Wakati umepigika kazi gani ya ajabu uliwaza kufanya?

Wakati umepigika kazi gani ya ajabu uliwaza kufanya?

Am not happy at all
Nilipomaliza cha nne,nkapata kazi ya kumenya viazi vya chips maeneo ya magomeni aiseee nlikuwa nameny viazi zaidi ya debe 6-8 per day home mambo yalikuwa magumu sana mother alisha dead tangu nkiwa form 2 so life home lilikuwa ngumu askuambie mtu mshua tungi tu daily
Nkawa naenda asubhi saa 12 nafanya usafi na kufungua goli nakoleza moto napika chai nakunywa then naanza kumenya viazi vyangu hiyo ngoma mpaka saa4 ucku salary 1500 per day

Sasa nkawa na demu wangu anasoma pale babtist sec,anaitwa mary mtot wa wa ushuani upanga magorofa ya BOT,na pale nnapofanya kazi ndio kituo chao cha kuja kula kiepe na mazaga zaga mengine nkaona ooooh isiwe kesi akifungua shule hapa akanikuta mm ndio namenya viazi ntazid kuongeza matatizo na papa ntaishia kuliskia kwenye bomba mkasepaa

Nkapata kazi ya kuuza glosary oale maeneo ya shecklango sinza ndani pale wanapochinja kuku kaglosary kenyew ukiuza sana unapata buk 3-5 na mm mshahara wangu ni chakula tu,so nkawa nakagua bia,soda,wine zilizo expare nazigida tu so full day nimelewa zangu sina habar naiba na krate naenda kuuza ela natombea stakagi shida mim....



Form six,nlipomaliza nkaenda kuwa saidia fundi aisee maeneo ya tegeta madale nilivuta bangi hasa nilichangantikiwa kabisa nkapewa jina nlikuwa naitwa "mother fucker" per day nlikuwa nakula 10000 so nkaona sio case nkawa namuhonga tu dem wangu mary huku najipakulia mtot taratibu

Nlipomaliza chuo nkatafuta kazi weee holla,nkarudi zangu saidia fundi kama kawaida kula 10 per day nkaona maisha ndio haya vuta mabangi sana nlikuwa na laptop nkauza nguo nzur nzur za kutoa mtu ukifika bei nauza staku shida za kingese mm .....
Nlipiga ile kazi nkaja nkapata kazi ya kuuza magodoro pale nyamala natuta mawili hapo ndio nkasettle nkawa napiga pesa nkanza na kuchepuka mary na yy anaona nazingua akapata bwana abafanya kazi airport akailewa ckuwah kushika 4ml za kwangu mm mwenywe ila kipindi hiyo nilizishika

Nkaja kuajiruwa na serekal na ndio umaskini ukaanzia hapo mpaka leo napata ela ya kula tu na watoto wanaenda shuke ila bado natembea na miguu sana and I am not happy at all

Mungu sio wa wote kila mtu apambane anavyojua ili mradi utoboe tu

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Miaka hiyoo nikiwa hapa hapa east sfrica ila nchi za watu niliwahii kula msoto hadi ikanipelekea kuwa pusha.

Nilisha uza sana ngada naletewa za laki 3 nauza faida zaidi ya laki 2 hadi 3 kabisa.

Kitu walikuwa wananipenda nilikuwa situmii hata kidogo.

Kuwa na urafiki na watu wengine ila sio wa Nigeria.

Sitaki kukumbuka now ni miaka kama 7.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ilikua 2013 wakati nasubiri matokeo ya kidato cha nne kama sikosei ilikua mwezi january.Kutokana na ukata wa kukaa home mda mrefu huku nikikosa hata pesa za vocha na bi mother akiwa amepigika nikawa nina njaa iliokithiri(sio njaa ya kula njaa ya hela).

Jioni ya siku moja kabala ya tukio mshikaji wangu Dullah akaniambia amepata kazi ya ukarani kwenye ghala la korosho kesho yake anaanza,nikamwambia basi nami anifanyie mpango akasema sawa atajaribu.

