sawima
JF-Expert Member
- Jul 9, 2019
- 5,792
- 9,017
[emoji1][emoji1][emoji1]Posho za 5k’ 10k Au 20 mchezo[emoji23][emoji23] lazima uikumbuke tu kijua kikali tena jua la dodoma ila unakomaa tu na mikutano
Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji1][emoji1][emoji1]Posho za 5k’ 10k Au 20 mchezo[emoji23][emoji23] lazima uikumbuke tu kijua kikali tena jua la dodoma ila unakomaa tu na mikutano
Pole sanamm nishakuwa mlinzi getini ktk nchi ya watu alafu pesa niliyokuwa nalipwa ni kama elfu50 ya kibongo na mwisho wa siku niliambulia risasi tu ya kiuno, staki kuandika mengi kuhusu hili jambo maana kila nnapoenda kuoga nikiliona hili kovu roho inaniuma sana.
Pole sana mkuu,usikate tamaa zidi iupamvana tu mpaka mwisho.Ambao bado tupo kwenye stage ya kupigika nadhani tunaruhusiwa hapa!
Ni mwaka 2017 tu hapo mzee katimuliwa kazi hapo ndipo kila kitu kilipoharibika na nipo chuo,hapo niliuza hadi viatu na nguo mradi tu kitabu kiemde.
Hapo deni la ada linasoma 2.3mil...nikauza kila kitu cha thamani deni likasoma 1.1mil..na mwaka wa kuhitimu 2018 march huu hapa!!...na hii ni mwezi February!!!
Sijakaa vizuri barua hii hapa tayari nishatupwa nje ya chuo aisew wiki 2 kabla ya final..nilipambana mno bila mafanikio ikabidi tu nirudi chuoni na kuwapigia magoti hadi wakaniruhusu kuattend final kwa sharti la kushikilia vyeti hadi niwalipe chao...
Kuingia kitaa pagumu mno pagumu kwelikweli...kuna muda mtu mnakaa hata two days no chakula..msoto zikawa sio pasi ndefu tena bali crosi kabisa!
Nikaanza na kubangua korosho kiwanda fulani hivi...ndoo ndogo hii ukishabangua ukaijaza bado wanachambua zile zilizojeruhiwa hata kuparuzwa tu hazihesabiwi unakuta umejaza ndoo ndogo ila znazopimwa ni nusu ndoo tu....mbaya zaidi ukute unajaza ndoo mpja na nusu kwa wiki hivyo mwisho wa wiki unakuta una 6000 taha on hand..hapo inakulazimu tu kuchapa mguu huwezi toa nauli kwenye 6000 tshs issue ya kula ni pasi ndefuuuu...
Ilikuja kunishinda baada ya kuwa natapika kila nikivuta hewa na fukuto la mafuta ya korosho hivyo nikafurushwa..hapa nikaanza kusomba mchanga na kuuza kwa tshs 200 kwa kiroba,kubeba tofali,saidia fundi...muda kidogo nakuta mwili unazidi kuwa dhaifu hivyo nikastop vibarua vya kutumia nguvu.
Kwa vile fieled yangu ni mwalimu nikaanza kufundisha tuition pale home kila kichwa ni tshs 200 kwa siku na nilibahatika kuwa na vichwa 12...kazi ikafanyika na maisha ilibidi yaendelee tu.
Hivi karibuni kuna mmama kanipa kibarua cha houseboy...natamani iwe stori tu lakini kumbe ndio nipo katikati ya stori!
Sent using Jamii Forums mobile app
Yaani utoe tako kabisaaa?? Mungu turehemu, twakuomba utusikieNiliwaza kutoa tigo tight mpya Ila nikahisi mteja akiwa muhuni akinirusha,haya maisha jamani,usiombe uishiwe hata mkeo unaweza tamani umruhusu achepuke muishi,tufanyeji kazi kwa bidii siku zote za uhai wetu tukiwa na uthubtu wa maisha
Nilihofia wangenisaka hadi mtaani kwangu.Kwani ungeingia mitini na hiyo hela na hivyo vifaa wangekupata wapi??
Sent using Jamii Forums mobile app
Mbona kama hujaeleweka embu funguka mkuu,washika dau wap humu humu ndan[emoji848][emoji848]Niliwaza kutoa tigo tight mpya Ila nikahisi mteja akiwa muhuni akinirusha,haya maisha jamani,usiombe uishiwe hata mkeo unaweza tamani umruhusu achepuke muishi,tufanyeji kazi kwa bidii siku zote za uhai wetu tukiwa na uthubtu wa maisha
Babu unajibizana na Delicious soma alama za nyakati [emoji44][emoji44]Kitufe xha mduara ila usijeniroga
Mshahara wanalipa ngapi?Nafanya KK ( GardaWorld )
Hizi kazi huwa ni mapito tu na siyo sehemu ya kufanya kwa muda mrefu.
