Wakati umepigika kazi gani ya ajabu uliwaza kufanya?

Wakati umepigika kazi gani ya ajabu uliwaza kufanya?

Baada ya muda mrefu kutaabika nkajikuta Sina kila kitu!yaani from hero to zero!!kitu pekee nlikua nimebaki nacho ni nyumba ila Sasa utakula nyumba?lazima maisha yaendelee! Nkauza nyumba nipate msingi Cha ajabu mtu aliyenipa wazo la biashara mpya ndie alinunua nyumba tena kwa kuilipia nusu nusu nkajikuta pesa imeisha na Niko ndani ya hiyo hiyo nyumba!!nkageuka kuwa mpangaji akaanza kuniomba Kodi ya nyumba

Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16],we ndo pumbafuu kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilipokuwa chuo mwaka wa pili, bum limekata home siwezi kuomba kwani nilikuwa najisomesha mwenyewe . Nikafikiria nikaona nikipata bum nikanunue jezi niwe nauza, biashara ikakubali ikawa inanilipa, ghafla mtaji ukakakata nyumbani kulikuwa na mamatatizo ikanilazimu kusolve. Nakumbuka siku hiyo ilikuwa alhamis nili lala njaa. Ijumaa naamka njaa yaniuma vibaya Sana utumbo unawasha halafu Sina ramani ya kupata pesa.siku hiyo nikamkumbuka mungu niaksema wacha niende masjid na Leo ijumaa. Nikaenda msikiti mmoja uko town msikiti wa waarabu. Sasa bhana Yule sheikh wa pale msikitini akajichanganya akaniona mstaarabu sijui kwa kuwa navaa miwani ya macho. Akanipa bahasha ya kaki akaniomba nisimame mlangoni Ili waumini wakiingia kusali waweke sadaka kwenye Ile bahasha ya kaki. Nikasimama waumini wakioita wanaupia sadaka mpaka muda wa khotuba ulipofuka nikaenda kukaa nisikize khotuba. Happy njaa inauma utumbo na akili havikuwana ushirikiano. Utumbo unawasha, kichwani naona Kama wadudu wanatembea. Nikaenda chooni haja ndogo, nilipomaliza nikaitoa Ile bahasha kuifungua nakuta noti za 10000 za kutosha. Akili ikanambia to " Mungu ana samehe Saba mara sabini, utakufaa njaa kizembe " Sikuhesabu nikapita na misimbazi 3( 30000) nikarudi ndani msikitini .Tulipomaliza kusali fasta nikamfuata Yule sheikh nikamkabidhi bahasha yake nikamwambia nawahi chuo. Akapokea, nikatembea sikugeuka nyuma.

Mungu atusamehe kwa kweli, kupigika kubaya
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16], huyo sheikh alikuwa mwarabu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mm safari yng ya kwanza SOUTH AFRICA, nilipigika kinyama baada ya jamaa aliepaswa kunipokea kuingia mitini... Msamaria mwema mmoja akanipeleka Masjid Habibbiyah - Cape Town... Hapo kazi ilikuwa kusafisha Msikiti na Mazingira yake... Kula Kulala humo humo... Bureeee...

Ngoja kwanza nishuke kwenye daladala ntarudi...!

Sent using Jamii Forums mobile app
Naisubiri hii kwa hamu
 
Dah kumbe tuko wengi nilidhani ni mimi tuu, usikate tamaa mkuu. Me nimemalizwa kabisaa bora ww sasa unayo hata nafasi ya kukimbizana na wanyam wakali me nimelala tuu muda huu. Lakini usikate tamaa tafta njia mpya, zipo njia utatoka tuu me bado nina imani ndio maana sijajiua mpaka sasa? Mungu ni mmoja tu.
una mchongo gani now

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ngoja niwape story ya kuuza chuma na ilivyonipitisha njia ya kifo

Early 2000s nikiwa ninakaribia kumaliza primary ninaishi na bibi yangu Moshi mjini mzee na mama walitengana kitambo ikaishia mama akaniacha na bibi pia akaenda kutafuta maisha nje ya nchi mshua yupo dar na mke mwingine anachojali yeye ni kulipa ada tuu

