Bushmamy
JF-Expert Member
- Aug 18, 2019
- 11,208
- 20,517
Chezea mimi weweUnamuweza mandingo au jack napier au shane diesel?
Chezea mimi weweUnamuweza mandingo au jack napier au shane diesel?
Kutoa tigo!!! Duh..Niliwaza kutoa tigo tight mpya Ila nikahisi mteja akiwa muhuni akinirusha,haya maisha jamani,usiombe uishiwe hata mkeo unaweza tamani umruhusu achepuke muishi,tufanyeji kazi kwa bidii siku zote za uhai wetu tukiwa na uthubtu wa maisha
Kwa huu mwandiko wee bado ni mtoto wa mama[emoji41][emoji41]Meuza kuni mimi jamani, mbaya zaidi wanunuzi wanajiongezea kuni, wanalalamika ila namshukuru Mungu kwa kweli nilifanikiwa kuvuka salama kwenye mapito!
Daah pole sana mzee mi pia nimepitia Garage ila sikupata changamoto kama zako ila kweli hua hawakulipi kuna dogo nilimkuta hapo Garage ana miaka miwili analala kwenye magari katokea MtwaraMimi sio kuwaza tu bali nlipigika tena nikiwa mdogo..
Ipo iv baada ya kumaliza la saba nlikataa kuendelea na shule nikazamia mjini nkapata kazi mshahara kwa mwezi 15k nkapiga kama mwaka nikawa na 180kb nkaona hyo kazi inanipotezea mda nkachukua hyo 180kb nkaenda lipia driving school nikiwa na miaka16 tu
Nkasoma kwa miezi kadhaa nkachukua cheti ila leseni nkaambiwa umri na kimo vinapishana na sheria za nchi,hapo iliniuma maana lengo langu lilikua nipate leseni nikatafute kazi ya kuendesha tax.
Nikarudi mtaan nmekaa kama siku mbili wazo likanijia niende garage nkajifunze kutengeneza magari huko ndio nlikutana na binadamu wasiokua na huruma ata chembe kwanza kumbuka hapa kabla ya kuruhusiwa kujifunza kuna form anatakiwa kujaza mzazi wako ili ata jek likifyatuka huko ukafa wao hawatahusika kwa chochote..
Nakumbuka nlipigika unaingia garage saa12 asubuhi ukiwahi sana kutoka ni saa5usiku na hulipwi ata mia ya pipi..
Gari lumekata spring ikichomelewa unatakiwa kuibeba mda huo huo haijalishi imepoa au haijapoa kuna siku sijui ni lichuma gani lizito lilikuja chomelewa af mm nlikua nmetoka ile narud tu nambiwa sogeza ilo chuma huku,kuja kushika nliungua mpaka ngozi za viganja zikabaki kwenye chuma..wala jamaa ni washenzi sana!
Kesho yake sikwenda garage nlibaki nyumban naugulia maumivu mda wote npo na ndoo ya maji barid nmeloweka huko mikono maana ilikua inawaka moto mbaya..
Baada ya siku mbili nkarudi kwa mwajiri wangu Wa 15k kwa mwezi mikono nyuma kama mateka akanihurumia nkaingia kazini japo sikuipenda ila sikua na chaguo tena..
Now wale walionitesa garage mm ndio mteja wao ata kama ni kopo la castle..
Sent using Jamii Forums mobile app
Nimeroga sana na kuuza mizoga ya wafu
Jr[emoji769]
Kwa hiyo wewe unakaa kijiweni unaomba watu wafe ilo upate ulaji [emoji23]Mie baada ya kufeli darasa la nne mara mbili nikaacha shule na kuanza wizi wa mafuta ya transfomer na baada ya miaka ikabidi nianze kujifunza kuchonga majeneza mpaka leo ndo biashara yangu mjini na nnagonga shavu kali za chuo na wake za watu
Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna vipigo aisee huwezi hata kufanya hiyo kazi ya ajabuHabari za muda huu wakuu, naimani mko poa na January inaendelea kuyoyoma. Naomba niende moja kwa moja kwenye swali langu.
Kwanza kabisa lazima tukubali kuna muda mtu unapigika na life hadi unaanza kuwaza kazi za ajabu au ambazo hukuwahi dhani utayafanya. Wengine wanafikia maamuzi na wanafanya, na wengine wanaishia kuwaza tu na kabla hawajafanya wanabadili maamuzi au wanapaka kazi nyingine ya kawaida.
Binafsi wakati nimemaliza elimu yangu ya hali ya juu Dar es salaam nilipitia wakati mgumu sana kimaisha kwani sikuwa na wakumtegemea. Nilikuwa napenda sana kuingia JF kujipotezea mawazo.
Siku moja nikakutana na uzi wa jamaa fulani akidai kuwa amepata mchongo wa kuigiza video za kikubwa huko majuu na akadai kuwa yeyote atayehitaji yupo tayari kumuunganishia.
Kiukweli nimelelewa vizuri tu lakini ilibaki kidogo tu nimtafute jamaa aniconnect nizame majuu. Lakini huwa napenda kufanya utafuti wa jambo kabla halijafanyika, hivyo nikazama Google kutafuta undani wa industry ya video za kikubwa.
