Wakati Serikali ikiendelea kuficha ukweli kuhusu COVID 19, baadhi ya Watanzania wenzetu inawatesa

Wakati Serikali ikiendelea kuficha ukweli kuhusu COVID 19, baadhi ya Watanzania wenzetu inawatesa

G Sam,

Afadhali umetanabaisha kwamba tunaweza kufikiri mnatumiwa na Mabeberu, na huo ndio ukweli. Hivyo basi, fanya ulichotumwa ili upate ujira wako. Tunachofahamu ni kwamba Mungu amemtumia Rais wetu kutuonesha njia ya kuishi japo mnasema kunao huo ugonjwa.
Usibadiri jina ,ni yesu
 
Pengine watu wanaweza kufikiri kuwa sisi baadhi yetu tunaisakama sana Serikali kuhusu COVID 19 kwa kutumwa na mabeberu, la hasha! Tunafanya hivyo kwa kuwa tunawapenda sana ndugu zetu na watanzania kwa jumla.

Inashangaza sana kuona serikali inayojiita serikali makini ikitoka hadharani na kuitambia dunia kuwa Tanzania COVID 19 imepungua sana na hitokaa itokee eti maambukizi yaongezeke. Matokeo yake watanzania wengi wameamua kuishi kwa namna ya ajabu kabisa. Haya ni matokeo ya kunyimwa ukweli na wakulaumiwa ni Serikali na Wizara ya Afya kwa jumla.

Ninasema hayo kwa kuwa nimeshuhudia ndani ya siku za hivi karibuni Watanzania wenzangu wakisimbuliwa na homa kali na kikohozi huku wakiwa na dalili nyingi za Corona! Serikali iko wapi?

Kama kwa hakika tutaendelea hivi na hii tabia ya kupuuza puuza kutokana na asili yetu watanzania na mbaya zaidi tunao sasa viongozi wanaoendana na asili yetu basi tutajikuta tuligharamika kwa kiwango kikubwa na matokeo yake ni nchi kuanza kupata midororo mikubwa ya kibiashara.

Nitoe Rai kwa serikali, kusema kuwa baadhi ya Wataznania wanasumbuliwa na Corona si dhambi, kutoa tahadhari na kuhimiza watu kujikinga si dhambi. Dhambi ni mwenenndo ambao kwa sasa tumeamua kusafiri nao.

Tuweke kumbukumbu ili siku moja tuje kusemezana bila haya!
Hivi bado mko bize na covid19?
 
Wiki chache zilizopita nilipatwa na ugonjwa usioeleweka, mafua makali, kikohozi, homa kali, uchovu/maumivu ya mwili, kifua kubana kwa mbali na kupoteza uwezo wa kunusa/ladha ya chakula. Hakuna dawa nilizozoea zilizofanya kazi (Azuma,Toff-Plus,Coldril,Ampicillin) nilihamia kwenye mchanganyiko wa tiba asili na dawa za mzungu.
  • Kunywa mara tatu mpaka tano kwa siku mchanganyiko wa limao+tangawizi+pili pili kichaa -> Kupunguza kikohozi.
  • Kusukutua koo na mchangayiko wa maji ya uvuguvugu na chumvi -> Kupunguza maumivu ya vindonda kooni.
  • Kutafuna karafuu na tangawizi mbichi - kurudisha ladha ya chakula, na kutuliza maumivu ya vidonda kooni.
  • Kujifukiza kwa majani ya mkaratusi, tangawizi na viks kingo ya mafuta ->Kufungua pua na kurudisha pumzi.
  • Panadol -> Kupunguza maumivu ya kichwa na kutuliza homa.
Nilienda hopsitali wakaniambia sina tatizo zaidi ya uchovu na ninywe maji tu kwa wingi lakini hali haikutengemaa, nilikosa usingizi kwa siku 4 mfululizo hali ilipokuwa mbaya ila ndio hivo nilijipa moyo muda wangu ulikuwa haujafika na kuendelea kupambana, inawezekana niliumwa corona na kuambukiza watu wengi katika mizunguko yangu ama ilikuwa ni aina nyingine ya ugonjwa mpya bila vipimo ni ngumu kujua.

Ushauri wangu ni chukua tahadhari, jipatie maarifa ya namna ya kutuliza dalili zinazoendana na ugonjwa wa COVID-19 kwa njia asili pale ambapo dawa za kawaida unazotumia zimeshindikana, ondoa hofu kabisa pale unapoona hali ni mbaya kifo kipo na utakufa mara moja, ni bora ufe ukipambania uhai wako mpaka pumzi ya mwisho kuliko kukata tamaa na kusubiria ujifie, mwisho usitegmee mwanasiasa yoyote akulinde afya ama uhai wako.

Maisha lazima yaendelee lakini kuchukua tahadhari na kujiongezea maarifa katika mapambano sio ujinga.
 
Pengine watu wanaweza kufikiri kuwa sisi baadhi yetu tunaisakama sana Serikali kuhusu COVID 19 kwa kutumwa na mabeberu, la hasha! Tunafanya hivyo kwa kuwa tunawapenda sana ndugu zetu na watanzania kwa jumla.

Inashangaza sana kuona serikali inayojiita serikali makini ikitoka hadharani na kuitambia dunia kuwa Tanzania COVID 19 imepungua sana na hitokaa itokee eti maambukizi yaongezeke. Matokeo yake watanzania wengi wameamua kuishi kwa namna ya ajabu kabisa. Haya ni matokeo ya kunyimwa ukweli na wakulaumiwa ni Serikali na Wizara ya Afya kwa jumla.

Ninasema hayo kwa kuwa nimeshuhudia ndani ya siku za hivi karibuni Watanzania wenzangu wakisimbuliwa na homa kali na kikohozi huku wakiwa na dalili nyingi za Corona! Serikali iko wapi?

Kama kwa hakika tutaendelea hivi na hii tabia ya kupuuza puuza kutokana na asili yetu watanzania na mbaya zaidi tunao sasa viongozi wanaoendana na asili yetu basi tutajikuta tuligharamika kwa kiwango kikubwa na matokeo yake ni nchi kuanza kupata midororo mikubwa ya kibiashara.

Nitoe Rai kwa serikali, kusema kuwa baadhi ya Wataznania wanasumbuliwa na Corona si dhambi, kutoa tahadhari na kuhimiza watu kujikinga si dhambi. Dhambi ni mwenenndo ambao kwa sasa tumeamua kusafiri nao.

Tuweke kumbukumbu ili siku moja tuje kusemezana bila haya!
Wki iliyopta nilibanwa na homa kali na mafua mepesi
 
Ha
Mnapotaka kujua takwimu za vifo na wagonjwa wa corona, msisahau kuhimiza pia mortality rate ya magonjwa mengine coz Tanzania kama nchi inasumbuliwa na magonjwa mengi mno.
Hapo chacha...
Ninawashauri Hawa VIJANA wenzangu wakishapata hela ya 3 mzuka wawe wanabajeti na kunywa maziwa na kupunguza FARU JOHN kwi kwi kwi kwi in Zitto Kabwe voice
 
sasa hivi BBC swahili wapo kimya .HUKO KENYA korona inaua na wagonjwa wanazidi kuwa wengi.
Lakini kwenye page yao ya instagram wapo kimyaa.ngoja wapate habari za corona Tanzania uone walivyo fasta kupost
 
Tumpe tahadhari pia Mwenyekiti wetu Mbowe, kwenda kulewa na hawara wake maeneo ya wazi kama bar na pubs kunaweza mletea Corona.

Nawasilisha makamanda wenzangu.
Wakati mwingine wana JF tuwe serious kwa michango yetu. Maada iliyeko mbele yetu ni very serious. Hapa kinachojadiliwa ni hatua ya serikali na raia wake kuhusu Corona. Tukatae au tukubali: KORONA IPO!! Mbowe na hawara yake inatuhusu nini hapa? Au ni njia ya kututoa kwenye mada?
 
Muangalie huyu mzee leo HII hataki kusikia hyo mbinu mliyokuwa mkiililia
Screenshot_20200623-151213.jpg
 
Kama corona ni hatari kama mnavyotuaminisha mbona I'd za wapiga debe wa hivi vijimafua ziko active na hamfi? Serikali haiwezi kuangaika vijimafua visivyo weza kuua hata kuku chapeni kazi
 
Tumpe tahadhari pia Mwenyekiti wetu Mbowe, kwenda kulewa na hawara wake maeneo ya wazi kama bar na pubs kunaweza mletea Corona.

Nawasilisha makamanda wenzangu.
Hivi "Bia yetu" kabadili ID au katoweka humu??
 
TUSIPENDE KUAMINI MANENO YA WATU WASIYO NA WATALAM WA AFYA.

Jaribu kufikiria kidogo; vyuo vimefunguliwa tarehe 1 mwezi 6. Wanafunzi wanatoka pande zote kutoka hapa Tanzania, lakini mpaka Leo hakuna mgonjwa wa CORONA aliyegunduliwa kutoka taasisi yeyote ya elimu hapa nchini. Maswali yangu

1. Hiyo CORONA inayopigiwa kelele inawakamata watu gani make hakuna aliyeshudia ata jirani yake mwenye Corona.

2. Je, kuna serikali ambayo haipendi taifa lake?
Mwishi naomba tuachane na propaganda tufanye kazi kujenga uchumi wa familia na taifa kwa ujumla
 
Kama corona ni hatari kama mnavyotuaminisha mbona I'd za wapiga debe wa hivi vijimafua ziko active na hamfi? Serikali haiwezi kuangaika vijimafua visivyo weza kuua hata kuku chapeni kazi
Tunajikinga sana sana sana. Tunaonea wenzetu ambao licha ya kutokujikinga pia hawapewi msukumo wowote ule na mamlaka. Maisha tunayoishi hapana!
 
Back
Top Bottom