Mwezi mmoja kabla sijamaliza primary bibi akavuta, tulikuwa na maisha ya wastani sikuwahi kukosa kitu kwa bibi yangu mzaa mama, nyumba ni ya ukoo ikaamuliwa aje akae mdogo wake bibi yangu hapo ndio msoto ulipoanza sasa, mke wa mzee hakuwahi kupenda mimi kwenda kwake na sikuwahi kwenda life lilichange ghafla, nikaanza kujiongeza nikikosa kitu na ninajua mama yangu katuma hela ninapanga namna ya kumpiga bibi asiyejali, nikashtukiwa hawakupata ushahidi, ilabidi niingie rasmi kwenye biashara ya vyuma chakavu nilianza kwa kukusanya mwenyewe kwa sababu ilikuwa ndio trend, nikaona siwezi hii kitu kwa umri uke kubeba kilo 15 ni ishu, nilichofanya ni kutafuta machimbo nanamkodii muendesha toroli mlevi mlevi tunaenda nnajaza mkokoteni tunaenda kuuza nnampa chake anasepa... 2003 nikaingia rasmi o level,

Hapo nikaenda na tabia zangu za kusaka hela, nikaja kupigwa suspension kwa kuvunja viti vya shule na kuuza km skrepa huko mtaani nina wafanya kazi wangu ninawatuma kufuata mzigo mahali wnapima wananipa changu nilikuwa nna deal na garages

Iyo siku nikajichanganya nikaenda kwenye garage moja ya waarabu wana majini tukakubaliana kabisa price ya vyuma na hela nnayotakiwa kuwalipa nikawapa advance kabisa ikabidi iyo siku nikasimamie show mwenyewe sijaenda shule kabisa, dah tumeingia wote na wafanyakazi wangu tukashangaa geti linafungwa jamaa wanaanza kutu attack wanarusha vyuma iyo siku niliona kifo hiki hapa hapo waarabu wamekaa juu watanzania wenzetu ndio wanatupiga, tulipambana, hamna aliyekufa ila tuliwavunja viungo nao walituvunja...nikaachana rasmi na hiyo biashara nikahamia kwenye car wash na grocery
majini kivipi??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Oooh kumbe ni wewe ulikua unatuuzua clips hostel.
Aisee, nakumbuka chuo boom limekata maisha magumu mno, nikafikiria nifanyaje, nikapata mawazo ya biashara nikaanza...
kuuza bubblegum/bigijii hizi super golila @500, nikanunua 8000 pakti ukiuza faida ni 5000 hivi, nashukuru ilikua tukienda class kabla lecture haijaanza nawatangangizia nnazo so wanachukua fresh,namaliza hata pkt 2 per day.

Nikaona niongeze biashara ya biscuits fulani hivi tamuu, nilikua nanunua pakti ya biscuit sh 900 nakuja kuuza 2000/=

Nikaongeza biashara ya crips za ndizi, nilikua napika mwenyewe nakumbuka nilikua nakaa hostel na hamruhusiwi kupika, so nikamuomba rafiki yangu alikua amepanga nje ya hostel nikawa napikia huko, nakumbuka siku ya kwanza nimepika crips hazikukauka vizuri dah,lainii kufika nazo hostel roommates wakanichekaa ila nilikomaa nikaziuza zingine nikawapa wale tu, siku 2, nikapika zimeungua nilikua nashindwa kukadiria moto, baada ya hapo nikawa napika vizurii, nikapeleka hadi blocks za wakaka faster zinaisha, napigiwa simu nipeleke zingine kama zipo hadi raha, faida ilikua ni nusu kwa nusu.

Nakumbuka nilikusanya faida hadi nikapata mtaji wa viatu flani vya kimasai ambao ulinisaidia hadi nilivomaliza chuo nikaendelea nao, nikafanikiwa kusave hadi sh 70,000/= per week kwa hiyo biashara,nakumbuka nilikua namsaidia hadi babe wangu vihela kidogo vya vocha,kabla hajapata kazi, japo alikuja akaniacha mfyuuu zake. Changamoto humpa mtu akili aisee.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahahahaha
Nilipomaliza cha nne,nkapata kazi ya kumenya viazi vya chips maeneo ya magomeni aiseee nlikuwa nameny viazi zaidi ya debe 6-8 per day home mambo yalikuwa magumu sana mother alisha dead tangu nkiwa form 2 so life home lilikuwa ngumu askuambie mtu mshua tungi tu daily
Nkawa naenda asubhi saa 12 nafanya usafi na kufungua goli nakoleza moto napika chai nakunywa then naanza kumenya viazi vyangu hiyo ngoma mpaka saa4 ucku salary 1500 per day

