"Wakati watu wanalia kuhusu kikokotoo nilikuwa naona kawaida, sasa nimeona ukali wake" Mtumishi aliyeambulia 10M baada ya kustaafu miaka 33 Magereza

"Wakati watu wanalia kuhusu kikokotoo nilikuwa naona kawaida, sasa nimeona ukali wake" Mtumishi aliyeambulia 10M baada ya kustaafu miaka 33 Magereza

analia kwa Furaha baada ya kukunja 21m at once ambayo haijawahi kuishika, analia kwasabb kachelewa kuzipata hizo 21m kwa sababu mbalimbali au analia kwa sababu fedha alizopata ni kidogo kutokana na kiasi kingine kulipa deni alilokopa na kumsaidia mwenye? au analia kwa Furaha kwasabb kiasi kilichobaki kitamsadia kwa muda marefu pole pole kidogo kidogo 🐒

na umejuaje analia kwa miongoni mwa sababu hizo hapo juu? wewe ni nani wake kwanza 🐒

aulizwe vizuri, huenda ana matatizo mengine binafsi makubwa zaidi, lakini Sheria hii haibagui cheo au nafasi ulioko. Sheria ni msumeno yeyote atakaestaafu atafuata sheria ya kikokotoo iliyopo 🐒
Yeyote anaestaafu? Na mbunge nae anafuata sheria hii?
 
Unapata kulingana na mshahara wako. Commissioner boss mkubwa huyo.
Asante kwa elimu, sasa hicho kikokotoo kikikatwa kinapelekwa wapi yaan mstaafu atakifaidi vipi?

Nilisikiaga watu wanapiga kelele sikufatiliaga kikokotoo ni cha nini na kikikatwa kinapelekwa wapi?
 
Asante kwa elimu, sasa hicho kikokotoo kikikatwa kinapelekwa wapi yaan mstaafu atakifaidi vipi?

Nilisikiaga watu wanapiga kelele sikufatiliaga kikokotoo ni cha nini na kikikatwa kinapelekwa wapi?
Unalipwa kiduchu,inayobaki nyingi wanakulipa kidogo kidogo wakijua baada ya miaka mitatu utakufa inayobaki wanajikopesha mikopo mikubwa isio na riba.
 
hao wanaenjoy privileges na immunities za kipekee sana kulingana na kazi, wajibu na majukumu yao mazito, makubwa mno na ambayo ni muhimu na sensitive sana kwa maslahi ya Taifa. Kwa hiyo, wao wako guided na kanuni na taratibu za bunge ambazo ziko kwa mujibu wa katiba. Just check East Africa parliamentary system, achilia mbali huko duniani 🐒
 
Unalipwa kiduchu,inayobaki nyingi wanakulipa kidogo kidogo wakijua baada ya miaka mitatu utakufa inayobaki wanajikopesha mikopo mikubwa isio na riba.
Unasemaje? Wabunge wa tanzania wamepitisha hii sheria? Embu wacha utani, na watumishi wamekubali?

So wakati wanamlipa kidogo ikitokea akifa na ndugu hawapewi kilicho baki?

Je hicho kikokotoo mstaafu anajua ni sh. Ngapi?
Mbona hii inaumiza jamani? Mbona mm siwezi ivumilia?
 
Ukifa beneficiaries hawaambulii kitu. Wanakupa pesa for 12 years. Kisha wanakata. Hivyo maana yake mwisho kuishi miaka 72 ufe. Ukizidi hapo utajua mwenyewe.
 
Ukifa beneficiaries hawaambulii kitu. Wanakupa pesa for 12 years. Kisha wanakata. Hivyo maana yake mwisho kuishi miaka 72 ufe. Ukizidi hapo utajua mwenyewe.
Hiki ndo kinaendelea tanzania hii?

Kwa hiyo ile ya kila mwezi nusu mshahara wa mstaafu haipo tena? Mbona maumivu.

Mimi niliachaga ualimu nikaenda kusoma kitu nilichokuwa napenda, ingawa nilisota mitaani ila sikuwahi kujuta kuacha ualimu, nilikuwa nauchukia kumbe bora niliuacha.

Mama yangu aliumia sana mimi kuacha ualimu eti nimekosa mshahara wa kila mwezi, eti walimu wanajenga mapema eti itakuwaje?

Nikamwambia mama wewe omba niwe hai, wakati ukifika nitakuwa nakutumia hela bila kusubiri mwisho wa mwezi, na ndivyo ilivyo kwa sasa baada ya msoto wa miaka kama 8.

Wakati nikiwa mwalimu kila mwezi nikifata mshahara nanunua mazagazaga, namtumia mama basi ilikuwa furaha yake kila mwezi mazaga zaga yakishushwa barabarani, basi mashoga zako wanamuonea wivu.

Nilipo acha kazi aliumia eti koz niliyo soma sitopataga kazi nani atamuhudumia? Ni kweli baada ya chuo sikupata kazi.

Yaani kwa ufupi nilipo acha kazi nikaenda kusoma kozi nyingine mshahara ukakatwa, mateso yakaanza ahaaa shoga yangu mama yangu anaumia balaa.

Mungu hana choyo jpm (rip) akatumbua wenye vyeti feki, wenye vyeti halali tukaanza kuwa na dhamani, hata private, ndo kazi ikapatikana, ambayo ni uhuru na ninacho kipata sio kusubiri kikokotoo.

