Wakati Waarabu wanaachana na biashara ya Mafuta na kukamata Sekta ya Bandari sisi Tanzania Ndio tumejikita kuuza magari ya Petrol na Diesel!

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Sina hakika kama pale Wizara ya viwanda na biashara kitengo cha Mipango na Maendeleo ya Biashara wanajua kinachoendelea duniani

Cha kushangaza Watanzania wenye mitaji Ndio wamejikita kufanya Biashara zilizopitwa na wakati

Hebu angalia Yadi za kuuza magari ya Petrol na Diesel zilivyojazana hadi vichochoroni kabisa Tandale huko ilhali Ulaya kwa mfano magari hayo yashapigwa Marufuku

Congo Vijana wao walizubaaga hivi hivi 🐼

Jumaa Karim πŸ˜„
 
Uzur zinauzwa gari za miaka 20 nyuma, zikiisha na sisi tutabadilika miaka 20 ijayo..

Kingine unataka kodi ya maana itoke wapi?
Gari ya dola 1000 bongo ushuru dola 5000...


Biashara nzur sana hiyo...

Hata compyuta ilivyokuja mambo ualikuwa hivyo hivyo.. tuwe wapole, maaana kuna office nyingi tu za umma mpaka sasa wanatumia makaratasi kwenye ku file documents na hawana mpango wa kutoka huko.
 
Wakulaumiwa ni CCM iliyoko madarakani kwa zaidi ya miongo sita, wao muda wote wanafikiria wizi wa kura ili waendelee kutawala bila kufikiri wataifanyia nini Tanzania.
 
Tunaongozwa na Chama Cha Mazezeta
 
Unajichanganya Mkuu

Ushasema Ulaya halafu unawazungumzia watanzania.

Ushasema biashara, biashara ni mahitaji.
 


Rushwa hupofusha macho
 
huelewi namna biashara inavyoenda wewe kasuku.

hata ipite miaka 1000 bado magari ya yanayotumia diesel na petrol yatauzwa tu
 
Trump Raisi wa Marekani anasema Drill baby drill,kwa maana endelea kuchimba visima vipya vya mafuta.
Pili kafuta upendeleo wa magari ya umeme.
Tatu kafuta kikomo cha kuzalisha magari ya diesel na petrol.
Kaidoa Marekani kwenye Aziimio la Paris kuhusu uchafuzi wa mazingira .
Hivyo kwa Tanzania kuendelea kuhiimalisha biashara magari yatumiayo diesel na petrol sio jambo la kushangaza.
Raisi Trump ndio mwamuzi.
 
1. Sekta ya Mafuta Bado ni Muhimu kwa Uchumi

Tanzania bado inategemea mafuta kwa uchumi wake. Miundombinu ya nishati mbadala, kama umeme wa magari ya umeme, bado haijakomaa vya kutosha kuweza kuchukua nafasi ya mafuta kikamilifu. Hii inamaanisha kuwa bado kuna soko kubwa la magari ya petroli na dizeli.

2. Teknolojia ya Magari ya Umeme (EVs) Tanzania Bado ni Changamoto
Tofauti na Ulaya, Tanzania haina miundombinu ya kutosha ya magari ya umeme. Ukosefu wa vituo vya kuchaji, gharama kubwa za magari ya umeme, na changamoto za upatikanaji wa vipuri ni mambo yanayofanya soko la magari ya petroli na dizeli kuendelea kuwa hai.

3. Waarabu Wanawekeza Katika Bandari Lakini Hawajaacha Mafuta
Nchi za Kiarabu kama Saudi Arabia na UAE bado zinawekeza kwenye mafuta huku zikihamasisha sekta nyingine kama bandari na utalii. Tanzania inaweza kujifunza kutoka kwao kwa kupanua sekta mbalimbali bila kuachana kabisa na biashara ya mafuta.

4. Magari ya Petroli na Dizeli Bado Yana Mahitaji Makubwa
Licha ya Ulaya kupiga marufuku magari mapya ya petroli na dizeli kwa siku zijazo, Afrika bado ina mahitaji makubwa ya magari haya. Soko la Congo, Zambia, na nchi jirani bado linategemea magari haya kwa usafiri wa biashara na binafsi.

5. Watanzania Wanajua Wanachokifanya
Watu wanawekeza kulingana na mazingira ya soko. Huwezi kulinganisha Tanzania na Ulaya kwa kila jambo, kwani maendeleo ya teknolojia yanatofautiana kati ya maeneo haya mawili.

Kwa hiyo, badala ya kusema "Tanzania bado sana," ni bora kuangalia hali halisi ya soko na maendeleo ya teknolojia kabla ya kutoa hitimisho kama hilo.
 
Anayeiamulia Marekani Kwa Sasa ni Elon Musk huyo Trump ni kama Tyson wa Lumumba πŸ˜‚
 
Dunia ya Leo inabadilika Kwa Kasi ya Mwanga bwashee

Haisubiri kama ile dunia yetu

Hii ni dunia ya Junior X siyo ya akina Lucas Mwashambwa πŸ˜„
 
huelewi namna biashara inavyoenda wewe kasuku.

hata ipite miaka 1000 bado magari ya yanayotumia diesel na petrol yatauzwa tu
Haya

1980 tulitumia Jeifong tunawasha kwa hendeli kama Kiki ya Pikipiki

Vijana wa Tanzania wamelemazwa na Uchawa πŸ˜€
 
Kama wapo serious wayatoe bure sisi tulipe ushuru tu. Ukichungulia bei ya gari mpya za diesel zilizoachiwa hivi karibuni utagundua hawapo serious.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…