Hili ni jukwaa huru Mkubwa....
Ina maana humu JF kila member ni aidha CCM ama CHADEMA, right?
Kama unadhani hivyo, nakuhakikishia kuwa, HAUKO SAHIHI kwa 1,500,000%....!!
Kuna watu tuko kinyume na serikali hii na Chama Cha Mapinduzi (CCM) na John Pombe Magufuli mwenyewe lakini hutatukuta CHADEMA, ACT Wazalendo ama chama chote cha siasa....!!
Grow up mkubwa, acha kuishi ktk UTUMWA na VIFUNGO vya vyama vya siasa....
Penda nchi yako tu, baasi.....!!
Kuwa mzalendo wa nchi yako tu, baasi.....!!
Kumpenda "mtu kiongozi fulani "ama "serikali", it's just an option" isiyo na ulazima wowote....
Serikali na vyama hivi vya siasa vitapita, lakini nchi yako ndiyo hii hii milele, haitapita.....haibadiliki...
Mfano leo hii itokee vyama vyote vya siasa vyote vife, nchi na watu wake yenyewe itakuwapo tu, haitakufa...
Hata ikitokea leo serikali ambayo kwa sasa inaongozwa na John Pombe chini ya CCM, ikalewa POMBE, ikajikwaa na kufa....nchi ya Tanzania na watu wake, itakuwepo tu, haitakufa....!!
Kitakachofanyika ni kutafuta namna nyingine ya kujitawala na kuindesha nchi yetu, yet, maisha yakaendelea bila matatizo yoyote...!!