Zikifika mwisho zenyewe, achana nazo. Usitumie nguvu kubwa sana kulazimisha kubaki kazini, kwasababu ni kazi za hatari na zisizo na future.
Binafsi, Nilitaka kupumzika mwaka jana mwezi wa 6 ila nikaona nifanye mpango kwanza nikope kama 1.6M then niilipie kwa kutumia kazi hii mpaka mwakani mwezi wa 3, then nishanye mambo yangu mengine.
Mwaka jana nilijitutumua nikalima mihogo kama ekari 6 haikurudi hata 100 !
So, Challenges nyingi sana na kila unapopambana na zenyewe zinaongezeka.
Nyambiza jr
Poleee,hio mistari 2 ya mwisho noma sanaAisee, nakumbuka chuo boom limekata maisha magumu mno, nikafikiria nifanyaje, nikapata mawazo ya biashara nikaanza...
kuuza bubblegum/bigijii hizi super golila @500, nikanunua 8000 pakti ukiuza faida ni 5000 hivi, nashukuru ilikua tukienda class kabla lecture haijaanza nawatangangizia nnazo so wanachukua fresh,namaliza hata pkt 2 per day.
Nikaona niongeze biashara ya biscuits fulani hivi tamuu, nilikua nanunua pakti ya biscuit sh 900 nakuja kuuza 2000/=
Nikaongeza biashara ya crips za ndizi, nilikua napika mwenyewe nakumbuka nilikua nakaa hostel na hamruhusiwi kupika, so nikamuomba rafiki yangu alikua amepanga nje ya hostel nikawa napikia huko, nakumbuka siku ya kwanza nimepika crips hazikukauka vizuri dah,lainii kufika nazo hostel roommates wakanichekaa ila nilikomaa nikaziuza zingine nikawapa wale tu, siku 2, nikapika zimeungua nilikua nashindwa kukadiria moto, baada ya hapo nikawa napika vizurii, nikapeleka hadi blocks za wakaka faster zinaisha, napigiwa simu nipeleke zingine kama zipo hadi raha, faida ilikua ni nusu kwa nusu.
Nakumbuka nilikusanya faida hadi nikapata mtaji wa viatu flani vya kimasai ambao ulinisaidia hadi nilivomaliza chuo nikaendelea nao, nikafanikiwa kusave hadi sh 70,000/= per week kwa hiyo biashara,nakumbuka nilikua namsaidia hadi babe wangu vihela kidogo vya vocha,kabla hajapata kazi, japo alikuja akaniacha mfyuuu zake. Changamoto humpa mtu akili aisee.
Sent using Jamii Forums mobile app
Am serious usisaau kunambia hilo deal.Mie nimeliona km bonge ya deal...naomb niconfirm kwanza...maana niligeuka mwandishi wa habari kuhoji...then ntakurudia...means ukiwa serious kwa siku unapata kuanzia 50!...sio migodini(usiogope)
Poa...!
Ss hivi unapiga mishe gani?Maisha haya nyie acheni nakumbuka nimemalixa chuo nasubir post halafu mfukoni sina kitu .....kila unapoenda kutafuta kujisikiza wanataka uchi kwanza!! [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Kuna dada tulikuwa nao mtaani jioni wanachomoka ....asubuh wanarudi wako vxuri nikawaambia wanisaidie kupata kazi
Wakaniambia kazi ipo vizano hotel ..mmmh kufika kumbe wanafanya kazi ya kujiuza .....halafu kuna mwarabu akawa ameniganda kweli si jui alihic mi mgeni maeneo yale yaani niliondoka kwa miguu hadi nyakato meko
Kesho yake nikatafuta kazi ya kuhudumia kwenye migahawa maeneo ya pale nundu...nikafanya kama miezi miwili nikapata ajira xikatoka ndio nikawa nimevuka du[emoji847]
Sent using i phone x
Hahaaa, ilikua kipindi hicho mkuu now sina ideas za utafutaji tena.vp saiv umeolewa au nijichukulie mwenyewe ninaetambua thamani yko
Sent using Jamii Forums mobile app
Ilikua 2013 wakati nasubiri matokeo ya kidato cha nne kama sikosei ilikua mwezi january.Kutokana na ukata wa kukaa home mda mrefu huku nikikosa hata pesa za vocha na bi mother akiwa amepigika nikawa nina njaa iliokithiri(sio njaa ya kula njaa ya hela).
