Keynez
JF-Expert Member
- Feb 12, 2007
- 3,809
- 6,948
Kutokana na kwamba sasa hivi tunaendelea kuwa na wingi wa Marais waliotumikia nchi yetu na wengine kufariki wakiwa madarakani, nadhani imefika wakati sasa tuwe na siku maalumu ya President's Day.
Siku hiyo tutaitumia kuwaenzi na kuyatafakari yale mazuri na yale tuliyojifunza kutoka kwa kila Rais aliyewahi kuwa madarakani. Hii pia italeta usawa katika kuwakumbuka marais wote.
Hii pia itasaidia kupunguza mrundikano wa sikukuu au maadhimisho yanayowahusu Marais mmoja mmoja. Tunaweza kuwa na majadiliano mapana na yenye tija zaidi tukiwa na mijadala ya marais wote na utendaji wa kila mmoja na legacy walizotuachia. Majadiliano na mijadala hiyo inaweza kuwa kwa kipindi cha wiki nzima kuelekea maadhimisho ya hiyo President's Day.
Kwa kusema hayo, napendekeza Nyerere Day ibadilishwe na kuwa Tanzania President's Day.