Wakati umepigika kazi gani ya ajabu uliwaza kufanya?

Wakati umepigika kazi gani ya ajabu uliwaza kufanya?

@kidukulilo akija kutoa ushuhuda wake mambo yatakuwa hivi:..

"Nimeteseka sana mimi..
Wakati nimemaliza shule pale IST nikaamua kuliko kukaa bure bora nitafute kazi
Nikaongea na mzee wangu anitafutie connection

Mzee akaniambia kuna issue canada nikasema sawa..
Nimeenda nikakuta kazi yenyewe ni kupanga mafile katika ofisi flani kwa masaa matatu kwa siku
Halafu mshahara wenyewe mdogo tu usd 300 kwa siku, nilisikitika sana...

niliteseka mimi, nyie acheni tu..

Ngoja aje humu[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]

Sent using Jamii Forums mobile app
Jama umeaua asee kwamba niliteseka mm...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bora Siku hizi kuna hata hizo Duplicator za milango 5, na printer za epson zilizo na original CISS. Mkuu zamani tukikuwa tunatumia desktop computer ku Burn CD CD moja moja, na HP kuprint CD moja moja . Nero ndio ilikuwa kiunganishi mhimu hapo
Mzee hujaprint cd 10000 zenye deadline siku moja machine inatoa pc 5 kwa 5 bado hujaweka cover halafu mpo watatu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ambao bado tupo kwenye stage ya kupigika nadhani tunaruhusiwa hapa!

Ni mwaka 2017 tu hapo mzee katimuliwa kazi hapo ndipo kila kitu kilipoharibika na nipo chuo,hapo niliuza hadi viatu na nguo mradi tu kitabu kiemde.

Hapo deni la ada linasoma 2.3mil...nikauza kila kitu cha thamani deni likasoma 1.1mil..na mwaka wa kuhitimu 2018 march huu hapa!!...na hii ni mwezi February!!!

Sijakaa vizuri barua hii hapa tayari nishatupwa nje ya chuo aisew wiki 2 kabla ya final..nilipambana mno bila mafanikio ikabidi tu nirudi chuoni na kuwapigia magoti hadi wakaniruhusu kuattend final kwa sharti la kushikilia vyeti hadi niwalipe chao...

Kuingia kitaa pagumu mno pagumu kwelikweli...kuna muda mtu mnakaa hata two days no chakula..msoto zikawa sio pasi ndefu tena bali crosi kabisa!

Nikaanza na kubangua korosho kiwanda fulani hivi...ndoo ndogo hii ukishabangua ukaijaza bado wanachambua zile zilizojeruhiwa hata kuparuzwa tu hazihesabiwi unakuta umejaza ndoo ndogo ila znazopimwa ni nusu ndoo tu....mbaya zaidi ukute unajaza ndoo mpja na nusu kwa wiki hivyo mwisho wa wiki unakuta una 6000 taha on hand..hapo inakulazimu tu kuchapa mguu huwezi toa nauli kwenye 6000 tshs issue ya kula ni pasi ndefuuuu...


Ilikuja kunishinda baada ya kuwa natapika kila nikivuta hewa na fukuto la mafuta ya korosho hivyo nikafurushwa..hapa nikaanza kusomba mchanga na kuuza kwa tshs 200 kwa kiroba,kubeba tofali,saidia fundi...muda kidogo nakuta mwili unazidi kuwa dhaifu hivyo nikastop vibarua vya kutumia nguvu.


Kwa vile fieled yangu ni mwalimu nikaanza kufundisha tuition pale home kila kichwa ni tshs 200 kwa siku na nilibahatika kuwa na vichwa 12...kazi ikafanyika na maisha ilibidi yaendelee tu.

Hivi karibuni kuna mmama kanipa kibarua cha houseboy...natamani iwe stori tu lakini kumbe ndio nipo katikati ya stori!

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu hii imenigusa sana! Mimi nmeanzia kwenye u house boy pia.

Japo mimi sijasoma kama wewe ila nilienda kusoma QT matokeo ya form 4 haya kutoka vizuri sana so ni kaamua kuachana na Habari za kusoma.

Kitu pekee ninachoshukuru nliambulia kufahamu lugha ya kingereza kwa sehemu na hiyo kingereza kimenisadia kusoma na kuelewa biashara ya mtandaoni forex.
Sasa hivi nahangaika na mtaji tu ila nikipata hata dola 500 basi nimetusua.

Komaa mkuu, mafanikio yako hayako mbali

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bora Siku hizi kuna hata hizo Duplicator za milango 5, na printer za epson zilizo na original CISS. Mkuu zamani tukikuwa tunatumia desktop computer ku Burn CD CD moja moja, na HP kuprint CD moja moja . Nero ndio ilikuwa kiunganishi mhimu hapo

Sent using Jamii Forums mobile app
Noma mzee..halafu lazima utest kua mzigo upo vizuri..hatari sana
 
Nakumbuka nimemaliza chuo2008 ,nikawa nipo tu home kila siku asubuhi baba wa kambo anafoka sana , na kuanza kutuambia msidhani mpo kwenye urithi wa malinzangu

Maneno yale yalikuwa yananiumiza sana ikanilazimu kwenda kutafuta kazi ya bar , nikawa counter pale kwenye bar

Yaani ugomvi matusi , kudharauli yote yakawa yangu ...usiku nalala mlemle kwenye bar sikutaka kirudi home kwa maneno yale ya mzee wetu!! Ila kazi ikawa na changamoto ukitembea tu na bamedi (sex)dharau zinaanza


Kipindi nipo pale bar nikabahatika kufahamiana na askari game watatu !! Wakawa mabest sana yaan hata kama hawana hela nawadhamini wanakunywa bia ,mwisho wa mwezi wanalipa ....

Wakanipa wazo si tuwe tunaenda na ww kwenye doria tukipata kitu tunakupa kidogo nikawaambia poa!! Ilikuwa ni kambi ya KIJERESHI

Ikawa ikifika uck km siku ya doria namuachia mdogo wangu wa pili ananisaidia kuuza pale bar ,maana tulikuwa kama makinda tukiugua mzee mara agome kutupeleka hospital ,nguo alikuwa hataki kbs ..kutuona tumevaa nguo nzuri [emoji24][emoji24][emoji24]

Tukawa tunaenda doria tukikutana na watu wameingia kwenye eneo la hifadhi tunawanyanganya kuni ,baskeli na kipigo juu kazi yangu ilikuwa kuigiza mizigo kwenye gari .....

Siku moja moja na wao walikuwa wanawinda nyati ,swala au nyumbu wananipa nyama naiuza ...napata hela kidogo kidogo natunza

Nilipokuwa mzoefu ......nikamfata gemu mmoja jina kapuni nikamwambia sasa si unifundishe kutumia bunduki tukawa tunaenda porin wananifundisha shabaa tukiwa tuna winda ..nikawa konki wa L4 ,kuitumia akanifundisha kuifuta na kuifungua

Baadae nikatafuta ya kukodi kwa mtu x alikuwa nayo na lisasi alikuwa akiniuzia moja sh 15000/- imeandikwa mzinga .ganda jekundu ..na zilikuwepo za kupigia tembo ganda jeusi ....ukimchapa na hiyo anaanguka

Nikaanza uharamia wa kuingia porini kwa kuwa nilikuwa na ratiba kamili ya askari game kufanya doria , nikawa nikikutana hata na mzoga wa mnyama nauchukua naupaka chumvi nyingi naukausha juani halafu ...nikirudi mjini natembeza mji kwa mji nyama ya porini watu walikuwa wakiipenda sana iliitwa vimoro

Nilitengeneza hela sana !! Tamaa ikanizidi bwana wakaja wasomali walielekezwa kuwa wakija kwangu hawatakwama njia nyingi nazijua

wanataka niwapeleke porini walikuwa na warundi na land cluzer ambayo ilikuwa na turbo na matenk mawili ...wakiwa na bunduki A.K 47 , NAbunduki moja inastand na mkanda wa risasi wakanilipa dola 250

Walikuwa na gari mbili kenta na land cruser tukaenda nao bwana tukapitia kijiji kinaitwa kijereshi tukaingia kwenye hifadhi ya serngeti

Ilikuwa mida ya saa moja saa tatu usiku jamaa walikuwa wana mwaga risasi kama karanga hawaangalia mnyama mkubwa mdogo !!

