Wakati umepigika kazi gani ya ajabu uliwaza kufanya?

Wakati umepigika kazi gani ya ajabu uliwaza kufanya?

Ambao bado tupo kwenye stage ya kupigika nadhani tunaruhusiwa hapa!

Ni mwaka 2017 tu hapo mzee katimuliwa kazi hapo ndipo kila kitu kilipoharibika na nipo chuo,hapo niliuza hadi viatu na nguo mradi tu kitabu kiemde.

Hapo deni la ada linasoma 2.3mil...nikauza kila kitu cha thamani deni likasoma 1.1mil..na mwaka wa kuhitimu 2018 march huu hapa!!...na hii ni mwezi February!!!

Sijakaa vizuri barua hii hapa tayari nishatupwa nje ya chuo aisew wiki 2 kabla ya final..nilipambana mno bila mafanikio ikabidi tu nirudi chuoni na kuwapigia magoti hadi wakaniruhusu kuattend final kwa sharti la kushikilia vyeti hadi niwalipe chao...

Kuingia kitaa pagumu mno pagumu kwelikweli...kuna muda mtu mnakaa hata two days no chakula..msoto zikawa sio pasi ndefu tena bali crosi kabisa!

Nikaanza na kubangua korosho kiwanda fulani hivi...ndoo ndogo hii ukishabangua ukaijaza bado wanachambua zile zilizojeruhiwa hata kuparuzwa tu hazihesabiwi unakuta umejaza ndoo ndogo ila znazopimwa ni nusu ndoo tu....mbaya zaidi ukute unajaza ndoo mpja na nusu kwa wiki hivyo mwisho wa wiki unakuta una 6000 taha on hand..hapo inakulazimu tu kuchapa mguu huwezi toa nauli kwenye 6000 tshs issue ya kula ni pasi ndefuuuu...


Ilikuja kunishinda baada ya kuwa natapika kila nikivuta hewa na fukuto la mafuta ya korosho hivyo nikafurushwa..hapa nikaanza kusomba mchanga na kuuza kwa tshs 200 kwa kiroba,kubeba tofali,saidia fundi...muda kidogo nakuta mwili unazidi kuwa dhaifu hivyo nikastop vibarua vya kutumia nguvu.


Kwa vile fieled yangu ni mwalimu nikaanza kufundisha tuition pale home kila kichwa ni tshs 200 kwa siku na nilibahatika kuwa na vichwa 12...kazi ikafanyika na maisha ilibidi yaendelee tu.

Hivi karibuni kuna mmama kanipa kibarua cha houseboy...natamani iwe stori tu lakini kumbe ndio nipo katikati ya stori!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahahha utawekwa kwenye hayo majeneza kabla ya wakati mkuu
Mie baada ya kufeli darasa la nne mara mbili nikaacha shule na kuanza wizi wa mafuta ya transfomer na baada ya miaka ikabidi nianze kujifunza kuchonga majeneza mpaka leo ndo biashara yangu mjini na nnagonga shavu kali za chuo na wake za watu

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukurasa wangu wa mapito sio mbaya sana na pia sio mzuri sana, naweza sema umenipa kujiamini na kujitegemea katika umri mdgo kabisa. Sikuwahi kuwaza kama ntafanya bodaboda, moja ya kazi ninaichukia hadi kesho. Nimefanya tax, nimelima, kazi za saidia fundi ujenzi, nimebadili noti feki bahati nzuri sikuwa kushikwa na mapoti, nimefanya udalali sana. Us**ge mwingine ni kufanya kazi porini kwa miezi 6 mfululizo kila aina ya wanyama wakali nimepishana nao
Duh hongera sana mkuu,hiyo ya kubadili noti feki mzee ni balaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aisee kupigika ni mbaya sana kipindi nimemaliza chuo niliangaika sana hapo Dar miaka ya 2002 bro wangu akanishauri nirudi home kijijini kuna minara ya voda inajengwa aniunganishie kazi ya ulinzi.Aisee sikuwa na namna akanitumia nauli ikawa mchana napiga kazi ya kibarua cha kumwaga zege hapo mnarani usiku naunganisha kulinda vifaa vya mnara nilipiga kazi km miezi minne la ilikuwa kazi ngumu halafu ni kijijini kwetu watu wanashaningaa mwanachuo kupiga kazi za hovyo but namshukuru bro alienipa wazo hilo Kwan nilitengeneza vihela plus wizi wa cement angalau kila siku mfuko mmoja mmoja haikuwa haba.Wale waliokuwa wananicheka wanashangaa baada ya mwaka narudi hapo kijijini na usafiri wa maaana kiasi plus na kuanza ujenzi wa nyumba ya mama yangu.


Sent using Jamii Forums mobile app
Hongera sana mkuu kwanza kwa kutokuchagua kazi,pili kwakuwa mjanja na mahesabu ya mbali (sio kwa kuiba cement[emoji3][emoji3])

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hongera kw akupambana mkuu usichoke na punguza uonga mambo yatakaa sawa.
Nilipohitimu Chuo nikawa sina hata mia, nakaa mpaka siku 3 sijala.

Mpaka nikilala, tumbo linahamia upande mmoja - Transcript, Academic, Enrolment na License natakiwa kulipia kama Tsh 200,000

Waswahili nao majungu mwanzo mwisho.

So, Nikawaza kwanini nisianze kuokota machupa.

Yaani Natoka Ukonga naenda hata Mburahati huko wasikonijua Naokota Nauza then narudi Jioni ?

Baada Ya Kutafakari sana, nikaghairi. Nikaingia Kampuni za ulinzi. Yaani gari zenyewe nilikuwa napata nauli kwa kuunga sana, na kwasababu ya njaa nusura siku moja nizimie kwenye daladala ( Kwasababu Ya Foleni na Kusimama )

Mpaka sasa niko huku mwaka wa pili huu.

Mimi ni mwoga sana ninapoona hakuna tumaini, huwa nakonda ghafla.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
2011 ilivyostishwa kazi yangu ktk kampuni nilipigika sana nikaamua kukimbilia katika kisiwa kimoja kilichopo ziwa victoria (Ikuza) nikiwa huko nilijikuta nimefanya kazi ambayo ni tamaa ya pesa

niliingia ktk hifadhi taifa ya rubondokinyume na taratibu kwenda kutega samaki usku wa manane nikiwa mgeni mimi pekee wenzangu walikua wenyeji siku nyingi walikua wakiingia ikiwa ndio malayangu ya tatu kuingia tulikamatwa na watu wa dolia gemu

kipondo tulichopewa ni cha mbwa koko miaka mi3jera hadi leo mguu wangu wa kulia una hitilafu

Sent using Jamii Forums mobile app
Pole sana mkuu,na wale jamaa wa hifadhi za wanyama naskia wana roho ngumu sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom