Msoto nimeuanza kitambo sana wakuu mpaka sasa napambana na bado sijaiona nuru.
1999-Kisanga kilianzia hapa.
Huu mwaka mambo yalizidi kuwa magumu sana kwa upande wa bi.mkubwa(mama),kipindi hicho nakaa na bi.mkubwa tu tumepanga nyumba ya bibi fulani ni mchawi balaa,yani full mauza uza hiyo nyumba.
Mambo yakazidi kuwa magumu balaa,bi.mkubwa akaona eeh hii ngoma ngumu,acha anipeleke kwa baba yangu (hapo tangu nazaliwa 199* sijawahi kumuona huyo wa kuitwa baba). Hata bi.mkubwa kuna muda alikua ananifanyia vitu hadi najiuliza huyu ni mama angu mzazi kweli?. Anyways tuyaache hayo..
Nakumbuka nilisafirishwa kutoka Bukoba-Rwamishenye mpaka Dodoma kama bahasha inavyoagizwa katika bus. Na kipindi hicho usafiri mkubwa ilikua ni meli mpaka Mwanza then train(gogo) mpaka Dodoma,to be the honest kipindi hicho nilikua na miaka 5.
Nilipofika Dom..
Kufika Dodoma nikakutana na mother wa kambo jau sanaaa,hapo ndio nikaanza kunyimwa msosi live huku nauona huu hapo,mixer vile visa vyote vya step mother nishapitia.
Njaa ilipozidi nikawa napita mitaani katika zile nyuma wanauza maandazi nje either ni barazani au pembezoni,nikawa naiba sana yale maandazi ya watu.
Ule mchezo ukaninogea,nikinyimwa msosi mi kwenda kufunua vindoo ya kachori na maandazi ya watu. Basi kuna siku nikanyimwa msosi tena na yule mother wa kambo nikapita katika machimbo yote ya maandazi na kachori nikakosa,nikarudi zangu home kinyonge sana, ni mida ya kama saa 1 kasoro night hiyo.
Kufika home nikakuta kuna mia mbili zile za noti( wahenga tunaenda sawa hapa) nikatembea na ile pesa wakuu,nikazama shop nikanunua zangu mazaga nikala.
Niliporudi home kilipigo nilichokutana nacho ni cha jibwa koko mpaka nikazima,yule mother akadhani kaua basi akataka aue soo kwa kunitupa katika kisima. Daah wakuu! hii dunia kuna watu wana roho mbaya kinomaaa,yani bila msaada wa majirani waliosikia kile kilio wakati napigwa bila shaka nisingekua naandika comment hii leo. (Nitakuja siku moja na thread kuelezea juu ya kunusurika kwangu kutupwa kisimani).
Kwa wakazi wa Dodoma waliokuepo kipindi kile bila shaka huu ukatili nilifanyiwa wa kutaka kutupwa kisimani ni lazma mliusikia,kwasababu iligeuka ni habari ya mji.
Baada ya lile tukio kuna ndugu alinichuka nikaishi nae,huku msoto ndipo ulikolea. Mwanzo mambo yalikua poa,ila baadae mkewe akaanza kunifanyia vimbwenga,mumewe akiwa kazini msosi sipewi,na mwanae anakula nikimtizama,na hakuna kushitaki kwa mumewe,thubutuuuuu.
Nikaona isiwe kesi,nikaanza kuokota vyuma,uza sana screpa,nikipata pesa nanunua juice ya unga ile(tulikua unaiita juice kola) nakoroga na mandazi nakula weee! Kitumbo ndiii!!
Kufikia darasa la saba nikawa nina energy ya kwa kias fulani,basi nikitoka shule nachukua mkweche wangu (baiskeli zile mnaziita Anita,ila inakua haina kiti cha nyuma wala zile gards za matope,haina vipra vya kukanyaga,ina misongo tu) au waweza kuuita "mfupa".
Basi bwana,huu mfupa nikawa naenda nao kubeba miwa huko bush,naifunga katika mwamba then narudi town kuiuza. Kuna kipindi nikawa mtoro sana shule,saa 4 tu sipo, niko road na mfupa wangu kuelekea kwa mzee Mtivike kulangua miwa.
2008
Hapa nilianza form one,kule kwa ndugu yangu wakawa kama wamenitelekeza hivi,yani niwe muwazi tu ambacho nilikuwa napata pale ilibaki kuwa ni mahala pa kulala tu pamoja na umri wangu mdogo.
Bahati mbaya katika kupangiwa shule nilipangiwa shule ya kata iliyo nje kiasi na mji,ilikua mpya hii.
Time ya kureport imefika mi niko niko tu mtaani kama chokoraa, nikijicheki sina pa kuanzia daah wakuu!! I remember nilizaka dox magari mabovu,watu wa Iringa wanapajua hapa nikadaka shati langu la langi nyeupe iliyokataa (dona), nikalifua fresh kesho nikatinga school na chini nina suruali ya home, tena kwa kuchelewa.
Nilifika pake kila teacher ana nishangaa tu kwasababu nilikua niko niko tu. Confidence ndio kitu nimejaaliwa,directly nikatamka kuwa nataka kuonana na mkuu wa shule, staff nzima wakaangua vicheko! Ila baadae nikaelekezwa ni wapi niende.
Nilipofika nikamdanganya kuwa mimi yatima na uongo mwingine mwingi tu mixer na ukweli kiasi ndani yake.
Kwa jinsi nilivyokua najieleza alitokea kunionea huruma sana,kwa kufupisha ni kwamba huyu mzee baadae alikua kama mfadhili wangu wa kimasomo.
Wakuu ng'ombe wa masikini hazai,akizaa anazaa dume tena asie zaa pia.
Basi bwana,yule mzee (headmaster) ambae alianza kunisaidia hakuchukua muda mrefu sana akafariki,ingawa hata kiafya hakua imara sana ila nilihisi ni pigo kwangu.
Kufikia form two hali ya kimaishanikaona inazid kuwa mbaya kwangu,na kipindi hicho nilikua nishaondoka pale home nikawa naishi ghetto na brother anafanya kazi ya kupakia mchanga,mawe,kokoto na tofali katika maroli (huyu brother nilikutana nae kipindi nauza miwa,nae alikua anauza miwa kama mimi kwa kipindi hicho).
Mimi wakati huo niko bize nauza pipi na bubble gum (tulikua tunaziita big jii/bablishi) kuanzia mtaani mpaka darasani.
Getto tulikua tunalipa 3000,ni chumba cha giza,hakuna maji wala choo,chini vumbi ila kitanda kilikuepo japo kidogo dogo. Kwa kifupi ilikua ni nyumba ambayo haijakamilika ujenzi, mitaa ya Kihodombi kanisani kwa chini katika yale maporomoko.
Baadae nikaamua na mimi kujiungana yule brother katika shughuli za kupakia mchanga,kokoto,tofali na mawe. Kituo chetu cha kazi ilikua ni hapo samora njia ya veta yalipokua yanapark maroli. Kijana mdogo nikapakia sana jiwe,pakia sana mchanga,kokoto na tofali...baadae nikawa mtoro shule,naenda mara mbili tu per week nabaki kitaa nikipiga hard works.
Nishachimba sana mchanga na kuchimba mawe huko Isakalilo,mapogoro mpaja kitasengwa(watu wa Iringa nadhani mnayajua haya maeneo).
Nishanusurika vifo na ulemavu mara kibao katika ajari za haya maroli , kuna muda mko mlimani huko porini roli lina kutana na kigongo cha maana then lina kua kama limezima ghafla! Kifuatacho hapo ni kuanza kuporomoka kinyume nyume! Hapo kila mtu anafanya jitihada za kuruka ili kuokoa maisha yake.
Mfano ni ajari fulani ilitutokea wakati tunapanda mlima wa kutokea chini huko wanapaita Zizi la Ng'ombe,dereva gari likamshinda katika corner akaingia bondeni gari miguu juu tukafunikwa humo,THANKS GOD nilitoka salama ingawa nilishudia kifo cha jamaa wa mkaa nae alipewa kama lift tu.
Mpaka namaliza kidato cha nne ni mambo mengi sana nilikua nishayafanya,ila siwezi kuyaweka hapa ili kufupisha story.
Nitaendelea...
Sent using
Jamii Forums mobile app