Siku ya tukio niko zangu home asubuhi kama saa 7 na dk kadhaa.,Dullah akaja kuniita nikatoka nje nikakutana na huyo mama tukawa watatu mimi,mama na dula,mazungumzo yalikua hivi.
Mama: hujambo?
Mimi: sijambo shikamoo
Mama: dulla ameniambia na wewe unataka kazi ndo nikamtum aje kukuita,kama upo tayari tuongozane.
Mimi : ndio mama nipo tayari na kwakua nimeshanawa ngoja nivae tu simpo twende(mpaka hapa nikajua ukarani)

Njiani yule mama akatuuliza "hivi mmekunywa chai?" Sisi tukamjibu kwa pamoja "bado"...mara akasema "eeee msije mkaniangukia huko,tukifika nitawanunulia chai"..nikauliza "kwani mama ni kazi gani,si kuandika tu"? Sikujibiwa ,mara paap tukawa tumefika kiwanda(ghala) cha korosho pale mbagala kokoto.Kweli akatuagizia chai na chapati mbili mbili,wakati nakunywa chai nilikutana na jamaa mmoja anaitwa robert(nilimzoea kwa jina la jirani) ikabidi aniulize vipi dogo mbona uko hapa ? Nikamjibu "nimekuja kufanya kazi bro humo kiwandani" akasema utaweza ndugu yangu kubeba gunia za korosho ? Nikamjibu mimi sibebi gunia tumeambiwa tutakua makarani.,akasema sawa ila kama ni kubeba gunia ndugu yangu wewe hutaweza humo ndani ni kama jehanam,Dullah akaninong'oneza achana nae mama mwenyewe ni kiongozi na ndo kasema tutakua makarani.

Mara saa 2:30 ikafika tukawa tumeingia tukaambiwa tubadilishe nguo tukavaa za kazi(hapa kichwani niakanza kujawa na masawali) Yule jirani akasema haya dogo karibu jehanam..aisee unabeba gunia(kiroba) la kwanza likaenda la pili likaishia kati wahindi wakaanza kupiga kelele nimemwaga korosho na kuchana kiroba(wakuu gunia kuliweka mgongoni sio kazi kazi ipo kwenye miguu namaanisha balance ndo ishu). Ikabidi nihamishiwe kwenye kupakia korosho maana kubeba siwezi huko nako ilikua balaa gunia zilikua nyingi balaa halafu hakuna vitendea kazi hakuna mask wala gloves mikono ilichubuka ukitaka kupumzika wahindi wanapiga kelele .

Yule Dullah mara akapokea simu(ya uongo) ghafla nikamuona anaanza kulia akaulizwa kulikoni akasema amefiwa na babu yake doh ikabidi aruhusiwe asepe nikawa nimebaki mimi na wengine.Mpaka kufika saa 6 mchana niko hoi mikono vidonda vitupu,nakumbuka nilimwambia Yule Jirani dah hapa si tayari tumeshamaliza akasema hapana dogo bado kabisa nikazidi kuchoka na kujuta nikamuuliza tena inamaana maisha yako jirani ndo yako hapa akasema ndio nina miaka 5 na nilianza kama wewe ila kwa sasa nishazoea na wewe utazoea,akaanza kunitajia wengine huyu ana miaka 3,7 mpaka 9 aisee nikastaajabu sana mara akaja muhindi tukahamishiwa kiwanda kingine kubeba gunia tupu ili ziletwe huku zipakiwe aisee ilikua balaa gunia zina vumbi nikaishiwa nguvu kwa kukisa hewa ikabidi nitolewe nje ya stoo...

Baada ya hapo tukarudishwa kiwanda kile cha mwanzo kwa ajili ya kuendelea kupakia mpaka kufika huo muda nikikohoa natoa kohozi jeusi nikipenga kamasi hivyo hivyo nikasema hapa hapana ngoja nitoroke..walinzi wakaniuliza unaenda wapi nikasema nimeagizwa mmoja akauliza mbona umebeba na nguo zako sikuangalia nyuma nikawa nishafungua mlango nikaondoka.Kufika home kifua na mwili unaniuma nakohoa balaa nikamuona Dullah aliponiona alicheka sana akasema yeye hakufiwa ila aliona kazi imemshinda alitafuta kisingizio(huyo dullah ni mbavu ila alichemka sasa jiulize hiyo kazi ilikua ngumu kiasi gani).

Ilipofika saa 1 usiku akaja yule mama kuniulizia akasema mbona nimeondoka sijaaga na hela sikuchukua,nikamuuliza hiyo hela hapo unayo? Akasema hana kaicha nikaifuate kesho yake nikamjibu hapana nimesamehe...wiki nzima niliumwa kifua na mwili na tangu siku hiyo nikaapa sitakuja kufanya kazi kwa muhindi wale jamaa ni wauwaji kazi kubwa vifaa hakuna au duni.

