Wakati umepigika kazi gani ya ajabu uliwaza kufanya?

Wakati umepigika kazi gani ya ajabu uliwaza kufanya?

Mimi sio kuwaza tu bali nlipigika tena nikiwa mdogo..

Ipo iv baada ya kumaliza la saba nlikataa kuendelea na shule nikazamia mjini nkapata kazi mshahara kwa mwezi 15k nkapiga kama mwaka nikawa na 180kb nkaona hyo kazi inanipotezea mda nkachukua hyo 180kb nkaenda lipia driving school nikiwa na miaka16 tu

Nkasoma kwa miezi kadhaa nkachukua cheti ila leseni nkaambiwa umri na kimo vinapishana na sheria za nchi,hapo iliniuma maana lengo langu lilikua nipate leseni nikatafute kazi ya kuendesha tax.

Nikarudi mtaan nmekaa kama siku mbili wazo likanijia niende garage nkajifunze kutengeneza magari huko ndio nlikutana na binadamu wasiokua na huruma ata chembe kwanza kumbuka hapa kabla ya kuruhusiwa kujifunza kuna form anatakiwa kujaza mzazi wako ili ata jek likifyatuka huko ukafa wao hawatahusika kwa chochote..

Nakumbuka nlipigika unaingia garage saa12 asubuhi ukiwahi sana kutoka ni saa5usiku na hulipwi ata mia ya pipi..

Gari lumekata spring ikichomelewa unatakiwa kuibeba mda huo huo haijalishi imepoa au haijapoa kuna siku sijui ni lichuma gani lizito lilikuja chomelewa af mm nlikua nmetoka ile narud tu nambiwa sogeza ilo chuma huku,kuja kushika nliungua mpaka ngozi za viganja zikabaki kwenye chuma..wala jamaa ni washenzi sana!

Kesho yake sikwenda garage nlibaki nyumban naugulia maumivu mda wote npo na ndoo ya maji barid nmeloweka huko mikono maana ilikua inawaka moto mbaya..

Baada ya siku mbili nkarudi kwa mwajiri wangu Wa 15k kwa mwezi mikono nyuma kama mateka akanihurumia nkaingia kazini japo sikuipenda ila sikua na chaguo tena..

Now wale walionitesa garage mm ndio mteja wao ata kama ni kopo la castle..

Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] hayo yanaitwa ni mateso bila chuki

sent from toyota Allex
 
Niliwaza kutoa tigo tight mpya Ila nikahisi mteja akiwa muhuni akinirusha,haya maisha jamani,usiombe uishiwe hata mkeo unaweza tamani umruhusu achepuke muishi,tufanyeji kazi kwa bidii siku zote za uhai wetu tukiwa na uthubtu wa maisha
Najifunza vitu aise

sent from toyota Allex
 
Nilikuwa nasubiri nione madada aliyewaza kuuza papuchi

Niliwaza kudanga’ kua kibarua kwa mma ntilie japo zote hizo sikufanya

Ukiwa mwanafunzi tena wa chuo kuna kipindi unapigika haswaaa na ukizingatia msaada wa nyumbani ni mchache Au hamna kabisa.. ni wiki Tatu tu za kufulia ila zilinipeleka nikawa nawaza kaZi nyingi sana hadi kuingia ccm[emoji23][emoji23] kuna ile mikutano wanaccm wanaelewa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mie baada ya kufeli darasa la nne mara mbili nikaacha shule na kuanza wizi wa mafuta ya transfomer na baada ya miaka ikabidi nianze kujifunza kuchonga majeneza mpaka leo ndo biashara yangu mjini na nnagonga shavu kali za chuo na wake za watu

Sent using Jamii Forums mobile app
kweli unamaendeleo unagonga pisi za chuo na wake za watu . we hatari sana

kitochi
 
Why hilo kovu linaonekana wkt wa kuogo tu? Mf ukiwa unakula MZIGO halionekani?
mm nishakuwa mlinzi getini ktk nchi ya watu alafu pesa niliyokuwa nalipwa ni kama elfu50 ya kibongo na mwisho wa siku niliambulia risasi tu ya kiuno, staki kuandika mengi kuhusu hili jambo maana kila nnapoenda kuoga nikiliona hili kovu roho inaniuma sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna kuzibua VYOO!
Afu kuna kuzibua MITARO!

