Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,108
- 10,191
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema kuwa Serikali imeendelea kuliimarisha Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) ili liweze kutoa huduma bora ya usafiri wa anga ndani na nje ya nchi ambapo amebainisha kuwa serikali imefanya malipo ya awali ya ununuzi wa ndege tano.
Japo hawajasema ni lini wamefanya malipo ya ndege hizo, ni muhimu kujiuliza ni kwa nini serikali haijataja mpango wake wa kupunguza ongezeko la bei lililopo ambalo linaongeza ugumu wa maisha.
Ndege mpya kati ya hizo, ndege moja ni aina ya Boeing 787-8 Dreamliner, ndege mbili aina ya Boeing 737-9, ndege moja aina ya De Havilland Dash 8-Q400, na ndege moja ya mizigo aina ya Boeing 767-300F hivyo kuifanya serikali kuwa na jumla ya ndege mpya 16.
Yes, ni jambo jema kuwa na shirika thabiti la ndege, Je ni sahihi kwa muda huu?