Liuumi
Senior Member
- Jun 17, 2015
- 164
- 165
Nilipitia kipindi kigumu sana hadi nguo ziliisha na ilibidi hata wakati wa kukaa Navizia maana ikipasuka tu, kiraka kitanihusu na pesa ya kiraka sina, muda huo huo suruali zilikuwa 2 na hapo ni graduate. Asiwaambie mtu wanajf, nilikuwa naamka ucku nawaza na ndugu pamoja na rafiki walinikacha kisa mkwanja. Niliwaza kufungua biashara ndogo ya kuuza half cakes kupitia vijana wanaotembeza maana naishi mjini. Nikande ngano na vijana wangu na waende kuuza na kuwalipa kitakachopatikana. Ila nilishindwa maana sikuwa na pesa na pia sina nyumba kwani nakaa kwa mama, na mama ananidharau na watoto wake. Ghafla nikapigiwa simu na rafiki yangu wa zamani sana kuwa nikafanye interview katika kampuni moja katika huo mji niliokuwa naishi, nikaenda na nilikuwa peke yangu, nikapigiwa simu kuanza kazi.
Unaambiwa ilikuwa saa 11 jioni mdada aliniambia..... nanukuu " When you expect to start your new job?" Nilimjibu hata sasa hivi, mdada alicheka sana kwani ilikuwa jumamosi, ila aliniambia tulia Mr. Baadae akaniambia utaanza jumanne ijayo na nimetuma offer kwa email yako, isaini na baada ya hapo uanze kazi. Sasa nashukuru nguo nimenunua, simu ninayo, dharau zimeisha home, nashukuru heshima imerudi.
Funzo: Usimdharau aliyesoma hasa mwenye elimu kuanzia degree 1, pia nikagundua kuwa nguo zikichakaa huwa zinawahi kuchafuka na zinachelewa kutakata unapozifua.
Tusomeshe watoto, huu ndio urithi pekee.
Sent using Jamii Forums mobile app
I like zinawahi kuchafuka na zina chelewa kutakata@kidambinya