Wakati Wanaojitambua Ghana wanarudisha Raia wao kutoka Ukraine na Urusi, wale Wasiojitambua wako busy Kushangilia Bendera yao Dubai

GENTAMYCINE

Hapo umesema ukweli bila chenga,lakini kwa sababu nchi hii ni ya mlengo wa kisiasa na unafiki.
Ni vigumu kwa wote kukuelewa!

Wakati haya yote yanatokea ikumbukwe kwamba kuna ndege za ATCL zimepaki,tena mpya kwa kukosa Route.

Wakati haya yote yanaendelea tunao watalii wapatao 900 kutoka Ukraine [emoji1255] ,ambao wamekwama Visiwani Zanzibar kwa kukosa usafiri wa kuwarudisha Ukraine [emoji1255] shauri ya hiyo vita.

Wakati watoto wetu wamekwama huko Ukraine [emoji1255] na Poland [emoji1200].
Serikali makini ingefanya utaratibu maalumu kwa kushirikiana na Ukraine [emoji1255] kwa kupitia ubalozi wao ulioko nchini
Kenya [emoji1139] .

Ili washirikiane na Tanzania [emoji1241] itowe ndege ya kuwasafirisha hao wa Ukraine [emoji1255] 900 walioko Zanzibar na kuwapeleka hadi nchi jirani ya Poland [emoji1200].

Kisha ndege hiyo hiyo pia itumike kuwabeba watanzania watakaokuwa wamevuka mpaka na kuingia Poland [emoji1200].
Wakiwemo pia hata raia wengine wa Afrika Mashariki.

Tunao ubalozi wetu uko pale
Sweden [emoji1236],na ndio unaotuwakilisha pia huko Ukraine [emoji1255] hivyo balozi wetu huko angetumika kuhakikisha anafanya jitihada za Watanzania kufanikiwa kuvuka mpaka na kuingia Poland [emoji1200].

Ili iwe rahisi wao kuchukuliwa kutokea pale.

Sasa hapo humsikii waziri husika akiongelea kufanya lolote zaidi ya wote kurundikana Dubai wakiishangilia picha ya mama na bendera.

Hatuko serious...
Tunacheka yale tuliostahili kulia...

Na
Tunalia yale tuliostahili kucheka.....
 
Waafrika wengi kama sio wote waliopo Ukraine na jirani zake, wameenda huko kusoma kwa scholarship.
 
Tumenunua ndege kwa gharama kubwa..tunahofia isije ikatunguliwa.maana kwenda ukraine na kurudi ni kama kamari..watz walioko huko sio masikini wenzako! mpaka mtu anaamua kuchukua option ya kusomea nje ni jeuri ya hela.
Wengi wao wapo kwa scholarship, hawana utajiri wowote. Usichanganye na wanaosoma US, UK ,France na Scandinavia
 
Viongozi wengi wa africa hawana utamaduni wa kupenda raia wake.. Hii ndio shida kubwa ya viongozi wengi wa africa....

Mfano mama katoka tanzania kwenda ufaransa kaenda tena belgium.. Baadae karudi tena kakaa siku 3 kaenda dubai.. Safari zote hzo ni ndege..

Lakin ilishindwa kutoa ndege yake hata moja kufuata raia wake ukraine kabla ya vuguvugu..

Africa tuna matatizo mengi sana sisi wenywe kabla hatujawasingizia wazungu na waarabu..
 
Upo sahihi sana, nakuelewa sana, na sio kwenye hili jambo tu, kwenye mambo kibao, ndio maana tuna dharaulika sana dunia,
 
Upo sahihi sana, nakuelewa sana, na sio kwenye hili jambo tu, kwenye mambo kibao, ndio maana tuna dharaulika sana dunia,
Yaan hup ni ukwel... Toka kipind cha corona kule china...

Viongoz wa kiafrica wanakemea ubaguzi wa rangi.. Na kipind hko hko na wao wanabagua watu wao..

Africa bado hatuja staarabika kbsa
 
Ndege zingekuwa zinaruhusiwa kutua Kiev nina uhakika mpaka muda huu watanzania wote wangekuwa wamekwisha kuondoka.

Yanayotokea Ukraine ni tofauti kabisa na yanayotokea Dubai. Ndege ipo Poland wanafunzi wameambiwa wafanye wawezalo wafike hapo ili iwachukue na waweze kurudi nyumbani.

Kukosoa ni kazi nyepesi sana, kila mtu anaiweza.
 
Usijidharau kwa kuamini huo upuuzi wa hizo study za wazungu. Kiasili wanajiona bora na wanaamini hivyo.

Wapo waafrika wengi tu wametoa mchango katika uvumbuzi wa vitu mbalimbali vinavyoifanya sayansi ikaheshimika, huwezi kuona mahali machapisho yenye kuhusu hayo waliyoyafanya.
 
Ndio maana nimesema angalia mambo in holistic way, wapo waafrika ma genius, ila swali la msingi linabaki kwann sisi ni masikini despite all the resources?
 
πŸ’πŸ’πŸ’
Your browser is not able to display this video.
 
Tuwekee hilo tamko la serikali la kuthibitisha uwepo wa ndege ya Tanzania [emoji1241] nchini Poland [emoji1200]
Ambayo inasubiri kuwasafirisha watanzania ila ikakuta hawapo.
 
Mataga una gubu, move on
 
Wewe dada huu mwaka hayo makalio yaatapungua
 

Kakosea wapi hebu dadavua
 
Kinachoendelaea katika balozi zetu hata kabla ya janga hili kinanipa mashaka na mifumo ya ulinzi ndani na nje,tunachojali kama taifa ni mapato as first priority.
kila idara ifanye kazi kwa ufanisi vinginevyo tutaumiza wengi kizembe...
 
Nimeona kinachoitwa taarifa ya ATCL ya kukanusha uvumi kuwa Kuna ndege ya shirika hilo inayoenda kuwachukua Watanzania waliokwama Ukraine. Taarifa hiyo imenikumbusha namna ndege ya shirika hilo ilivyochoma Mafuta kwenda Madagascar kubeba miti shamba ya COVID-19.
In fact, tuna safari ndefu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…