WAKATI UKUTA! Wacheza filamu za Kibabe wa zamani walivyo hivi sasa

WAKATI UKUTA! Wacheza filamu za Kibabe wa zamani walivyo hivi sasa

Hivi siku hizi kuna movie za kivita kweli kama zile za enzi zetu...Unakuta pale Eastern Condours pale Missing in Action, Delta Force, America Ninja, Fifty Fifty, President Man...
Hakuna movie za namna hiyo, siku hizi mambo ya animation, 3D yameshusha kiwango cha utamu wa movies.
 
mkuu,mie nimeanza kuzicheki pale tandale chama tangu the late 90s kwenda 2000s!halafu tunacheki mapicha,ikifika mida ya saa tatu usiku linawekwa "pilau" mpaka liamba!
Ni kitambo mkuu,kama umekulia uswazi hivi ni vitu vya kawaida kwa sie tulio kulia uswazi!!
Pakiandikwa usiku pilau sio uende na ndizi ilikuwa mambo yale hakuna fix kila kitu cha kweli.
 
Huwezi pingana na muda na aging pia.Wote ndo njia yetu iwapo ukibahatika kuishi muda mrefu hapa duniani
 
Siku hizi hakuna movie za kibabe. Ni makompyuta tu meengi na upuuzi wa aina hiyo. Eti starring mkali wa kukimbiza gari na pikipiki! Zamani starring ni mkono kwenda mbele lazima awe mtu wa martial arts, mbavu nene, na mkatili fulani hv. Ndio maana enzi hizo akitoa Rambo wote mnaitafuta, akitoa Damme, Arnold ni gumzo mtaani.

Siku hizi ni jambo la kawaida kumkuta kijana wa kiume kajikunyata na Dada zake sitting room anaangalia tamthilia za ki philipino za story za maigizo ya Mapenzi Kyoto wa kiume anatoa chozi na kila tamthilia haikosi character moja kuwa choko! Dunia inakaribia kufika Ubungo Bus terminal tushuke wote!
 
We jamaa umeniua yeuwiiiiiiiiiiiie mbavu zangu jaman auwiiiiiiiiiiie
 
Nguvu kitu cha kwisha mitaa ya kati tulikuwa na brother wetu mbavu nene kifua jumba sasa hakujua kama waqt hupita kuna siku kauvamia mfuko wa cement(dongo ulaya)kila akitaka kuunyanyua unarudi kila akikukuruka unarudi akabaki anautizama tukaenda kumsaidia tukakuta chozi linamtoka akasema enzi zangu mie sasa nimebaki django jina tu sio yule django mwenyewe.
hahaha maskini....
 
Ha haaa...dah bro atakua amehuzunika sana yaani amerudi kuwa mnyonge tena...maisha haya si ya kuyatambia hata kidogo
 
Yupo Pawa Masikaga Mbeya kule walikuwa wanabeba mifuko ya cement aka sument hadi mitano at a go miaka hiyo leo zimebaki story tu, chezea ujana fainali uzeeni
 
editing hizo...tena zipo application kule playsore ambazo waweza kumzeesha mtu
 
nakumbuka enzi hizo kuangalia pilau kwenye vibanda umiza ilikua n kuanzia saa mbl usiku,mwenyekiti wa kijiji ndio alikua anasimama mlangoni akikagua ndevu kama huna hauingii
 
Back
Top Bottom