Wakati wa mvua na mafuriko Dar es Salaam ndipo somo kwamba madaraja ya baharini sio kipaumbele cha kwanza kwa wakazi wa Dar litaeleweka!

"Ili watu wajue tofauti ya maendeleo yanayoletwa na yaliyokuwepo nilazima waone athari kwa vitendo ili tukileta maendeleo waone tulichomaanisha kabla ya kutekeleza ilani yetu..." alisikika akisema mgombea mmoja vegetarian
 
Kwani ao watu Wa jangwani si mda mrefu tu walipewaga viwanja magwepande na jk sasa kulikoni tena ziwe kelele kwa jpm..wabongo ni lawama tu
 
Kwani ao watu Wa jangwani si mda mrefu tu walipewaga viwanja magwepande na jk sasa kulikoni tena ziwe kelele kwa jpm..wabongo ni lawama tu
MKuu, tatizo la mafuriko Dar sio kwa watu wa Jangwani tu. NI karibu jiji lote
 
Mtu anatengeneza ka flyover kamoja fake kisha anapiga kelele kama mpiga debe!
 
Kaka.hata marekan kuna jaaga maj sehem nyingne....kama ulisoma vzur jiografia utaelewa kwann maeneo yaliyojaa maj yamejaa maj...hata uweke miundombinu gan...dar maj yatajaa tuu...
Hapana Mkuu . Maeneo yaliyojaa maji yana namna yake ya kuendeleza ili yasikabiliwe na mafuriko. Huwezi kuendeleza eneo huku ukijua wazi kwamba litakabiliwa na mafuriko, hapo utakuwa sio mhandisi wewe. Pia tofautisha mafuriko ya Marekani na huku kwetu. Mafuriko ya Marekani yanatokana na hurricanes, kina Katrina nk. Haya hayatabiriki na sio ya kila mwaka. Haya ya kwetu ni ya kila mwaka, ili mradi masika imefika.
 
Tatizo la mafuriko linalotoka na na miundo mbinu ya maji ilosanifiwa zamani,Leo mji umekuwa bado mifereji ya maji ile ile ya kipindi Cha miaka ya 70,Jambo la Tania za wakaz wa dar kugeuza mito na mikondo maji kuwa madampo ya takataka hivyo mvua zikinyenya madaraja madogo na makubwa huziba hivyo kupelekea mafuriko kwenye kingo zamito , kuepuka changamoto hiz ni serikali kupitia manispaa kujengea hiyo mito na mifereji ili kuzuia kingo kubomoka na pia kuendeleza eneo la jangwani ambapo ndo sehemu kubw ya mikutaniko ya mito inayoingia baharini pia bila kusahau kunyanyua daraja la jangwani.
 
Ndio hiki nilisema haitachukua gharama ya kutengeneza flyover moja kikirekebisha, lakini tukaona kuendezesha Dar kwa flyover ni muhimu zaidi, hata kama mafuriko yataua watu!
 
Mvua zinanyesha kwa msimu but foleni ipo mwaka mzima! Hasara inayosababishwa na foleni nikubwa ukilonganisha na mafuriko pia watu tunawaambia hameni mnang'ang'ania alafu mnakuja kipiga kelele hapa.
Ukijaribu kusoma kwa makini hicho ilichoandika utajua kuwa hauko sawa........sasa wewe mvua imesababisha vifo vya watu 12(je foleni imeshawahi sababisha vifo vya idadi hiyo)....watu wahame mabondeni(je pale daraja la kwa mfugale na jangwani ambapo serikali imejenga miundombinu yake ni bondeni au sio bondeni........huko Mbezi beach na kwingineko kuliko furika maji nako ni bondeni au sio???????
 
Mkuu sasa hizi nyumba zilizojengwa bondeni kuna miundombinu gani utajenga kuepusha kufunikwa na maji?
Asilimia kubwa ya nyumba zilizojaa maji ni za bondeni au zilizojengwa kwenye njia za maji.
Ndege moja tu isingenunuliwa iyo hela ikawekezwa kwenye miundombinu mabondeni ingesaidia. It's just easy as ABCD or as easy as to wink.

Wanipe hii nchi muone siku 100 tu kamwe mafuriko hamtayaona
 
Ndege moja tu isingenunuliwa iyo hela ikawekezwa kwenye miundombinu mabondeni ingesaidia. It's just easy as ABCD or as easy as to wink.

Wanipe hii nchi muone siku 100 tu kamwe mafuriko hamtayaona
Sawa mkuu.
 
Mkuu sasa hizi nyumba zilizojengwa bondeni kuna miundombinu gani utajenga kuepusha kufunikwa na maji?
Asilimia kubwa ya nyumba zilizojaa maji ni za bondeni au zilizojengwa kwenye njia za maji.
Halafu kitu kimoja unatakiwa kuelewa kama injinia ni kwamba mafuriko bondeni yanatokana na maji yanayoenda bondeni. Kwa hiyo tatizo sio kujenga bondeni au kurekebisha bondeni, bali ni kuengeneza njia za maji ili yasiende bondeni. Tunachokabili kwa sasa ni maji ku-find its own course kwa kuwa hayajawa controlled yaende yasikosababisha madhara
 
Sawa engineer. Ila naturally njia ya maji inaenda bondeni. Sasa utengeneze njia ya maji yasiende bondeni yaende wapi mlimani? Bonde la mto rufiji,bonde la mto Zambezi bonde la mto msimbazi hujasikia hayo maneno?! Hao ndugu zetu wameamua kuishi kwenye bonde la mto msimbazi huko lazima wapambane na maji ya mto msimbazi. Ni rahisi wao kuondoka kuliko kuyabadili maji ya mto msimbazi yasiende kwenye bonde la mto msimbazi.
 
Aaah Mkuu usiniangishe, utapelekaje maji yaende mlimani? Tunaposema yasiende bondeni ni bondeni kweny barabara na makazi ya watu. Unajua kwa Dar sehemu ya bondeni kuliko zote ni wapi? Ni baharini - huko ndiko bondeni yanatakiwa kwenda, the lowest point in Dar.
 
Ingekuwa wewe ndio Rais hao watu wa jangwani ungewasaidiaje kwa mfano?
Maana hao walishaambiwa wahame hapo hilo eneo sio zuri kwa makazi ya watu na wakapewa viwanja mabwepande wakauza na kurudi tena hapo jangwani ili mradi tu wakae karibu na mjini
Usiseme ungekuwa rais ungewafanyaje wa Jangwani, hapo Jangwani pangekuwa hapafai serikali isingejenga hapo kituo cha mwendokasi, kwahyo serikal haijui inafanya nini, kama inawalalamikia watu kujenga Jangwan wakati huo huo serikali yenyewe imejenga hapo unadhan akili zao zipo sawa? Ndo mana tunasema wamechoka kuongoza serikal
 
Kwa hiyo wewe uhai/roho yako unailinganisha na thamani ya gari la mwendokasi?
maana hao serikali hapo wamelaza magari tu lakini hawalali hapo wewe unaulaza mwili wako hapo jangwani halafu unajilinganisha akili yako na serikali
 
Sasa aliokwambia nchi inatakiwa kuzuia natural calamities ni nani?
Kinachoweza kufanyika ni kuwa na mamlaka ya serikali kama TMA ambayo inasaidia kusoma alama za nyakati kuhusiana na hali ya hewa na kutoa tahadhari mapema.

Hao ma shwaini wa Jangwani wameshapigiwa kelele kwa miaka na miaka. Wahame ila wanajitia ujuaji😂😂😂 waache wapate hasara. Niko na Magufuli katika hili.
 
Kimsingi kabla ya kuanza project ya Salenda, walipaswa kuanza na ngoma hii ya jangwani.

Inafedhehesha mji sana hii kitu ya jangwani... Mafuriko ya jangwani naona ndiyo yanatudharirisha zaidi..
Jangwani ni mkondo wa Maji. Pale hapakutakiwa watu waishi kabisa.
 
Very right. Maji yanafuata mkondo wake. Raia wamejenga kwenye mkondo wa Maji. Maji haya flow kwa wepesi sasa mafuriko yakija tena lawama zinarudi serikalini tena?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…