Wewe unafikiri ni kwa nini kila siku wanahangaika kuanzisha vitu vya kuwabana?
Ni kwa sababu na wenyewe wanafahamu fika watumishi wengi wa kati na wale wa chini wenye akili timanu, hawafanyi kazi kwa 100%. Na hata wawabane vipi, bado watategea tu kutokana na kukata kwao tamaa.
Yaani unilipe laki 3 kwa mwezi, halafu hela hiyo hiyo umpe Mbunge kama posho kwenye kikao kimoja tu, huku akiwa amelala tu kwenye kiti, au kupiga makofi na kuunga mkono hoja! Halafu nifanye kazi kwa moyo! Ni kutegea tu kwa kwenda mbele.