Wakati umepigika kazi gani ya ajabu uliwaza kufanya?

Wakati umepigika kazi gani ya ajabu uliwaza kufanya?

Mimi na x wangu tulimaliza chuo pamoja na wote tukawa tumefulia kipindi hatujapata kazi, kuna siku (Mpaka leo najuta sana) nilimwambia ajipeleke kwa x wake wa zamani ili mradi tupate kupitisha siku, maisha haya tunapitia mengi sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ilikuaje baada ya hapo?mliendlea kuwa pamoja?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mm nishakuwa mlinzi getini ktk nchi ya watu alafu pesa niliyokuwa nalipwa ni kama elfu50 ya kibongo na mwisho wa siku niliambulia risasi tu ya kiuno, staki kuandika mengi kuhusu hili jambo maana kila nnapoenda kuoga nikiliona hili kovu roho inaniuma sana.
Duh nchi gani hiyo mkuu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna kazi niliyokuwa naichukia na siipendi mpaka kesho japo wanaoifanya nawapenda na nawaheshimu saana! Sitaitaja kiuwazi ila kimaudhui wenye ufahamu wataelewa! Nilikuwa graduate fani tofauti na hiyo lakini nikajikuta natembea na bahasha kuomba toka ofisi moja hadi nyingine mwisho wa siku nikapata kuwapa maharifa form1. I seee! Nilivyokuwa nimepigika na nimekonda nilishukuru saana kupata japo hiyokazi na ulikuwa ndo mlango wa kupambana nikapata kamtaji nikaacha hiyo kazi na kuanza biashara iliyoniwezesha kutoboa kiasi fulani namshukuru Mungu!
Hongera.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukurasa wangu wa mapito sio mbaya sana na pia sio mzuri sana, naweza sema umenipa kujiamini na kujitegemea katika umri mdgo kabisa. Sikuwahi kuwaza kama ntafanya bodaboda, moja ya kazi ninaichukia hadi kesho. Nimefanya tax, nimelima, kazi za saidia fundi ujenzi, nimebadili noti feki bahati nzuri sikuwa kushikwa na mapoti, nimefanya udalali sana. Us**ge mwingine ni kufanya kazi porini kwa miezi 6 mfululizo kila aina ya wanyama wakali nimepishana nao
 
Aisee kupigika ni mbaya sana kipindi nimemaliza chuo niliangaika sana hapo Dar miaka ya 2002 bro wangu akanishauri nirudi home kijijini kuna minara ya voda inajengwa aniunganishie kazi ya ulinzi.Aisee sikuwa na namna akanitumia nauli ikawa mchana napiga kazi ya kibarua cha kumwaga zege hapo mnarani usiku naunganisha kulinda vifaa vya mnara nilipiga kazi km miezi minne la ilikuwa kazi ngumu halafu ni kijijini kwetu watu wanashaningaa mwanachuo kupiga kazi za hovyo but namshukuru bro alienipa wazo hilo Kwan nilitengeneza vihela plus wizi wa cement angalau kila siku mfuko mmoja mmoja haikuwa haba.Wale waliokuwa wananicheka wanashangaa baada ya mwaka narudi hapo kijijini na usafiri wa maaana kiasi plus na kuanza ujenzi wa nyumba ya mama yangu.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom