Wakati unaingia mjini kitu gani ulifanya na hutosahau?

Mbao za Mawe

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2015
Posts
23,372
Reaction score
54,943
Mimi kati ya vitu ambavyo sitosahau ni pale nilipoenda mji mmoja hivi hapa nchini sasa bhana nikahisi barafu ni muwa nikanunua zile za kwenye kijiti badala ya kulamba mwenzio nikang'ata nusu yake nikajaribu kutafuna bhana weeee nilichokipata mwenyewe najua.

Nilishindwa kutema nikashindwa kumeza, nikasema nikitema askari alikuwa mbele yangu angesema nachafua mazingira.

Sikuwa na hamu na barafu tena hicho ndo kitu nakumbuka niliingia mjini kwa mara ya kwanza nilifanya.

(Ngumu kutafuna usiimeze haraka)

Na wewe sema nini kilikutokea
 
Haaa mimi niliona watu wanakunywa kahawa nikatamani na mimi ninywe!! Basi mzee mzima nikajjikaza nikaita kama mwenyeji vile ""lete kahawa!""tena kwa ukali!! Huwezi amini nilionja mara moja tuu na nikaitema na kikombe nilikiachia hadi chini maana ile kyweka mdomoni mwili ullisisimka balaa[emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2]
 
mi nilivyokua mdogo kaka yangu akanitoa out,
tukaenda kula ice cream (koni) nilivyomaliza nikarudisha kikombe chao
 
Nakumbuka nilipong'aka kwa mhudumu wa hotel enzi hizo Rex Hotel nilipoagiza chips chicken nilipotanguliziwa supu nikamwambia mhudumu nimeagiza chips chicken mbona unaleta supu na slesi za mikate akanifahamisha hiyo ni kwa ajili ya kupasha tumbo ulichoagiza kinakuja nilijiona mjinga sana kwa kutovuta subira kiangalia kinachofuata mwaka 1975
 
Nakumbuka mara ya kwanza kununua friji ilikuwa siku nzuri sana kwangu kaduka kangu kadogo kakiwa ndio kanashamiri mtaani nikaamua kununua friji ili kuuza vinywaji baridi basi baada ya kuingiza dukani usiku mtu yeyote akiwa hajui nikafungua mlango wa friji nikaiwasha ili inipe ubaridi na joto la dar kumbuka nilikuwa nalala dukani basi kulipokucha asubuhi kafriji kameharibika na hakapozi tena nikaishia kusumbuana na mafundi
 
Aise kuna kijana alipofika town alikuwa akisalimia kila mtu yaani nilikuwa nasikia zinatoka kwa mkupuo kufuatana na vichwa anavyoviona shikamo....shikamo....shikamoo...
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
nilikuwa natmbea san pek angu afu bila mpanglio adi nachlewa kurud hom na kupoteaaa njia ovyo.
 
Aise kuna kijana alipofika town alikuwa akisalimia kila mtu yaani nilikuwa nasikia zinatoka kwa mkupuo kufuatana na vichwa anavyoviona shikamo....shikamo....shikamoo...
Ahaaaaaaaa ahaaaaa kweli ushamba mzigo.
 
Me nilivyokuwa mdogo nikiingia kwny maduka ya nguo hata yale masanamu yanayovalishwa nguo nilikuwa nayasalimiaga[emoji38] [emoji38]
 
Aise kuna kijana alipofika town alikuwa akisalimia kila mtu yaani nilikuwa nasikia zinatoka kwa mkupuo kufuatana na vichwa anavyoviona shikamo....shikamo....shikamoo...
[emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15]
 
Me nilivyokuwa mdogo nikiingia kwny maduka ya nguo hata yale masanamu yanayovalishwa nguo nilikuwa nayasalimiaga[emoji38] [emoji38]
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Niliibiwa 5,000 TZS pale buguruni chama nilikua kwenye daladala natoka kwa mwenyeji wangu narudi shule nilikua boarding advanced level
Iliniuma sana kwa kipindi kile buku tano ya kupewa ni pesa mingi sanaaa[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Mi nakumbuka 97 naingia town kufanyakazi dukani sasa kwenye hiyo nyumba yenye duka kuna kabinti kalikua ndio kameingia darasa la sita mwaka huo ila sikua najua, nikawa nakaamkia shikamoo kwa sababu alkua na kaumbo kakubwa, alafu nguo zake za shule zilifanana na za sekondari ya kijijini kwetu nkajua kanasoma sekondari, nikajajua nimekazidi miaka mitatu nilijicheka sana
 
Acha kabisa mie ile kuingia mjini nikakutana na daladala zimeandikwa city bus nikajikuta namuuliza mwenyeji wangu hivi haya magari yote yaliyo andikwa hivi niyamtu mmoja?...sikuamini kicheko alichokiporomosha hapo
 
Kuna Siku nilipanda chai maharage( daladala, mwaka 1995) kwenda kariakoo wakati wakurudi nilikaa kituoni kuisubilia gari hiyo hiyo mpaka ilipotokea tena.nilijua daladala inayotoka eneo hilo ni hiyo moja tu.kipindi hicho zilikuwa hazijaandikwa zinapokwenda.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…