Wakati Uchumi wa nchi una nafuu wafanyakazi waliongezewa kati ya elfu 8-12. Je, sasa hivi itakuwaje?

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Hakika Wafanyakazi wa Tanzania ni wa kuhurumiwa mno! Kama mwaka uliopita ambako hakukuwa na Maandamano ya kupinga Ugumu wa Maisha Nyongeza ya Mshahara ikafichwa siku ya Mei mosi, kwa maelezo kwamba watakutana nayo kwenye mshahara wa July, lengo likiwa Wafanyabiashara wasipandishe bei ya bidhaa (porojo), japo ilikuja kubainika kwamba walichoongezwa ni kati ya elfu 8 na elfu 12 kulingana na kima cha mshahara.

Sasa tunajiuliza je, mwaka huu ambao Ugumu wa maisha ni kama gumzo la nchi kiasi cha kusababisha Maandamano, wafanyakazi wa Tanzania wataongezewa sh ngapi?

Hebu ngoja tusubiri.

Kwa shingo upande nawatakia Mei mosi Njema.
 
Mishahara kupanda kila mei mosi haiko sustainable. Hilo haliwezekani, anayesema otherwise anaamua tu kupotosha watu kwa maslahi yake.
 
Huwa wanamshangilia, acha aupige mwingi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…