sajo
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 3,474
- 6,195
Wakati umma ukiendelea kusubiri ripoti ya Kamati ya Mwakyembe baada ya muda iliopewa ile kamati hiyo kuchunguza nini kinachosababisha wanafunzi wa Shule ya Sheria Tanzania kufeli kwa kiwango cha kutisha kwisha toka tarehe 13 Novemba 2022, hakuna taarifa ni lini Kamati hiyo itasoma na kukabidhi ripoti kwa Waziri wa Sheria Dr. Ndumbaro tayari LST wametoa ratiba ya mitihani kwa wanafunzi waliopo darasani na wale zaidi ya 500 wanaotakiwa kurudia tena masomo waliyofeli. Ratiba inaonesha mitihani itaanza tarehe 02.12.2022.
Tafsiri ni kuwa wale waliofeli kwa matokeo yaliyopita ambayo yapo kwenye uchunguzi wa Kamati ya Mwakyembe maana yake wanahesabika wamefeli rasmi, hakuna uonevu wowote uliofanywa na LST kama wanafunzi wanavyolalamika.
Wembe tayari unanolewa kunyoa wanafunzi wa LST na kama ilivyozoeleka mtaani, Ngariba haogopi mkojo. Wanafunzi jiandaeni na msiache kumwomba Mungu awaongoze vyema na kuwajalia mfaulu.
Mwakyembe na Kamati yake waendelee kufanya compilation ya ripoti, wallet zinenepe. Watanganyika wamezoea kuona kamati zikiundwa ila hawajazoea kuziona zikitoa ripoti kwa wakati au zisitoe kabisa.
Tanzania ni kichwa cha mwendawazimu