Sasa nkawa na demu wangu anasoma pale babtist sec,anaitwa mary mtot wa wa ushuani upanga magorofa ya BOT,na pale nnapofanya kazi ndio kituo chao cha kuja kula kiepe na mazaga zaga mengine nkaona ooooh isiwe kesi akifungua shule hapa akanikuta mm ndio namenya viazi ntazid kuongeza matatizo na papa ntaishia kuliskia kwenye bomba mkasepaa

Nkapata kazi ya kuuza glosary oale maeneo ya shecklango sinza ndani pale wanapochinja kuku kaglosary kenyew ukiuza sana unapata buk 3-5 na mm mshahara wangu ni chakula tu,so nkawa nakagua bia,soda,wine zilizo expare nazigida tu so full day nimelewa zangu sina habar naiba na krate naenda kuuza ela natombea stakagi shida mim....

Form six,nlipomaliza nkaenda kuwa saidia fundi aisee maeneo ya tegeta madale nilivuta bangi hasa nilichangantikiwa kabisa nkapewa jina nlikuwa naitwa "mother fucker" per day nlikuwa nakula 10000 so nkaona sio case nkawa namuhonga tu dem wangu mary huku najipakulia mtot taratibu

Nlipomaliza chuo nkatafuta kazi weee holla,nkarudi zangu saidia fundi kama kawaida kula 10 per day nkaona maisha ndio haya vuta mabangi sana nlikuwa na laptop nkauza nguo nzur nzur za kutoa mtu ukifika bei nauza staku shida za kingese mm .....
Nlipiga ile kazi nkaja nkapata kazi ya kuuza magodoro pale nyamala natuta mawili hapo ndio nkasettle nkawa napiga pesa nkanza na kuchepuka mary na yy anaona nazingua akapata bwana abafanya kazi airport akailewa ckuwah kushika 4ml za kwangu mm mwenywe ila kipindi hiyo nilizishika

Nkaja kuajiruwa na serekal na ndio umaskini ukaanzia hapo mpaka leo napata ela ya kula tu na watoto wanaenda shuke ila bado natembea na miguu sana and I am not happy at all

Mungu sio wa wote kila mtu apambane anavyojua ili mradi utoboe tu

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu hii imenigusa sana! Mimi nmeanzia kwenye u house boy pia.

Japo mimi sijasoma kama wewe ila nilienda kusoma QT matokeo ya form 4 haya kutoka vizuri sana so ni kaamua kuachana na Habari za kusoma.

Kitu pekee ninachoshukuru nliambulia kufahamu lugha ya kingereza kwa sehemu na hiyo kingereza kimenisadia kusoma na kuelewa biashara ya mtandaoni forex.
Sasa hivi nahangaika na mtaji tu ila nikipata hata dola 500 basi nimetusua.

Komaa mkuu, mafanikio yako hayako mbali

Sent using Jamii Forums mobile app
Tafuta $200 tu mtafute Mwl RCT
Hiyo ni EA(Ambayo inatumika ktk trade)
Ameweka $200 within 6days ana $1000 na ushee huoni its profit?
IMG_20200114_083228_640.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilipomaliza chuo, nikajifunza mbinu kibao za kuiba mtandaoni ikiwemo ya kwenye mobile banking miaka ile ndo zinaanza kulikuwa na bonge la loop hole ila ulokole ukanisaidia sikufanya maana zile ishu ukianza uachi mpaka udakwe, namshukuru Mungu nimeajiriwa mambo sio mabaya nawaombea vijana wenzangu na nyie mtoboe msikate tamaa, ni kupambana tu.
 
Tafuta $200 tu mtafute Mwl RCT
Hiyo ni EA(Ambayo inatumika ktk trade)
Ameweka $200 within 6days ana $1000 na ushee huoni its profit?View attachment 1323713

Sent using Jamii Forums mobile app
Very risk kutoboa unless uwe na mtaji mkubwa maana hiyo ni kama 400% profit, kawaida kwa robot ni 10%-30% kwa mwezi ndo unaweza survive kama unabisha muulizie akupe history ya hiyo account kwa miezi mitatu,pamoja.
 
Mngepanga siku nyingine mvunje kiuno hata Mwarabu mmoja

Back
Top Bottom