WAKATI UKUTA! Wacheza filamu za Kibabe wa zamani walivyo hivi sasa

Wakati umebaki kuwa kitendawili...binadamu mpaka leo karne ya 21 tumeshindwa kuufanyia "figisu" angalau tuweze kuUrudisha au kuongeza japo sekunde moja, TUMESHINDWA. Hatuna hayo mamlaka. Ukizaliwa unakuja na "time frame" ambayo hata wewe huijui...

KWa hizo picha kuna mengi ya kujifunza. Ujana ni maji ya moto, tusijisahau tukaona kuwa yatabaki kuwa ya moto milele. Kama yalivyoanza kuwa ya moto taratibu mpaka kufikia kuwa ya moto sana ndivyo hivyo hivyo yatakavyoanza kupoa mpaka kufikia hatua kuwa umoto haufai hata kukandia kidole.

Tukiutumia ujana wetu vizuri, hakika uzeeni hatutopata tabu na wala hatutokuwa na usumbufu kwa jamaa zetu.
Ujana ndio wakati wa kupiga kazi hasa, usichoke wala kupumzika ila pale inapobidi...nguvu zikishapotea yanabaki majuto tu.
Utatizama nyuma kujutia nafasi ulizopoteza na hakika huwezi kurudisha wakati nyuma kuzipata tena...majuto ni mjukuu.

Naamini hao Arnold and Co. wametumia ujana wao vyema kwa kufanya kila walichokipenda, ni wazi kabisa wana machache sana ya kujutia. Sasa ni watu wazima wakitizama nyuma wanatabasamu kwa kumbukumbu nzuri.
 
ahahaha,mkuu nimekulia tandale beo beo,pale lingo la kuni kabla ujakifikia kituo cha daladala cha tandale chama na nimesoma msingi pale makurumla(sasa mwalimu nyerere primary school) opposite na msikiti wa mwembechai!
Dah! Nilijua umekulia kama sio mbelekese, itakua magungumuka au zénzélégé.
 
Uswaz kuna raha yake mnaweza kujikuta mpo na baba ako mnaangalia pilau bla kujijua
 
Rambo naona bado yupo poa ila Arnold aseeeh daah, alikuwa anatumia dawa za kusisimua misuli ndiyo maana imelelemka ama?

Maana wote umri unaendana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…