Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
COMMISSIONER GENERAL OF PRISON (CGP)Kamishina generali wa magereza
Hata ukiongea kilugha pesa haiongezekiCOMMISSIONER GENERAL OF PRISON (CGP)
Nimeongeza Kwa Ung'eng'e Hapo
CCM Mbele Kwa Mbele, Hatunywi Sumu Hatujinyongimitano mingine
Bora umesema, yaani wakuu wao wamepewa priverage kibao hapo kila siku anapokea miposho kibao, 10% za kumwaga na pension yake haitumii kabisa kwani atapewa kila kitu anachohitaji wakati wa kustaafu. Au mmesahahu yule aliyepewa V8 mpya kabisaCommissioner General of Prison
Ndio mkuu wa magereza kama alivyo mkuu wa polisiCCM IGP.
Hawa huwa hawaumii na wanachofanyiwa wa chini yao maana huwa ni sehemu ya wakandamizaji hivyo ili wasiwashe moto wanapostaafu hulipwa posho nono na kuendelea kutunzwa ,kupewa nafasi za kimaamuzi kwenye bodi mbalimbali au ubalozi.
Kuandaa cha kufanya bila kuandaa namna ya kufanikisha unachoandaa ni sawa na kuota usingiziniIla alishajiandalia cha kufanya
Sio rahisi kiasi hichoHiyo milioni 10 anunue pikipiki 2 ambazo ni almost 6m awe analetewa hesabu hiyo nne ndiyo akahangaike kutafuta shamba ambalo halitazidi 1m aanze kilimo mdogomdogo ataweza kuwa na uzee mwema kidogo
Mpaka yakukuteKwani Askari magereza hawapati Ile pension ya kila mwezi baada ya hizo hela za mkupuo?
Akinyolewa utie maji?Hapana.Pambana ubaki na afro.Siyo kila msemo uufuate.Utakwama."mwenzio akinyolewa tia maji nywele zako" Ndio hii
Swali lako siyo la kijinga ila unashangaza sana.Kwani Askari magereza hawapati Ile pension ya kila mwezi baada ya hizo hela za mkupuo?
Wanawaandamania watu wasiojielewa.Waamke.Time is now!Waulize wabunge wakimaliza miaka mitano ya kuparuza meza bungeni(wajinga huita kustaafu) hulipwa shilingi milioni mia ngapi?Halafu,waulize akina "Shamte" kwa miaka 33 ya utumishi serikalini hulipwa senti ngapi?Watumishi amkeni na muache uzuzu wenu.Au mmezaliwa mazuzu by nature?Mkiona Chadema wanaandamana NDO MUELEWE
Wanasemaga ccm oyeeMara nyingi tunajiona tuko salama, tunafikiri mabadiliko, kanuni, sheria za kigandamizi zinazofanywa na watawala hazituhusu sisi hasa hawa watumishi wa uma; watu wa magereza, wanajeshi, maaskari police, watumishi wa almashauri, walimu, mahakimu n.k.
Hutashangaa kusikia kada hizi zikikemea wanaopinga kikokotoo kipya, hutashangaa kusikia wakiwapinga na kuwabeza wanaotaka katiba mpya, hutashangaa wakiwabeza wanaowauliza watawala dhalimu maswali magumu na ya msingi kuhusu kubinafsishwa kwa bandari zetu zote na baadhi ya misitu na hifadhi za wanyama. Kinyume utawasikia wakisema hao wana wivu, hawa ni wapinga serikali, hawa hawana akili, wametumwa na mabeberu, hakika watatuhalibia amani na upendo wa nchi yetu
Sasa leo yamemkuta aliyekuwa mtumishi wa Magereza ndugu Shamte (56) staff Surgent alipojikuta akiambulia kiinua mgongo (malipo ya pension ya kustaafu) cha shilingi 21 millioni badala ya shilingi 55 millioni aliyotarajia baada ya kuitumikia serikali kwa miaka zaidi ya 33.Mstaafu huyo aliyasema hayo baada ya kutembelea ofisi za Magazeti ya mwananchi juzi.
"Najiona mfungwa mtarajiwa baada ya kubakia na shillingi 10 millioni kwani shillingi 10 millioni nyingine zimekatwa baada ya kuwa nilikopa chama cha ushirika wa Akiba na Mikopo cha watumishi wa Jeshi la Magereza" alitoa masikitiko yake bwana Shamte akitumia mfano wa mateso ya watu aliokuwa akiwachunga kila siku wakati akifanya kazi gerezani, kwani anajua machungu ya kuwa mfungwa. "Nilitegemea nikanunue shamba la kulima mazao niweze kujisitili baada ya kustaafu sasa haiwezekani, sioni mbele maisha yatakuwaje" bwana Shamte akitoa sentensi kuashiria kukata tamaa ya maisha
"Wewe ndugu, utaratibu wa malipo ya pensheni halipi CGP, waziri husika au katibu mkuu, utalipwa kulingana na michango yako" hayo ndiyo majibu ya kifupi na kukatisha tamaa aliyopewa mtumishi mstaafu ndugu Shamte kutoka kwa wakuu wake baada ya kupata ujumbe wa kiasi atakacholipwa.
Swali la kujiuliza ni, je ? tuko akina Shamte wangapi? akina shamte ambao tunakubali kila kitu watawala wanachopitisha kwa manufaa yao, akina shamte tunaokuwa wa kwanza kuwanyooshea vidole wale wachache wenye akili timamu na uthubutu wa kuhoji haya mabadiliko dhalimu kwa niaba na manufaa yetu, utasikia hawana akili hao, utasikia wamechanganyikiwa hao, nakwambia utasikia wametumwa na wazungu , mabeberu. Wengi wetu tunafikili madhara ya sheria dhalimu , mabadiliko kandamizi haya hayatuhusu sisi, yanawahusu wale tu wanaolalamika.
