Wakati wafanyabiashara wakigoma, kwa nini wafanyakazi nao wasigomee mishahara midogo? Serikali haiongezi mishahara kwa kiburi.

Muuza Kangala

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2021
Posts
1,242
Reaction score
4,813
Hebu mjitafakari hasa walimu na watumishi wengine.

Tgs A ni shilingi za kitanzania 330000 kwa njinsi maisha yalivyo magumu. Hii pesa mtu unaweza kutoboa kweli?

Sukari bei juu, kodi ya pango juu, alafu mei mosi inapita patupu bila nyongeza ya mshahara.

Wafanyabiashara wamegoma na wamesikilizwa. Nyinyi mbona hamsikilizwi?
 
Wewe unafikiri ni kwa nini kila siku wanahangaika kuanzisha vitu vya kuwabana?

Ni kwa sababu na wenyewe wanafahamu fika watumishi wengi wa kati na wale wa chini wenye akili timanu, hawafanyi kazi kwa 100%. Na hata wawabane vipi, bado watategea tu kutokana na kukata kwao tamaa.

Yaani unilipe laki 3 kwa mwezi, halafu hela hiyo hiyo umpe Mbunge kama posho kwenye kikao kimoja tu, huku akiwa amelala tu kwenye kiti, au kupiga makofi na kuunga mkono hoja! Halafu nifanye kazi kwa moyo! Ni kutegea tu kwa kwenda mbele.
 
Sijui ni nani atawakomboa wafanyakazi wanyonge wa Kitanzania, maana kwa asili ya hawa viongozi tulio nao kila mmoja kula kulingana na urefu wa kamba yake, watasubiri sana nyongeza za mishahara ya kuridhisha au kutosheleza.
 
Back
Top Bottom