Wakati umepigika kazi gani ya ajabu uliwaza kufanya?

Matumizi yote ni Muhimu, hakuna tumizi la kizembe hapo
 
Kaka usingetolewa Rwamishenye, huwezi ishi mji ule ukapitia maisha hayo. Mitaa ya home hapo ungekomaa na kina Roja, Saddam, Chai Jaba na wajanja kibao nakadiria lika lenu maana mwaka unaondoka maybe nilikuwa sijaanza kuongea au sijazaliwa kabisa. Ingawa nimecheka sana stori yako.
 
Dah! Nilifanya sana kazi ya kufyeka Mzumbe chuoni na kuzunguuka na Trekta lile la uchafu kama mzoa taka kwa mshahara wa 22,000/= kwa mwezi, aisee acha tu sometime nikikuwa najificha nisionekane na wanaonifahamu, nilipiga kazi pale nadhani kama miezi3 hivi
 
Mshahara wa 2.8 milioni kwa miaka 9, halafu kiinua mgongo milioni 4

Maafisa utumishi mtufafanulie kidogo
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aisee pole mkuu, ingekuwa mimi ningemtafuta hata mmoja nimshikishe adabu apate kilema

Kiukweli tulipanga kisasi cha mda mrefu kama tungefanya mda ule tungekuwa jela sasa hivi, ila hakikufanikiwa maana boss nilirudi full time school afu nikaja home dar kwa mshua baada ya hilo balaa, nilikuwa nna mabalaa sana moshi mtukutu kweli kweli

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona kawaida tu kama hujipangi we 2.8 mil unaona nying hyo
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole sana mkuu, Hakika wewe umesota

Tangu ukiwa na miaka 5, aisee umeteseka
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakubaliana na wewe, kwenye kila utajiri wa mtu kuna siri kubwa mno nyuma yake...

Kisa chako kimenikumbusha Tajiri mmoja pale mwanza, pia kawekeza sana Dar, biashara zake nyingi anafanyia nje analeta bidhaa Nchini...

Hapo kabla alikuwa jangiri na Mwizi wa mifugo ila baada ya kupata pesa akaamua kuwekeza kwenye biashara, hadi sasa huyo mtu anapesa chafu sana...

Usione mtu kafanikiwa ukafikiri haja hustle, tena wengi huwa wamefanya dili chafu sana na pengine kwenye dili zao chafu wameua watu kabisa...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unamtetea lakini ukweli ni kwamba hakujipanga,

Inaonesha alikula bata sana japo na ndugu walimshika miguu

Inaonesha aliona hizo hela zipo tu siku zote, kumbe kuna muda huwa zinakata (hili kosa watu wengi wanalifanya)

Kuna Uzi wa watu kufilisika, ukisoma utagundua watu wanavyochezea maisha

Ukitaka ku justify hata matumizi ya milioni 20 hazitatosha kwa mwezi
hii hela kama huna ndio unaiona kubwa ila kwa sisi watu wa extended family hiyo hela ni kidogo sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona kawaida tu kama hujipangi we 2.8 mil unaona nying hyo

Sent using Jamii Forums mobile app

Nimeandika nikafuta.

Nimekumbuka ni Intl NGO na safari za nje ‘kibao’ kwa miaka 9, mshahara 2.8M ila kiinua mgongo ni 4M tu... maisha yako tofauti sana.

Kisha baadae karudi kugombea kazi ya mshahara 90k na aliishi fresh tu, maisha yana vionjo vingi sana.... yote inawezekana.
 
Sasa baadae aliishi kwa 90K kwa mwezi

Mbona aliishi, mbona maisha yaliendelea

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Daah mkuu nadhani mother aliona maisha yanazidi kuwa magumu,akaamua kunitoa maeneo hayo.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nayakumbuka maeneo hayo ya Rwami,Kwa Kagambo,Kibeta,hamjuju,n.k
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata 50M haitoshi kwa mwezi haya mimi nitasema nyumba nimepanga 45M kwa mwezi ndio tunarudi kule jamaa kaorodhesha matimizi ananiwekea kodi 300,000/= serious na matumizi mengine ya kijinga.

Waafrika hatujui muda wa Making na muda wa Spending jamaa ame Spend sana muda ambao alitakiwa afanye making.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…