Unafikiri kwa kutumia nini?Bro. Wewe na CORONA tu . Ulishaambiwa CORONA iwepo au isiwepo maisha lazima yaendelee. Kama ukijisikia dalili za CORONA Jifukize au kama unaiogopa sana CORONA Chukua tahadhari binafsi wewe na wale uwapendao.
FactKorona ipo na inaendelea nasi tunahitaji kula na serikali inahitaji kodi lazima tuishi nayo anaeumwa atibiwe tusioumwa tuendelee kupiga kazi atakaekufa siku zake zimefika! ni wakati sasa tufunge mjadala wa korona ni hakika sasa ni old story na inakera sababu hatumudu lockdown kwanini tupoteze nguvu kuzungumzia korona?!!
Atakosa pa kulalaMficha malazi ?
Uliona wapi mchinja kuku asitoke na doa la damu? πππNenda Hospitali ya Mwananyamala uone jinsi corona ilivyotafuna madaktari
Kwanini mamlaka hazijikiti kuhimiza watu wajihadhari na kuelezea uelekeo wa ugonjwa huo nchini? Yes nipo karibu sana na wanaoathirika na hili janga na kwa hakika katika mwezi huu wa sita hali imeendelea kuwa ya kutokuridhisha kabisa!Mkuu, bandiko lako hili linaweza kuwa na maana sana kama wewe uliyeandika bandiko hili ni mtalaam wa tiba tena anayeona wagonjwa kila siku kwa lengo la kutibu. Unaposema kuwa kuna watu unaowaona wakiwa na vikohozi vyenye dalili zinazofanana na COVID 19, haina maana kuwa vikohozi vyao vinasababishwa na virusi vya Corona.
Nikushauri tu uwaache watalaam wa tiba wafanye kazi yao bila kuingiliwa na mambo haya ya kisiasa kwa sababu wao ndio wenye vipimo vinavyothibitisha kuwa kinachomfanya akohoe ni vijidudu vya aina gani. kama ni mwanahabari basi jikite kwenye maadili ya kazi yako, vinginevyo unaonekana kama mchochezi fulani hivi.
Kama njia inayotumiwa na watanzania kwa sasa kama tunavyoiona ni hiyo wanayosema Mungu kamtuma mtumishi wake tuishi hivyo basi huyo Mungu aliyemtuma hawapendi Watanzania.Afadhali umetanabaisha kwamba tunaweza kufikiri mnatumiwa na Mabeberu, na huo ndio ukweli. Hivyo basi, fanya ulichotumwa ili upate ujira wako. Tunachofahamu ni kwamba Mungu amemtumia Rais wetu kutuonesha njia ya kuishi japo mnasema kunao huo ugonjwa.