Shoga yangu sasa nyumbani tukiwa tunapiga stori anasema dah waalimu wana maden dah, ila wana mikopo nabaki nacheka, mimi hela ya kusubiri kila mwezi siiwezi.

Hicho kikokotoo kitanikuta nikiwa hai? Kula hela yako ukiwa hai.
 
zipo kanuni na taratibu za bunge ambazo ni kwa mujibu wa katiba, lazima zizingatiwe katika kumpatia mbunge mafao yake 🐒
Jibu swali, mbunge anapitia kikotoo kama huyo mstaafu wa magereza? Swali hili nimeuliza baada ya wewe kusema kila mstqafu anapitia utaratibu HUO.
 
hao wanaenjoy privileges na immunities za kipekee sana kulingana na kazi, wajibu na majukumu yao mazito, makubwa mno na ambayo ni muhimu na sensitive sana kwa maslahi ya Taifa. Kwa hiyo, wao wako guided na kanuni na taratibu za bunge ambazo ziko kwa mujibu wa katiba. Just check East Africa parliamentary system, achilia mbali huko duniani 🐒
Nigga please!
 
Mara nyingi tunajiona tuko salama, tunafikiri mabadiliko, kanuni, sheria za kigandamizi zinazofanywa na watawala hazituhusu sisi hasa hawa watumishi wa uma; watu wa magereza, wanajeshi, maaskari police, watumishi wa almashauri, walimu, mahakimu n.k.

Hutashangaa kusikia kada hizi zikikemea wanaopinga kikokotoo kipya, hutashangaa kusikia wakiwapinga na kuwabeza wanaotaka katiba mpya, hutashangaa wakiwabeza wanaowauliza watawala dhalimu maswali magumu na ya msingi kuhusu kubinafsishwa kwa bandari zetu zote na baadhi ya misitu na hifadhi za wanyama. Kinyume utawasikia wakisema hao wana wivu, hawa ni wapinga serikali, hawa hawana akili, wametumwa na mabeberu, hakika watatuhalibia amani na upendo wa nchi yetu

Sasa leo yamemkuta aliyekuwa mtumishi wa Magereza ndugu Shamte (56) staff Surgent alipojikuta akiambulia kiinua mgongo (malipo ya pension ya kustaafu) cha shilingi 21 millioni badala ya shilingi 55 millioni aliyotarajia baada ya kuitumikia serikali kwa miaka zaidi ya 33.Mstaafu huyo aliyasema hayo baada ya kutembelea ofisi za Magazeti ya mwananchi juzi.

"Najiona mfungwa mtarajiwa baada ya kubakia na shillingi 10 millioni kwani shillingi 10 millioni nyingine zimekatwa baada ya kuwa nilikopa chama cha ushirika wa Akiba na Mikopo cha watumishi wa Jeshi la Magereza" alitoa masikitiko yake bwana Shamte akitumia mfano wa mateso ya watu aliokuwa akiwachunga kila siku wakati akifanya kazi gerezani, kwani anajua machungu ya kuwa mfungwa. "Nilitegemea nikanunue shamba la kulima mazao niweze kujisitili baada ya kustaafu sasa haiwezekani, sioni mbele maisha yatakuwaje" bwana Shamte akitoa sentensi kuashiria kukata tamaa ya maisha

"Wewe ndugu, utaratibu wa malipo ya pensheni halipi CGP, waziri husika au katibu mkuu, utalipwa kulingana na michango yako" hayo ndiyo majibu ya kifupi na kukatisha tamaa aliyopewa mtumishi mstaafu ndugu Shamte kutoka kwa wakuu wake baada ya kupata ujumbe wa kiasi atakacholipwa.

Swali la kujiuliza ni, je ? tuko akina Shamte wangapi? akina shamte ambao tunakubali kila kitu watawala wanachopitisha kwa manufaa yao, akina shamte tunaokuwa wa kwanza kuwanyooshea vidole wale wachache wenye akili timamu na uthubutu wa kuhoji haya mabadiliko dhalimu kwa niaba na manufaa yetu, utasikia hawana akili hao, utasikia wamechanganyikiwa hao, nakwambia utasikia wametumwa na wazungu , mabeberu. Wengi wetu tunafikili madhara ya sheria dhalimu , mabadiliko kandamizi haya hayatuhusu sisi, yanawahusu wale tu wanaolalamika.

Hakika bwana shamte amekumbuka shuka wakati kunakucha , amekumbuka jinsi alivyokuwa akiwadharau waliokuwa wakipinga kikokotoo kipya na pengine alishiriki kuwahadhibu walipopelekwa gerezani alikokuwa akifanya kazi, hakika alimalizia kwa kutubu na kusema "Wakati watu wanalia kuhusu kikokotoo nilikuwa naona kawaida,sasa nimeona ukali wake.

Swali la msingi ni, Je...? wewe na mimi tumejifunza nini katika kisa mkasa hiki cha mstaafu Shamte?
Mm najuta sana, mkataba umeisha toka mwaka jana May, nafutalia pesa zangu lakin bilabila unaambiwa mpk miaka 55-60 wakati hata 40 sijafika mamaeeeeh
 
Back
Top Bottom