa mitihani.
4. Assessment in General iwe realistic not business oriented. Lets hope Tume ita leta vitu vizuri. Tiyari naona kelele zimesaidia nafasi za kazi LST zilitangazwa.
 
Back
Top Bottom