Sent using Jamii Forums mobile app
Ilikuwa chemba.... Siku hyo tulipigika sana
Mara tukashuka mitaa ya kinondoni road tukakutana na mwanetu mmja smdy Jose gama
Akatuambia anakwenda dssd pale mwmbe jini
Kuwaita wazibua chemba maana kwao limeziba
Ah tu kamwambia we Vp hyo Kazi si utupe fasta tukachkua mipira mirefu tu kaenda kwa mzee Gama tukazibua chmba wacha tucheze na minyesi lkn tulikuwa mpunga mzuri
Maana siku hyo ilikuwa hata tsh 20 hakuna mfukoni

Ova

Sent using Jamii Forums mobile app
 
vp saiv umeolewa au nijichukulie mwenyewe ninaetambua thamani yko
Aisee, nakumbuka chuo boom limekata maisha magumu mno, nikafikiria nifanyaje, nikapata mawazo ya biashara nikaanza...
kuuza bubblegum/bigijii hizi super golila @500, nikanunua 8000 pakti ukiuza faida ni 5000 hivi, nashukuru ilikua tukienda class kabla lecture haijaanza nawatangangizia nnazo so wanachukua fresh,namaliza hata pkt 2 per day.

Nikaona niongeze biashara ya biscuits fulani hivi tamuu, nilikua nanunua pakti ya biscuit sh 900 nakuja kuuza 2000/=

Nikaongeza biashara ya crips za ndizi, nilikua napika mwenyewe nakumbuka nilikua nakaa hostel na hamruhusiwi kupika, so nikamuomba rafiki yangu alikua amepanga nje ya hostel nikawa napikia huko, nakumbuka siku ya kwanza nimepika crips hazikukauka vizuri dah,lainii kufika nazo hostel roommates wakanichekaa ila nilikomaa nikaziuza zingine nikawapa wale tu, siku 2, nikapika zimeungua nilikua nashindwa kukadiria moto, baada ya hapo nikawa napika vizurii, nikapeleka hadi blocks za wakaka faster zinaisha, napigiwa simu nipeleke zingine kama zipo hadi raha, faida ilikua ni nusu kwa nusu.

Nakumbuka nilikusanya faida hadi nikapata mtaji wa viatu flani vya kimasai ambao ulinisaidia hadi nilivomaliza chuo nikaendelea nao, nikafanikiwa kusave hadi sh 70,000/= per week kwa hiyo biashara,nakumbuka nilikua namsaidia hadi babe wangu vihela kidogo vya vocha,kabla hajapata kazi, japo alikuja akaniacha mfyuuu zake. Changamoto humpa mtu akili aisee.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mm safari yng ya kwanza SOUTH AFRICA, nilipigika kinyama baada ya jamaa aliepaswa kunipokea kuingia mitini... Msamaria mwema mmoja akanipeleka Masjid Habibbiyah - Cape Town... Hapo kazi ilikuwa kusafisha Msikiti na Mazingira yake... Kula Kulala humo humo... Bureeee...

Ngoja kwanza nishuke kwenye daladala ntarudi...!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimeuza ubuyu chuo. Wateja dharau mingi sana. Wanakopa kulipa deni mpaka ugomvi.

Nachukua ubuyu kwa babu issa packet moja 1000, naagiza packet 100 hiyo inakua tsh 100,000/=. Plus cost ya kusafirishia 20,000/=. Nikiuza mmoja 2000/= hapo faida napata kama 80,000/= it's alot faida nzuri. Sema nlikua nauza packet moja Hadi 4 kwa siku. Biashara ilikua slow lakini nikawa sikosi pesa ya kula kila siku

Changamoto niliokutana nayo kwenye hiyo biashara kuna mama mmoja nae alikua mwanachuo, mzanzibari yeye akamwambia mume wake amnunulie ubuyu nae awe ana uza. Akaja na mbwembwe eti anauza mmoja 1500/= mimi nikienda na wangu wa 2000/= wateja wanaleta dharau mbona flani anauza bei ya chini. Nikarudi zangu maskani nikakaa kuwaza sasa next step. Pesa naitaka lakini bei sitaki kushusha. Baada ya kuwaza na kuwazua nikaona sio mbaya nikaenda supermarket nikanunua vile vikopo vina mfuniko nikaja kufanya packaging, kwenye ile packet ya 2000/= mimi nikawa natoa vikopo vitatu, kila kopo nauza buku. So nikawa napata 3000/= nikamuacha yule shoct anauza 1500/= [emoji23][emoji23][emoji23]. Biashara ni akili asiee

Nilijaribu hadi kujifunza kupika kashata, nikanunua raw material zote , nikazama utube kucheki jinsi ya kupika kashata. Aisee hii ilinishinda kashata zilikua zinatoka ngumu kama mawe. Nikaachana nazo.

Sent using Jamii Forums mobile app
I wish nikuonee... Such a brilliant and smart woman...!! Nimekupenda sana aisee ni moja ya wanawake smart sana japo sijawahi kukuona but upo creative sana salute

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom