Wakati umepigika kazi gani ya ajabu uliwaza kufanya?

Wakati umepigika kazi gani ya ajabu uliwaza kufanya?

ANKO JEI

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2018
Posts
1,319
Reaction score
2,504
Habari za muda huu wakuu, naimani mko poa na January inaendelea kuyoyoma. Naomba niende moja kwa moja kwenye swali langu.

Kwanza kabisa lazima tukubali kuna muda mtu unapigika na life hadi unaanza kuwaza kazi za ajabu au ambazo hukuwahi dhani utayafanya. Wengine wanafikia maamuzi na wanafanya, na wengine wanaishia kuwaza tu na kabla hawajafanya wanabadili maamuzi au wanapaka kazi nyingine ya kawaida.

Binafsi wakati nimemaliza elimu yangu ya hali ya juu Dar es salaam nilipitia wakati mgumu sana kimaisha kwani sikuwa na wakumtegemea. Nilikuwa napenda sana kuingia JF kujipotezea mawazo.

Siku moja nikakutana na uzi wa jamaa fulani akidai kuwa amepata mchongo wa kuigiza video za kikubwa huko majuu na akadai kuwa yeyote atayehitaji yupo tayari kumuunganishia.

Kiukweli nimelelewa vizuri tu lakini ilibaki kidogo tu nimtafute jamaa aniconnect nizame majuu. Lakini huwa napenda kufanya utafuti wa jambo kabla halijafanyika, hivyo nikazama Google kutafuta undani wa industry ya video za kikubwa.

Nikafahamu mengi sana, faida na hasara, gharama wanazolipa na mambo kibao, mwisho wa siku sauti ndani yangu ikawa inakataa sana hizo shughuli, basi nikaacha nikapambana kutafuta ishu nyingine.

Je wewe ni kazi gani ya ajabu kwako ulifikiria kuifanya kipindi ukiwa huna kazi na life limekunyoosha.

Karibuni.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna kazi niliyokuwa naichukia na siipendi mpaka kesho japo wanaoifanya nawapenda na nawaheshimu saana! Sitaitaja kiuwazi ila kimaudhui wenye ufahamu wataelewa!

Nilikuwa graduate fani tofauti na hiyo lakini nikajikuta natembea na bahasha kuomba toka ofisi moja hadi nyingine mwisho wa siku nikapata kuwapa maarifa form1. I seee!

Nilivyokuwa nimepigika na nimekonda nilishukuru saana kupata japo hiyo kazi na ulikuwa ndo mlango wa kupambana nikapata kamtaji nikaacha hiyo kazi na kuanza biashara iliyoniwezesha kutoboa kiasi fulani namshukuru Mungu!
 
1- Kuna jamaa nilikuwa nae kitaa ila yeye anatoka asubuhi (alfajir) kwenye saa 9 alafu anarudi saa 4 asubuhi anatutambia mtaani nikasema huyu jamaa anapiga kazi nzuri sana yaani masaa ma 4 karudi kitaa na mpunga fresh, basi kwa kuwa nilikuwa nimepigika na life nikamwambia jamaa anipe connection jamaa akaniambia kesho asubuhi na mapema njoo Kariakoo mitaa ya Sokoni kuna mtu nitakukutanisha nae.

Basi kesho yake lukwili nikaenda K/koo nikakutana na jamaa kumbe kazi yake ilikua ni kusambaza maziwa kwenye madumu ya Lita 20 unapakia mawili kwenye Baiskeli unawasambazia mama ntilie na vimigahawa vidogodogo vya mulemule K/koo.

Ilikua ni hardwork kwangu mimi maana nilikuwa si mzoefu kuendesha Baiskeli alafu ukizingatia maeneo ya K/koo jinsi kulivyo kuwa busy na watu asubuhi.

Nikamwambia jamaa ngoja nikafikirie basi sikurudi tena

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi sio kuwaza tu bali nlipigika tena nikiwa mdogo..

Ipo iv baada ya kumaliza la saba nlikataa kuendelea na shule nikazamia mjini nkapata kazi mshahara kwa mwezi 15k nkapiga kama mwaka nikawa na 180kb nkaona hyo kazi inanipotezea mda nkachukua hyo 180kb nkaenda lipia driving school nikiwa na miaka16 tu

Nkasoma kwa miezi kadhaa nkachukua cheti ila leseni nkaambiwa umri na kimo vinapishana na sheria za nchi,hapo iliniuma maana lengo langu lilikua nipate leseni nikatafute kazi ya kuendesha tax.

Nikarudi mtaan nmekaa kama siku mbili wazo likanijia niende garage nkajifunze kutengeneza magari huko ndio nlikutana na binadamu wasiokua na huruma ata chembe kwanza kumbuka hapa kabla ya kuruhusiwa kujifunza kuna form anatakiwa kujaza mzazi wako ili ata jek likifyatuka huko ukafa wao hawatahusika kwa chochote..

Nakumbuka nlipigika unaingia garage saa12 asubuhi ukiwahi sana kutoka ni saa5usiku na hulipwi ata mia ya pipi..

Gari lumekata spring ikichomelewa unatakiwa kuibeba mda huo huo haijalishi imepoa au haijapoa kuna siku sijui ni lichuma gani lizito lilikuja chomelewa af mm nlikua nmetoka ile narud tu nambiwa sogeza ilo chuma huku,kuja kushika nliungua mpaka ngozi za viganja zikabaki kwenye chuma..wala jamaa ni washenzi sana!

Kesho yake sikwenda garage nlibaki nyumban naugulia maumivu mda wote npo na ndoo ya maji barid nmeloweka huko mikono maana ilikua inawaka moto mbaya..

Baada ya siku mbili nkarudi kwa mwajiri wangu Wa 15k kwa mwezi mikono nyuma kama mateka akanihurumia nkaingia kazini japo sikuipenda ila sikua na chaguo tena..

Now wale walionitesa garage mm ndio mteja wao ata kama ni kopo la castle..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna kipindi nilipigika mpaka nikawa sielewi kesho yangu itakuwaje, basi asubuhi moja nikaenda zangu uwanjani kwenye mazoezi kama kawaida, nilipomaliza akanifuata mshkaji mmoja tunafanya nae mazoezi amezoea kuniita sister T, akaniambia natafuta mdad wa kazi za nyumbani! Nikamuuliza mshahara na kazi zake nikamwambia ngoja nikutafutie then ntakupa jibu...

Nikarudi home nikawaza weeee, kazi za ndani nikafanye ya kwenda na kurudi mpaka hapo nitakapopata uelekeo, basi nikamtext mshkaji kumuuliza kama wanahitaji wa kwenda na kurudi akasema hakuna shida maadam mke wake yupo home maana ndio ametoka kujifungua...

Nikamwambia basi mimi nipe hyo nafasi! Kwanza alimute alafu baadae akapiga kabisa na kuuliza, upo serious? Una tatizo gani? Kwa nini umeamua hvyo? Nikajieleza pale akasema hapana, siwezi kukuweka wewe uwe mtumishi wangu aisee! Nilisononeka pale lkn baada ya wiki akaniambia kuna mahali amenitafutia kwny duka la rafiki yake nikajishikize kwa muda mpaka mambo yangu yatakapokuw sawa!! Nikavuka
 
Back
Top Bottom