"Wakati watu wanalia kuhusu kikokotoo nilikuwa naona kawaida, sasa nimeona ukali wake" Mtumishi aliyeambulia 10M baada ya kustaafu miaka 33 Magereza

Hiyo mil 10 aloyobaki nayo je hakuna posho yoyote atakayokuwa anapata kila mwisho wa mwezi ??

Hapo hiyo mil 10 ndo silaha yake ya mwisho anabodi kuitumia vzr Sana .
 
Jibu swali, mbunge anapitia kikotoo kama huyo mstaafu wa magereza? Swali hili nimeuliza baada ya wewe kusema kila mstqafu anapitia utaratibu HUO.
nimekuelekeza jinsi mambo yalivyo, unataka kuleta mambo ya agano la kale hapa. shauri yako kama hutaki kuchukua hiyo, baki hivyo hivyo maana hakuna namna nyingine 🐒

lakini waandamizi katika mihimili ya dola wanaenjoy privileges na immunities kadha wa kadha kwa mujibu wa kanuni, taratibu, Sheria na katiba ya nchi bila mbambamba yoyote ndugu mwananchi 🐒
 
TuliambiwPX
Si Bora hata huyo kapata m10 yake. Wengine hata Senti hatukupewa na tunaambiwa tutafute ajira as if wanajua malengo yangu.
Mkuu yaani uliajiriwa ukatumikia miaka kibao siku ya kustaafu hukupata kitu?
 
Hela ya kila mwezi (pension) unaipata kwa miaka 12 tu kisha inakoma.
Hongera kwa kujiongeza. Tanzania pagumu kwa wengi na neema kwa wachache at the cost of many.
 
Haiwezekani Samaki Sato/Sangara...akalingana bei na Kambale!

Kila mbuzi ale kwa urefu wa kamba yake,

Haiwezekani mshahara wa lakini 4 upate pensheni sawa na anaelipwa mil 2 Kwa mwezi!

Ili mjifunze ya kwamba Kuna maisha baada ya hizo nafasi zenu mnazojivunia!

Kila mtu ale kwa urefu wa kamba yake!

Mbona sisi sekta binafsi tunalipwa kile tulichochangia tu!?

Tena bila hata faida yoyote! Na pesa wameizalishia miaka!


Mpate pensheni kulingana na mlichochangia!

Ova!
 
Mfuko ni mmoja.
Mimi naongea sio stori ya kijiweni. Ndugu yangu aliyestaafu kaambiwa wanalipwa kwa miaka 15 tu.
Mimi ni mstaafu.
Na wako waliostaafu kabla yangu wanalipwa, nitafuatilia na pia kwa wenzangu
Ili nilete majibu ya kina, ila hii kikotoo ni kibaya sana. Tungejua wanapata kiasi gani kila mwezi pia sababu tumeambiwa, watapata hela nyingi.
Nitafuatilia miaka 60 +15 naona 75 hapokati wengi tunarudisha namba.
Kwa ushauri wangu bora ustaafu miaka 55 unakuwa na nguvu kidogo. Miaka 60 hata upewe 600m akili na mwili umechoka majukumu na hela unawakabidhi ndugu ns watu wengine wakufanyie miradi kinschofuata ni stress tu na kufa mapema.
 
HIVI nyie mnaowasema askari,mnazijua protocal na viapo vyao?au mnajisemea tu...brabrabra
protocal na viapo kwenye swala la maisha yako binafsi... yani uumie na familia iteseke utuliee kisa protocal na viapo ningekuwa mwajiriwa wa serekali lazima ningekuja kuacha kazi nisingekubali kustafu kwenye uzee huku mustakabari wa maisha yangu upo ktk mfumo wa watu furani never.
 
Wa miaka ya nyuma haiwahusu. Imeanza kwa waliostaafu kuanzia mwaka wa fedha mpya. Lakini kwa ninavyojua siasa za nchi hii, si ajabu akaja rais mwingine akafuta au huyuhuyu akafuta miaka ya usoni kisha wakaitumia kama political campaign.
 
Mbunge anayetunga sheria miaka mitano anaondoka na mamilioni ya fadha na huyo mtumishi miaka 33 ameitumikia nchi hii kwa uaminifu mkubwa.
So sad kwa kweli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…