Jioni ya siku moja kabala ya tukio mshikaji wangu Dullah akaniambia amepata kazi ya ukarani kwenye ghala la korosho kesho yake anaanza,nikamwambia basi nami anifanyie mpango akasema sawa atajaribu.
Siku ya tukio niko zangu home asubuhi kama saa 7 na dk kadhaa.,Dullah akaja kuniita nikatoka nje nikakutana na huyo mama tukawa watatu mimi,mama na dula,mazungumzo yalikua hivi.
Mama: hujambo?
Mimi: sijambo shikamoo
Mama: dulla ameniambia na wewe unataka kazi ndo nikamtum aje kukuita,kama upo tayari tuongozane.
Mimi : ndio mama nipo tayari na kwakua nimeshanawa ngoja nivae tu simpo twende(mpaka hapa nikajua ukarani)
Njiani yule mama akatuuliza "hivi mmekunywa chai?" Sisi tukamjibu kwa pamoja "bado"...mara akasema "eeee msije mkaniangukia huko,tukifika nitawanunulia chai"..nikauliza "kwani mama ni kazi gani,si kuandika tu"? Sikujibiwa ,mara paap nitakuwa tumefika kiwanda(ghala) cha korosho pale mbagala kokoto.Kweli akatuagizia chai na chapati mbili mbili,wakati nakunywa chai nilikuatana na jamaa mmoja anaitwa robert(nilimzoea kwa jina la jirani) ikabidi aniulize vipi dogo mbona uko hapa ? Nikamjibu "nimekuja kufanya kazi bro humo kiwandani" akasema utaweza ndugu yangu kubeba gunia za korosho ? Nikamjibu mimi sibebi gunia tumeambiwa tutakua makarani.
Mara saa 2:30 ikafika tukawa tumeingia tukaambiwa tubadilishe nguo tukavaa za kazi(hapa kichwani niakanza kujawa na masawali) Yule jirani akasema haya dogo karibu jilehanam..aisee gunia(kiroba) la kwanza likaenda la pili likaishia kati wahindi wakaanza kupiga kelelenimemwaga korosho na kuchana kiroba. Ikabidi nihamishe kwenye kupakia korosho maana kubeba siwezi huko nako ilikua balaa gunia zilikua nyingi balaa halafu hakuna vitendea kazi hakuna mask wala gloves mikono ilichubuka.Yule Dullah mara akapokea simu(ya uongo) ghafla nikamuona anaanza kulia akaulizwa kulikoni akasema amefiwa na babu yake doh ikabidi aruhusiwe asepe nikawa nimebaki mimi na wengine.Mpaka kufika saa 6 mchana niko hoi tukahamishiwa kiwanda kingine kubeba gunia tupu ili ziletwe huku zipakiwe aisee ilikua balaa gunia zina vumbi nikaishiwa nguvu kwa kukisa hewa ikabidi nitolewe nje ya stoo...
Baada ya hapo tukarudishwa kiwanda kile cha mwanzo kwa ajili ya kuendelea kupakia mpaka kufika huo muda nikikohoa natoa kohozi jeusi nikipenga kamasi hivyo hivyo nikasema hapa hapa ngoja nitoroke..walinzi wakaniuliza unaenda wapi nikasema nimeagizwa mmoja akauliza mbona u ebeba na nguo zako sikuangalia nyuma nikawa nishafungua mlango nikaondoka.Kufika home kifua na mwili unaniuma nakohoa balaa nikamuona Dullah aliponiona alicheka sana akasema yeye hakufiwa ila aliona kazi imemshinda alitafuta kisingizio.Ilipofika saa 1 usiku akaja yule mama kuniulizia akasema mbona nimeondoka sijaaga na hela sikuchukua,nikamuuliza hiyo hela hapo unayo? Akasema hana kaicha nikaifuate kesho yake nikamjibu hapana nimesamehe...wiki nzima niliumwa kifua na mwili na tangu siku hiyo nikaapa sitakuja kufanya kazi kwa muhindi wale jamaa ni wauwaji kazi kubwa vifaa hakuna au duni.
Ndefu samahani.
Sent using Jamii Forums mobile app
Ilikua kipindi hicho mkuu.[emoji849]Natufata mke mpambanaji kama wewe[emoji6][emoji846]