Nikafahamu mengi sana, faida na hasara, gharama wanazolipa na mambo kibao, mwisho wa siku sauti ndani yangu ikawa inakataa sana hizo shughuli, basi nikaacha nikapambana kutafuta ishu nyingine.
Je wewe ni kazi gani ya ajabu kwako ulifikiria kuifanya kipindi ukiwa huna kazi na life limekunyoosha.
Karibuni.
Sent using Jamii Forums mobile app
Wanakazi boxing day mtoto wa chuo unamkabidhi jeneza Kama zawadiKwa hiyo wewe unakaa kijiweni unaomba watu wafe ilo upate ulaji [emoji23]
Sent using Jamii Forums mobile app
Gerezani Siku hizi kuna intanenti unachati kabisa jf nin[emoji23][emoji23][emoji23]Nilipigika mpaka sio vizur nikaamua kuchinja mtu nikakae gerezan japo kuwa life la gereza sio poa
Ahsante. Kuna kipindi mambo yalikua mengi nikaacha. Now nimerudi tena nauza vitu vya kina dada.
Duuh, pole na hongera kwa kuvuka mkuuMimi sio kuwaza tu bali nlipigika tena nikiwa mdogo..
Ipo iv baada ya kumaliza la saba nlikataa kuendelea na shule nikazamia mjini nkapata kazi mshahara kwa mwezi 15k nkapiga kama mwaka nikawa na 180kb nkaona hyo kazi inanipotezea mda nkachukua hyo 180kb nkaenda lipia driving school nikiwa na miaka16 tu
Nkasoma kwa miezi kadhaa nkachukua cheti ila leseni nkaambiwa umri na kimo vinapishana na sheria za nchi,hapo iliniuma maana lengo langu lilikua nipate leseni nikatafute kazi ya kuendesha tax.
Nikarudi mtaan nmekaa kama siku mbili wazo likanijia niende garage nkajifunze kutengeneza magari huko ndio nlikutana na binadamu wasiokua na huruma ata chembe kwanza kumbuka hapa kabla ya kuruhusiwa kujifunza kuna form anatakiwa kujaza mzazi wako ili ata jek likifyatuka huko ukafa wao hawatahusika kwa chochote..
Nakumbuka nlipigika unaingia garage saa12 asubuhi ukiwahi sana kutoka ni saa5usiku na hulipwi ata mia ya pipi..
Gari lumekata spring ikichomelewa unatakiwa kuibeba mda huo huo haijalishi imepoa au haijapoa kuna siku sijui ni lichuma gani lizito lilikuja chomelewa af mm nlikua nmetoka ile narud tu nambiwa sogeza ilo chuma huku,kuja kushika nliungua mpaka ngozi za viganja zikabaki kwenye chuma..wala jamaa ni washenzi sana!
Kesho yake sikwenda garage nlibaki nyumban naugulia maumivu mda wote npo na ndoo ya maji barid nmeloweka huko mikono maana ilikua inawaka moto mbaya..
Baada ya siku mbili nkarudi kwa mwajiri wangu Wa 15k kwa mwezi mikono nyuma kama mateka akanihurumia nkaingia kazini japo sikuipenda ila sikua na chaguo tena..
Now wale walionitesa garage mm ndio mteja wao ata kama ni kopo la castle..
Sent using Jamii Forums mobile app
mlikuwa mnatumia kemikali?2011 ilivyostishwa kazi yangu ktk kampuni nilipigika sana nikaamua kukimbilia katika kisiwa kimoja kilichopo ziwa victoria (Ikuza) nikiwa huko nilijikuta nimefanya kazi ambayo ni tamaa ya pesa
niliingia ktk hifadhi taifa ya rubondokinyume na taratibu kwenda kutega samaki usku wa manane nikiwa mgeni mimi pekee wenzangu walikua wenyeji siku nyingi walikua wakiingia ikiwa ndio malayangu ya tatu kuingia tulikamatwa na watu wa dolia gemu
kipondo tulichopewa ni cha mbwa koko miaka mi3jera hadi leo mguu wangu wa kulia una hitilafu
Sent using Jamii Forums mobile app
Nimeroga sana na kuuza mizoga ya wafu
Jr[emoji769]
Mpaka leo bado unafanya ulinzi.Nilipohitimu Chuo nikawa sina hata mia, nakaa mpaka siku 3 sijala.
Mpaka nikilala, tumbo linahamia upande mmoja - Transcript, Academic, Enrolment na License natakiwa kulipia kama Tsh 200,000
Waswahili nao majungu mwanzo mwisho.
So, Nikawaza kwanini nisianze kuokota machupa.
Yaani Natoka Ukonga naenda hata Mburahati huko wasikonijua Naokota Nauza then narudi Jioni ?
Baada Ya Kutafakari sana, nikaghairi. Nikaingia Kampuni za ulinzi. Yaani gari zenyewe nilikuwa napata nauli kwa kuunga sana, na kwasababu ya njaa nusura siku moja nizimie kwenye daladala ( Kwasababu Ya Foleni na Kusimama )
Mpaka sasa niko huku mwaka wa pili huu.
Mimi ni mwoga sana ninapoona hakuna tumaini, huwa nakonda ghafla.