Wakati unaingia mjini kitu gani ulifanya na hutosahau?

Wakati unaingia mjini kitu gani ulifanya na hutosahau?

Kuna Siku nilipanda chai maharage( daladala, mwaka 1995) kwenda kariakoo wakati wakurudi nilikaa kituoni kuisubilia gari hiyo hiyo mpaka ilipotokea tena.nilijua daladala inayotoka eneo hilo ni hiyo moja tu.kipindi hicho zilikuwa hazijaandikwa zinapokwenda.
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Nakumbuka mara ya kwanza kununua friji ilikuwa siku nzuri sana kwangu kaduka kangu kadogo kakiwa ndio kanashamiri mtaani nikaamua kununua friji ili kuuza vinywaji baridi basi baada ya kuingiza dukani usiku mtu yeyote akiwa hajui nikafungua mlango wa friji nikaiwasha ili inipe ubaridi na joto la dar kumbuka nilikuwa nalala dukani basi kulipokucha asubuhi kafriji kameharibika na hakapozi tena nikaishia kusumbuana na mafundi
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Aise kuna kijana alipofika town alikuwa akisalimia kila mtu yaani nilikuwa nasikia zinatoka kwa mkupuo kufuatana na vichwa anavyoviona shikamo....shikamo....shikamoo...
Kijana wap bana sema ukwel, sio ww mwenyewe
 
Nakumbuka Posta nlikutana na maulid kitenge nkamuuliza hivi nshakuonaga wapi?tabora eeh?akajibu labda kwenye tv......nkasema ooookeeey
 
Ktk mizunguko niko na mwenyeji wangu tukawa tunaingianyumba moja ina gate kali. Mara kwa nje naona switch, nikasema yaani hawa washamba kweli wanawekaje switch ya taa nje ya nyumba, alinicheka kweli. Kumbe kengere bhana. Huwa nikikumbuka najiona kweli mi msukuma wa kuja tu mjini
 
Back
Top Bottom