Hakika bwana shamte amekumbuka shuka wakati kunakucha , amekumbuka jinsi alivyokuwa akiwadharau waliokuwa wakipinga kikokotoo kipya na pengine alishiriki kuwahadhibu walipopelekwa gerezani alikokuwa akifanya kazi, hakika alimalizia kwa kutubu na kusema "Wakati watu wanalia kuhusu kikokotoo nilikuwa naona kawaida,sasa nimeona ukali wake.
Swali la msingi ni, Je...? wewe na mimi tumejifunza nini katika kisa mkasa hiki cha mstaafu Shamte?
Askari wenye akili wanaasi viapo wanaleta MapondiziHIVI nyie mnaowasema askari,mnazijua protocal na viapo vyao?au mnajisemea tu...brabrabra
Kwa hiyo ukipata kazi ya kiapo na protokali ndiyo uwe mpumbavu.HIVI nyie mnaowasema askari,mnazijua protocal na viapo vyao?au mnajisemea tu...brabrabra
Ila bongo nyoko sana yaani ufaye kazi 33 years tyen unalipwa usd 9000 ndio pension...iseeeMara nyingi tunajiona tuko salama, tunafikiri mabadiliko, kanuni, sheria za kigandamizi zinazofanywa na watawala hazituhusu sisi hasa hawa watumishi wa uma; watu wa magereza, wanajeshi, maaskari police, watumishi wa almashauri, walimu, mahakimu n.k.
Hutashangaa kusikia kada hizi zikikemea wanaopinga kikokotoo kipya, hutashangaa kusikia wakiwapinga na kuwabeza wanaotaka katiba mpya, hutashangaa wakiwabeza wanaowauliza watawala dhalimu maswali magumu na ya msingi kuhusu kubinafsishwa kwa bandari zetu zote na baadhi ya misitu na hifadhi za wanyama. Kinyume utawasikia wakisema hao wana wivu, hawa ni wapinga serikali, hawa hawana akili, wametumwa na mabeberu, hakika watatuhalibia amani na upendo wa nchi yetu
Sasa leo yamemkuta aliyekuwa mtumishi wa Magereza ndugu Shamte (56) staff Surgent alipojikuta akiambulia kiinua mgongo (malipo ya pension ya kustaafu) cha shilingi 21 millioni badala ya shilingi 55 millioni aliyotarajia baada ya kuitumikia serikali kwa miaka zaidi ya 33.Mstaafu huyo aliyasema hayo baada ya kutembelea ofisi za Magazeti ya mwananchi juzi.
"Najiona mfungwa mtarajiwa baada ya kubakia na shillingi 10 millioni kwani shillingi 10 millioni nyingine zimekatwa baada ya kuwa nilikopa chama cha ushirika wa Akiba na Mikopo cha watumishi wa Jeshi la Magereza" alitoa masikitiko yake bwana Shamte akitumia mfano wa mateso ya watu aliokuwa akiwachunga kila siku wakati akifanya kazi gerezani, kwani anajua machungu ya kuwa mfungwa. "Nilitegemea nikanunue shamba la kulima mazao niweze kujisitili baada ya kustaafu sasa haiwezekani, sioni mbele maisha yatakuwaje" bwana Shamte akitoa sentensi kuashiria kukata tamaa ya maisha
"Wewe ndugu, utaratibu wa malipo ya pensheni halipi CGP, waziri husika au katibu mkuu, utalipwa kulingana na michango yako" hayo ndiyo majibu ya kifupi na kukatisha tamaa aliyopewa mtumishi mstaafu ndugu Shamte kutoka kwa wakuu wake baada ya kupata ujumbe wa kiasi atakacholipwa.
Swali la kujiuliza ni, je ? tuko akina Shamte wangapi? akina shamte ambao tunakubali kila kitu watawala wanachopitisha kwa manufaa yao, akina shamte tunaokuwa wa kwanza kuwanyooshea vidole wale wachache wenye akili timamu na uthubutu wa kuhoji haya mabadiliko dhalimu kwa niaba na manufaa yetu, utasikia hawana akili hao, utasikia wamechanganyikiwa hao, nakwambia utasikia wametumwa na wazungu , mabeberu. Wengi wetu tunafikili madhara ya sheria dhalimu , mabadiliko kandamizi haya hayatuhusu sisi, yanawahusu wale tu wanaolalamika.
Hakika bwana shamte amekumbuka shuka wakati kunakucha , amekumbuka jinsi alivyokuwa akiwadharau waliokuwa wakipinga kikokotoo kipya na pengine alishiriki kuwahadhibu walipopelekwa gerezani alikokuwa akifanya kazi, hakika alimalizia kwa kutubu na kusema "Wakati watu wanalia kuhusu kikokotoo nilikuwa naona kawaida,sasa nimeona ukali wake.
Swali la msingi ni, Je...? wewe na mimi tumejifunza nini katika kisa mkasa hiki cha mstaafu Shamte?
Na,katika hizo 9000 bado una deni la 4500 unatakiwa ufanye clearance. Wazimu usipokushika ujue wewe ni malaika in disguise.Ila bongo nyoko sana yaani ufaye kazi 33 years tyen unalipwa usd 9000 ndio pension...iseee