Wakati umepigika kazi gani ya ajabu uliwaza kufanya?

Wakati umepigika kazi gani ya ajabu uliwaza kufanya?

Niliwaza kudanga’ kua kibarua kwa mma ntilie japo zote hizo sikufanya

Ukiwa mwanafunzi tena wa chuo kuna kipindi unapigika haswaaa na ukizingatia msaada wa nyumbani ni mchache Au hamna kabisa.. ni wiki Tatu tu za kufulia ila zilinipeleka nikawa nawaza kaZi nyingi sana hadi kuingia ccm[emoji23][emoji23] kuna ile mikutano wanaccm wanaelewa
Wangekutoa ubongo ubaki kama @Wakudadavua

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Niliwaza kutoa tigo tight mpya Ila nikahisi mteja akiwa muhuni akinirusha,haya maisha jamani,usiombe uishiwe hata mkeo unaweza tamani umruhusu achepuke muishi,tufanyeji kazi kwa bidii siku zote za uhai wetu tukiwa na uthubtu wa maisha
Mimi na x wangu tulimaliza chuo pamoja na wote tukawa tumefulia kipindi hatujapata kazi, kuna siku (Mpaka leo najuta sana) nilimwambia ajipeleke kwa x wake wa zamani ili mradi tupate kupitisha siku, maisha haya tunapitia mengi sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mm nishakuwa mlinzi getini ktk nchi ya watu alafu pesa niliyokuwa nalipwa ni kama elfu50 ya kibongo na mwisho wa siku niliambulia risasi tu ya kiuno, staki kuandika mengi kuhusu hili jambo maana kila nnapoenda kuoga nikiliona hili kovu roho inaniuma sana.
 
Wakati nipo chuo life ilikua ngumu sana. Boom hilo hilo kula, kodi, umeme, maji bado sijavaa basi nikaona sio mbaya niunde biashara. Nikafikia conclusion nipike biriani niwe na deliver mwenyewe.

Basi siku ya jmosi nanunua vitu vyote, jumapili naanza kupika asubuhi mapema by saa 6 chakula kipo tayari. Napack vizuri kwenye take away. Hapo nishachukua order tayari.

Kimbembe kilikuaa Kwenye kufanya delivery. Uzuri wateja wengi walikua wanaishi karibu na chuo. Ila sasa nazunguka jua kali linanichoma yani. Hapo delivery ni bure. Niliweka free ili wateja wasione uvivu.

Sema regardless ya hustle ile bado nilikua na make profit. Nikipika biriyani elfu 30 nauza elfu 60. Sema nilifanya kwa mwezi tu nikaja nikapata zali (story for another day) ndo ikawa mwisho wa kupika mama ntilie.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimeuza ubuyu chuo. Wateja dharau mingi sana. Wanakopa kulipa deni mpaka ugomvi.

Nachukua ubuyu kwa babu issa packet moja 1000, naagiza packet 100 hiyo inakua tsh 100,000/=. Plus cost ya kusafirishia 20,000/=. Nikiuza mmoja 2000/= hapo faida napata kama 80,000/= it's alot faida nzuri. Sema nlikua nauza packet moja Hadi 4 kwa siku. Biashara ilikua slow lakini nikawa sikosi pesa ya kula kila siku

Changamoto niliokutana nayo kwenye hiyo biashara kuna mama mmoja nae alikua mwanachuo, mzanzibari yeye akamwambia mume wake amnunulie ubuyu nae awe ana uza. Akaja na mbwembwe eti anauza mmoja 1500/= mimi nikienda na wangu wa 2000/= wateja wanaleta dharau mbona flani anauza bei ya chini. Nikarudi zangu maskani nikakaa kuwaza sasa next step. Pesa naitaka lakini bei sitaki kushusha. Baada ya kuwaza na kuwazua nikaona sio mbaya nikaenda supermarket nikanunua vile vikopo vina mfuniko nikaja kufanya packaging, kwenye ile packet ya 2000/= mimi nikawa natoa vikopo vitatu, kila kopo nauza buku. So nikawa napata 3000/= nikamuacha yule shoct anauza 1500/= [emoji23][emoji23][emoji23]. Biashara ni akili asiee

Nilijaribu hadi kujifunza kupika kashata, nikanunua raw material zote , nikazama utube kucheki jinsi ya kupika kashata. Aisee hii ilinishinda kashata zilikua zinatoka ngumu kama mawe. Nikaachana nazo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwaka jana wakati nimefulia kodi nadaiwa, mfukoni hakuna kitu kuna jamaa yangu nikakutana nae akaniambia niende Somalia kutengeneza engine za boti kule mafundi wachache sana.

Nauli ya kufika Somalia ikawa tatizo kufika Kenya kwa kuunga ingewezekana. Kenya kwenda Somalia njia alizonipa ngumu sana.
Ikanibidi nibaki hapa hapa Tanzania.
 
Back
Top Bottom