Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,336
- 4,731
Kipindi cha uchaguzi na maajabu yake, utasikia maneno na mipango ya busara kutola kwenye chama kikongwe huku wakijitenga kuwa chanzo cha uharibufu na umasikini uliopo, watatoa mawazo chanya yenye akili kama siyo wao waliokaa madarakani toka kabla ya kuanza kwa vyama vingi nchini Tanzania ila lugha wanayoongea na mbinu ya kuwasilisha hoja zao unaweza dhani Tanzania imekuwa chini ya Chama kingine ambacho kiliharibu mifumo na kifuja pesa na wao ndio wamekuja kuweka plan B ili tujikwamue kutoka kwenye uharibifu uliokuwa umefanyika awali na vyama vilivyokuwepo madarakani kumbe ni wao wenyewe
Mbinu hiyo hutumiwa na chama hicho kikongwe ambacho dhamira yake ya kubaki madarakani Si tena kuisaidia nchi na wananchi wake kwani tayari wameshashindwa na hawana tena hoja mpya ila dhamira yao ya kufanya janjajanja za kubaki ni ili waendelee kunufaika na pesa za nchi huku wakijua kabisa kwa madudu waliofanya wakiwa madarakani yakiwa hadharani watapoteza heshima kabisa au hata kustahili kuishia jela sasa ili kujilinda wanalazimika kubaki kwa mbinu yoyote ili waepuke hayo na pia waendelee kula mema
Wakati huu Utaanza kuwaona wakikosoa na kutoa mawazo ambayo baada ya kuapishwa huwa hawana mpango nayo maana si kitu wanachotaka kufanya bali ni ulaghai dhidi ya watanzania wengi kwani wameshawadharau na kuona hawawezi kutambua kama wanawadharau, wanawaona wajinga na wameshajua kuwa hawawezi kuwatoa hapo kwa kura maana kila kitu kwenye mfumo wa uchaguzi ni chao
Wakati huu wa kuelekea uchaguzi ndio utasikia maslahi ya walimu yanajadiliwa kwani ni kundi la kulitumia kufanyia janja ya uchaguzi sasa ili kuwapata ni lazima wawalaghai kwa kuwaongeza senti kidogo ya kununulia fungu la dagaa, utasikia maaskari nao wanaguswa huku vijana wakiahidiwa ajira na ahadi nyingine pamoja na hoja zinazoambatana na mishangao ya ilikuwaje Toto afya kadi ikafutwa utadhani wao siyo ndio wahusika wa ufutaji huo