Ndefu samahani.

Sent using Jamii Forums mobile app
Dhhh, pole mkuu
 
Hakyanani misha haya!!!acha tu.Kuna siku mwaka flan nilishawah kutaman kuwa omba omba wale viwete wanaokaa njian.

Ilikua kama mwez mzima hiv nimekula msoto wa kiwango cha SGR.nikiwa kwenye mishe zangu maeneo ya posta, sina 100 mbovu mfukoni njaa inauma kishenzi jua kali na kiu ya maji imekaba ila hata kandoro siwez mudu kununua nijipooze, hatari na simu hata 0 ya kubip haina salio.

Nakatiza mitaa ya posta pale ilipo postal bank , kuna kiwete anaomba omba ila nadhan alikua break time muda ya saa 7 mchana ametulia, pembeni naliona kwenye mkoba lundo la coins zake, halaf kaletewa pilau nyama na kachumbali kwa juu.Pemben ana maji yake ya uhai ya baridiii halaf mkonon kashika vocha anakwangua ili ajaze salio.

Aliponiona akaanza kuniomba tena na mm hela, Dah, nikapata hasira ilochanganyika na huruma halaf nikajionaje sijui.Kimoyo moyo nikasema ww mjinga ungejua navyokutaman niwe kama ww hapo dakika hii!!!

Nikapita kimya kimya.Nilikua na mshkaji wangu anaitwa Bony basi tulipofika mbela tukacheka sanaaa na kujionea huruma maana na yy alii notice hiyo hali halaf wote tulikua juubya vyuma balaa.
 
Hakyananimqisha haya!!!acha tu.Kuna siku mwakanflan nikishawah kutaman kuwa omba omba wale viwete wanaokaa njian.

Ilikua kama mwez mzima hiv nimekula msoto wa kiwango cha SGR.nikiwa kwenye mishe zangu maeneo ya posta, sina 100 mbovu mfukoni njaa inauma kishenzi jua kali na kiu ya maji imekaba ila hata kandoro siwez mudu kununua nijipooze, hatari na simu hata 0mya kubip haina salio.

Nakatiza mitaa ya posta pale ilipo postal bank , kuna kiwete anaomba omba ila nadhan alikua break time muda ya saa 7 mchana ametulia, pembeni naliona kwenye mkoba lundo la coins zake, halaf akletewa pilau nyama na kachumbali kwa juu.Pemben ana maji yake ya uhai ya baridiii halaf mkonon kashika vocha anakwangua ili ajaze salio.

Aliponiona akaanza kuniomba tena na mm hela, Dah, nikapata hasira ilochanganyika na huruma halaf nikajionaje sijui.Kimoyo moyo nikasema ww mjinga ungejua navyokutaman niwe kama ww hapo dakika hii!!!

Nikapita kimya kimya.Nilikua na mshkaji wangu anaitwa Bony basi tulipofika mbela tukacheka sanaaa na kujionea huruma maana na yy alii notice hiyo hali halaf wote tulikua juubya vyuma balaa.
hahahaha..angekuaa haoni..ungemwibia helaa ww

Sent using Jamii Forums mobile app
 
We jangiri ni kiboko
Nakumbuka nimemaliza chuo2008 ,nikawa nipo tu home kila siku asubuhi baba wa kambo anafoka sana , na kuanza kutuambia msidhani mpo kwenye urithi wa malinzangu

Maneno yale yalikuwa yananiumiza sana ikanilazimu kwenda kutafuta kazi ya bar , nikawa counter pale kwenye bar

Yaani ugomvi matusi , kudharauli yote yakawa yangu ...usiku nalala mlemle kwenye bar sikutaka kirudi home kwa maneno yale ya mzee wetu!! Ila kazi ikawa na changamoto ukitembea tu na bamedi (sex)dharau zinaanza


Kipindi nipo pale bar nikabahatika kufahamiana na askari game watatu !! Wakawa mabest sana yaan hata kama hawana hela nawadhamini wanakunywa bia ,mwisho wa mwezi wanalipa ....

Wakanipa wazo si tuwe tunaenda na ww kwenye doria tukipata kitu tunakupa kidogo nikawaambia poa!! Ilikuwa ni kambi ya KIJERESHI

Ikawa ikifika uck km siku ya doria namuachia mdogo wangu wa pili ananisaidia kuuza pale bar ,maana tulikuwa kama makinda tukiugua mzee mara agome kutupeleka hospital ,nguo alikuwa hataki kbs ..kutuona tumevaa nguo nzuri [emoji24][emoji24][emoji24]

Tukawa tunaenda doria tukikutana na watu wameingia kwenye eneo la hifadhi tunawanyanganya kuni ,baskeli na kipigo juu kazi yangu ilikuwa kuigiza mizigo kwenye gari .....

Siku moja moja na wao walikuwa wanawinda nyati ,swala au nyumbu wananipa nyama naiuza ...napata hela kidogo kidogo natunza

Nilipokuwa mzoefu ......nikamfata gemu mmoja jina kapuni nikamwambia sasa si unifundishe kutumia bunduki tukawa tunaenda porin wananifundisha shabaa tukiwa tuna winda ..nikawa konki wa L4 ,kuitumia akanifundisha kuifuta na kuifungua

Baadae nikatafuta ya kukodi kwa mtu x alikuwa nayo na lisasi alikuwa akiniuzia moja sh 15000/- imeandikwa mzinga .ganda jekundu ..na zilikuwepo za kupigia tembo ganda jeusi ....ukimchapa na hiyo anaanguka

Nikaanza uharamia wa kuingia porini kwa kuwa nilikuwa na ratiba kamili ya askari game kufanya doria , nikawa nikikutana hata na mzoga wa mnyama nauchukua naupaka chumvi nyingi naukausha juani halafu ...nikirudi mjini natembeza mji kwa mji nyama ya porini watu walikuwa wakiipenda sana iliitwa vimoro

Nilitengeneza hela sana !! Tamaa ikanizidi bwana wakaja wasomali walielekezwa kuwa wakija kwangu hawatakwama njia nyingi nazijua

wanataka niwapeleke porini walikuwa na warundi na land cluzer ambayo ilikuwa na turbo na matenk mawili ...wakiwa na bunduki A.K 47 , NAbunduki moja inastand na mkanda wa risasi wakanilipa dola 250

Walikuwa na gari mbili kenta na land cruser tukaenda nao bwana tukapitia kijiji kinaitwa kijereshi tukaingia kwenye hifadhi ya serngeti

Ilikuwa mida ya saa moja saa tatu usiku jamaa walikuwa wana mwaga risasi kama karanga hawaangalia mnyama mkubwa mdogo !!

Baadae wakawa wanachambua wanyama wanatupia kwenye kenta mpk ikajaaa , kumbe askari game walisikia milio ya risasi wakaja aise ......zilitembezwa risasi na wale maharamia wa kisomali bunduki ilikuwa inashikiliwa na watu wawilo ....

Game wakazidiwa kabisa tukaondoka tukarudi mpk lamadi wakaniacha mida ya saa 8 usiku wakacha mwendo tokea hapo nikahapa sitakwenda porini

Maisha haya nikajikuta nimetengeneza km m1 ....yaani mpk naenda kulipot kazini tarehe 1-09-2009 ..
Nikawa nipo vizuri sana

Mafanikio ya mtu yanatengenezwa na kujitoa sadaka !! Siwez kusahau



sent from toyota Allex

Sent using Jamii Forums mobile app
 
@kidukulilo akija kutoa ushuhuda wake mambo yatakuwa hivi:..

"Nimeteseka sana mimi..
Wakati nimemaliza shule pale IST nikaamua kuliko kukaa bure bora nitafute kazi
Nikaongea na mzee wangu anitafutie connection

Mzee akaniambia kuna issue canada nikasema sawa..
Nimeenda nikakuta kazi yenyewe ni kupanga mafile katika ofisi flani kwa masaa matatu kwa siku
Halafu mshahara wenyewe mdogo tu usd 300 kwa siku, nilisikitika sana...

niliteseka mimi, nyie acheni tu..

Ngoja aje humu[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]

Sent using Jamii Forums mobile app

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Chief unaweza nipatia mwongozo juu ya forex natamani sanaa hii biashara

mwanabhonga
Umekaribia kufirisika pole hakuna hela rahic fanya bishara mkuu achana na online busness

Sent using i phone x
 
Back
Top Bottom