voicer
JF-Expert Member
- Jul 13, 2020
- 5,545
- 11,935
GENTAMYCINESishangai sana kwani hata katika Ustaarabu Kihistoria barani Afrika ulianzia hasa nchini Ghana.
Sishangai mno kwani hata Siasa bora na Demokrasia iliyokomaa Barani Afrika ilianzia nchini Ghana wengine wakaiga.
Vile vile sishangai zaidi kwani hata Wasoni wengi na Watu Wetevu (Intelligent) Barani Afrika wako nchini Ghana.
Hatimaye leo hi Taifa la Ghana limethibjtisha kuwa halina Upuuzi, Siasa, maneno mengi na Ushamba kwa kuwa Taifa la Kwanza Barani Afrika lililothubutu na kufanikiwa Kuwarudisha Raia wake kutoka nchi Mbili zenye Mzozo wa Kivita za Ukraine na Urusi (Russia)
Mataifa mengine wakati Raia wao wakiwa Wanateseka, Wanabaguliwa na Kuhangaika sana Viongozi wao Waandamizi na Raia wao tokea Juzi, Jana na Leo wako busy Kushangilia na Kujisifu kwa Bendera yao Kupandishwa Dubai (Jengo refu Duniani) na muda wote Wanahimizana tu Kujimwambafai Mitandaoni na Redioni bila kusahau hata Runingani.
Natamani sana atokee tena Kiongozi mwingine (nchi Kubwa na Matajiri) huko Ulaya, Marekani, Mashariki ya Kati na hata Asia kama ambavyo aliwahi kufanya aliyekuwa Rais wa Marekani Mtukutu Mwerevu na Tajiri Donald Trump atunange Waafrika (tena wa nchi fulani moja hivi na Bibi Bomba wao) kuwa hatujitambui, hatujui Kufikiri, Washamba na tunachojua ni Kungonoka, Kuzaana, Uchawi, Majungu, Wivu na kulewa Pombe na Gongo.
Yaani Bendera imewekwa (tena kwa Kunakshiwa Kiteknolojia) na Waarabu waliotuzidi Akili kwa Shinkizo la Bibi Bomba na Pesa ya Ganji aliyowapa ili tumsifu Kiutendaji huku walioweka hiyo Bendera wskihakikishiwa kwenda Kuinyonya nchi kwa Mgongo aa Uwekezaji na percent fulani wanampa Bibi Bomba akawekeze Babarini Kwao Watu wanashangilia.
Taifa likikosa Critical Thinkers ni Hatari.
Hapo umesema ukweli bila chenga,lakini kwa sababu nchi hii ni ya mlengo wa kisiasa na unafiki.
Ni vigumu kwa wote kukuelewa!
Wakati haya yote yanatokea ikumbukwe kwamba kuna ndege za ATCL zimepaki,tena mpya kwa kukosa Route.
Wakati haya yote yanaendelea tunao watalii wapatao 900 kutoka Ukraine [emoji1255] ,ambao wamekwama Visiwani Zanzibar kwa kukosa usafiri wa kuwarudisha Ukraine [emoji1255] shauri ya hiyo vita.
Wakati watoto wetu wamekwama huko Ukraine [emoji1255] na Poland [emoji1200].
Serikali makini ingefanya utaratibu maalumu kwa kushirikiana na Ukraine [emoji1255] kwa kupitia ubalozi wao ulioko nchini
Kenya [emoji1139] .
Ili washirikiane na Tanzania [emoji1241] itowe ndege ya kuwasafirisha hao wa Ukraine [emoji1255] 900 walioko Zanzibar na kuwapeleka hadi nchi jirani ya Poland [emoji1200].
Kisha ndege hiyo hiyo pia itumike kuwabeba watanzania watakaokuwa wamevuka mpaka na kuingia Poland [emoji1200].
Wakiwemo pia hata raia wengine wa Afrika Mashariki.
Tunao ubalozi wetu uko pale
Sweden [emoji1236],na ndio unaotuwakilisha pia huko Ukraine [emoji1255] hivyo balozi wetu huko angetumika kuhakikisha anafanya jitihada za Watanzania kufanikiwa kuvuka mpaka na kuingia Poland [emoji1200].
Ili iwe rahisi wao kuchukuliwa kutokea pale.
Sasa hapo humsikii waziri husika akiongelea kufanya lolote zaidi ya wote kurundikana Dubai wakiishangilia picha ya mama na bendera.
Hatuko serious...
Tunacheka yale tuliostahili kulia...
Na
Tunalia yale tuliostahili kucheka.....