Baadae wakawa wanachambua wanyama wanatupia kwenye kenta mpk ikajaaa , kumbe askari game walisikia milio ya risasi wakaja aise ......zilitembezwa risasi na wale maharamia wa kisomali bunduki ilikuwa inashikiliwa na watu wawilo ....

Game wakazidiwa kabisa tukaondoka tukarudi mpk lamadi wakaniacha mida ya saa 8 usiku wakacha mwendo tokea hapo nikahapa sitakwenda porini

Maisha haya nikajikuta nimetengeneza km m1 ....yaani mpk naenda kulipot kazini tarehe 1-09-2009 ..
Nikawa nipo vizuri sana

Mafanikio ya mtu yanatengenezwa na kujitoa sadaka !! Siwez kusahau



sent from toyota Allex
Kama muvie vile kumbe ndio uhalisia yani.
 
Nilipomaliza cha nne,nkapata kazi ya kumenya viazi vya chips maeneo ya magomeni aiseee nlikuwa nameny viazi zaidi ya debe 6-8 per day home mambo yalikuwa magumu sana mother alisha dead tangu nkiwa form 2 so life home lilikuwa ngumu askuambie mtu mshua tungi tu daily
Nkawa naenda asubhi saa 12 nafanya usafi na kufungua goli nakoleza moto napika chai nakunywa then naanza kumenya viazi vyangu hiyo ngoma mpaka saa4 ucku salary 1500 per day

Sasa nkawa na demu wangu anasoma pale babtist sec,anaitwa mary mtot wa wa ushuani upanga magorofa ya BOT,na pale nnapofanya kazi ndio kituo chao cha kuja kula kiepe na mazaga zaga mengine nkaona ooooh isiwe kesi akifungua shule hapa akanikuta mm ndio namenya viazi ntazid kuongeza matatizo na papa ntaishia kuliskia kwenye bomba mkasepaa

Nkapata kazi ya kuuza glosary oale maeneo ya shecklango sinza ndani pale wanapochinja kuku kaglosary kenyew ukiuza sana unapata buk 3-5 na mm mshahara wangu ni chakula tu,so nkawa nakagua bia,soda,wine zilizo expare nazigida tu so full day nimelewa zangu sina habar naiba na krate naenda kuuza ela natombea stakagi shida mim....



Form six,nlipomaliza nkaenda kuwa saidia fundi aisee maeneo ya tegeta madale nilivuta bangi hasa nilichangantikiwa kabisa nkapewa jina nlikuwa naitwa "mother fucker" per day nlikuwa nakula 10000 so nkaona sio case nkawa namuhonga tu dem wangu mary huku najipakulia mtot taratibu

Nlipomaliza chuo nkatafuta kazi weee holla,nkarudi zangu saidia fundi kama kawaida kula 10 per day nkaona maisha ndio haya vuta mabangi sana nlikuwa na laptop nkauza nguo nzur nzur za kutoa mtu ukifika bei nauza staku shida za kingese mm .....
Nlipiga ile kazi nkaja nkapata kazi ya kuuza magodoro pale nyamala natuta mawili hapo ndio nkasettle nkawa napiga pesa nkanza na kuchepuka mary na yy anaona nazingua akapata bwana abafanya kazi airport akailewa ckuwah kushika 4ml za kwangu mm mwenywe ila kipindi hiyo nilizishika

Nkaja kuajiruwa na serekal na ndio umaskini ukaanzia hapo mpaka leo napata ela ya kula tu na watoto wanaenda shuke ila bado natembea na miguu sana and I am not happy at all

Mungu sio wa wote kila mtu apambane anavyojua ili mradi utoboe tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Baada ya muda mrefu kutaabika nkajikuta Sina kila kitu!yaani from hero to zero!!kitu pekee nlikua nimebaki nacho ni nyumba ila Sasa utakula nyumba?lazima maisha yaendelee! Nkauza nyumba nipate msingi Cha ajabu mtu aliyenipa wazo la biashara mpya ndie alinunua nyumba tena kwa kuilipia nusu nusu nkajikuta pesa imeisha na Niko ndani ya hiyo hiyo nyumba!!nkageuka kuwa mpangaji akaanza kuniomba Kodi ya nyumba

Sent using Jamii Forums mobile app
Binafsi kuuza nyumba ni hatua ya mwisho kabisa, tena sio kukosa chakula, nitauza kwa kitu kingine sio chakula

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom