Wakatoliki: Bikra Maria utuombee kwa mwanao Yesu. Je, bado yu hai?

Wakatoliki: Bikra Maria utuombee kwa mwanao Yesu. Je, bado yu hai?

Siku zote nimekuwa nikiwasikia wakatoliki katika sara zao wakimuomba bikra Maria, mama yake Yesu, awaombee. Hata katika nyimbo nyingi wanazotunga, wanamtaja bikra Maria na kumsihi awaombee kwa Yesu. Je, kwani huyu mama bado yu hai? Je, imani ya dini yao haihuruhusu muumini kumuomba Yesu moja kwa moja bila kupitia kwa mama yake?

View: https://www.youtube.com/watch?v=V9C1rqOJfxc
Hili ni swali ambalo nimekuwa nikijiuliza kwa muda mrefu bila majibu lakini nikaona leo nilete hili swali mbele ya wanazuoni wa masuala ya dini mliojaa hapa JF mnisaidie kutegua hiki kitendawili. Mtu yeyote anayefahamu hili suala kinagaubaga naomba anifahamishe nipate kuelewa.

Kwa uelewa wangu mdogo, nafahamu kuwa mtu pekee aliyekufa na kufufuka ni Yesu tu. Sasa huyu bikra Maria ina maana yeye hakufa? Kama bado yu hai yupo wapi? Tunaambiwa Yesu baada ya kufufuka alipaa mbinguni na ameketi mkono wa kuume wa Mungu. Je, Maria yeye yu wapi? Au yeye ndiye ameketi mkono wa kushoto?

Maswali ni mengi lakini kwa kuwa humu JF kuna watu wenye uelewa mkubwa wa masuala ya dini, wakiwemo mapdre na maaskofu wa kanisa Katoliki mliomo humu, naomba mnifafanulie kuhusu hili jambo nipate kufunguka macho.

Asanteni sana.

Sala za kipagani hizi
 
Uo
Hata historia ya Biblia hujui, nilikuuliza mwanzo ukakimbia, Miaka ya 300 tayar biblia ya vitabu73 ilikuwepo, nani sasa alipunguza? ni Martin Luther, na hakuishia hapo tu aliondoa vitabu vingi tu ikiwamo ufunuo wa Yohane lakini baada ya kufa wafuasi wake walivirudisha.
Io ni mwaka 300 sio
Lakini ila sio kipindi cha mitume
Mitume hawakuwa na hivyo vitabu mlivyoongeza.
Myahudi tu havitambui wala hawatambui ao waandishu
 
Na kuna ubaya gani kupitisha maombi yetu kwa Mama Maria kisha akafikisha kwa Yesu? Zote ni njia cha muhimu maombi yafike
Mungu aliweka njia ya kufikisha maombi kwake na sio kwa kupitia marehemu.
Alipokata roho yesu pazia la hekalu lilipasuka ili kila mtu azungumze na Mungu moja kwa moja sio kupitia mtu(kuhani)
 
Bikra Maria alibarikiwa na Mungu ili uzao utakatifu upitie kwake. Kwa hiyo ni Roho inaishi unaweza kuisujudia na ikakusaidia.
Yesu Kristo - ni Roho katika ule utatu na inaishi ambayo tunakombolewa nayo kwa Damu iliyomwagika pale msalabani.
Unaona huu upagani sasa
Hivi unajua mariam alikuwa nakina petro wakifunga na kuomba mpakaa siku ya pentekoste
Roho ilipowashukia akageuka kama mwehu sawa na wengine woote.
Unadhani kwanini alifunga na kuomba kama yeye ni mama wa Mungu
 
Aisee kumbe we ni chizi! I was wasting my energy.
Kazi ipo
Inamana hujui kuwa yesu alimwambia mariamu acha kunulilia mlee mwanao(yohana)
Hujui yohana ndie alikuwa mwanafunzi mdogo kupita wote na aliependwa sana na yesu
Wanafunzi walikuwa wakimtumia yeye kuuliza maswali.
Mariamu hakumzaa yesu tuu
Alienda akaishi na yusufu na wakaendeleza familia ama unadhani yusufu alioa mwanamke mwingine??
Ama aliishi na mwanamke aliemzalia mtoto ambae si wake tu.
Io roho ni ya ibilisi.
Inapinga bila kujua maandiko.
Watu walimuita yesu mwehu,belzebur mkuu wa majini na mapepo kwa kutokujua maandiko
 
Wewe huna lolote unalojua. Mvivu wa kufuatilia. Eti vimeongezwa. Yani watu wavikate vitabu miaka 1500 baadae ndio useme tumeongeza? Kweli waprotestanti mna funza kichwani.😂 Ukimuamsha mtu wa mwaka 1200 huko akiona kipande cha bibilia mnachosoma atawashangaa sana. Nani alimpa mamlaka Luther kukata vitabu? Paulo , na wengine wote vitabu vyao vikikuwa vinajitegemea, ndio kanisa kwa kuvuviwa na Roho wa Mungu likavikusanya alafu mnajikuta mnajua.
Kama funza waliopo kichwani wananifanya nidumu na neno la Mungu ni heri hao.
Vitabu vilishakuwepo kabla ya mwaka 1500 unaousema kabla ya kuunganishwa na vatikan nyaraka zakina petro na mitume zilishakuwepo
Biblia inasema neno la Mungu limeshikamana na halipingani,
Wewe unadhani kwanini luther alitakwa auwawe?
Wakati katoliki inauza vitubio vya dhambi ili mtu asamehewe na Mungu.
Unadhani kwa nini urumi usingeweza kukubaliwa israel tangu miaka hio??
Wewe unadhani waprotestan walikuwa wehu woote hao wakavikataa hivyo vitabu vya pombe na ulevi,?
Kwa sababu hivyo vitabu haviendani na neno la mungu la awali
 
Sasa hapa umeandika nini mkuu? Unataka kutuaminisha kuwa bikra Maria ni mmoja wa malaika wa Mungu?
Bikira maria hana sehem kwenye maandiko zaidi ya kumzaa Bwana yesu tu
Huyo mwanamke wa ufunuo wanaemchora ni fumbo na si mariam
 
Watu walioandika biblia kuna makosa mengi sana ya kiufundi walifanya.

Mfano: Huwezi kusema Mungu ni roho, halafu wakati huo huo ana MKONO WA KUUME na wa kushoto. Huo mkono unatokea wapi tena? Roho zina mikono?
Sisi kwenye Kitabu cha mtume SAW kuna kauli nyingi za kaulii taarifa. Sasa hao waliotuandikia walishindwa kumuwasilisha MUNGU wakafananisha na mtu. Halafu tukaelimishwa na kitabu hicho MUNGU hafanani na chochote ambayo inaweza make sense kuliko zile kauli taarifa.
 
Hakusema vitu kibao. We unadhani bibilia imesema kila kitu? Kumbuka kanisa lilianza kabla ya bibilia!
Yesu hakuwahi sema maombi kwenda kwake yapitie sehemu nyingine. Hakuwahi. Na utaona hata kuna sehemu alisema mama na ndugu zake ni wale wanaosikiliza na kufuata neno la Mungu. Bikra Maria tuna mheshimu kama mama ambaye alipitishiwa Yesu kisha kazi yake ikaisha hapo. Alibaki kuwa mama wa Yesu tu binadamu kama binadamu mwingine.
 
Wewe na waprotestanti mna matatizo ya kujikuta mnajua, ungejua maana ya "betrothment" na ndo ungeelea. Maria hakuzaa zaidi ya Yesu . Na kiyahudi cousins walikuwa regarded kama brother na sister. Hamjui kwanza maandiko wala mapokeo matakatifu na historia ya wakristo wa kwanza wakifufuka watawashangaeni nyie mapunguani mmetokea wapi? Nyie kwanza ata hamna ibada ni matamasha ya mziki na kelele.
Kazi ipo
Inamana hujui kuwa yesu alimwambia mariamu acha kunulilia mlee mwanao(yohana)
Hujui yohana ndie alikuwa mwanafunzi mdogo kupita wote na aliependwa sana na yesu
Wanafunzi walikuwa wakimtumia yeye kuuliza maswali.
Mariamu hakumzaa yesu tuu
Alienda akaishi na yusufu na wakaendeleza familia ama unadhani yusufu alioa mwanamke mwingine??
Ama aliishi na mwanamke aliemzalia mtoto ambae si wake tu.
Io roho ni ya ibilisi.
Inapinga bila kujua maandiko.
Watu walimuita yesu mwehu,belzebur mkuu wa majini na mapepo kwa kutokujua maandiko
 
Mmeipata wapi hii ?
Ni mapokeo ya wakristo wa kale, wote waliamini na kaburini pake palibaki na maua aina ya Lily. Ni kazi kwelikweli maana kwanza mnaamini sola scriptura kitu cha kutunga. Middle east kwenye wakristo hasa wote mpaka dakika hii wanaamini hivo.
 
Uo

Io ni mwaka 300 sio
Lakini ila sio kipindi cha mitume
Mitume hawakuwa na hivyo vitabu mlivyoongeza.
Myahudi tu havitambui wala hawatambui ao waandishu
Shida yako ndiyo hiyo unatumia ushabiki tu, kutotambuliwa na wayahudi si sababu lakini hata hivyo hao hao wayahudi hawamtambui Yesu wala agano jipya.
Mitume mpaka wanakufa hakukuwa na Biblia bali nyaraka tu ambazo zilikuwa nyingi sana, zingine hata kwenye hiyo Biblia unayotumia hakuna, lakini kwavile kichwani ni nmweupe hutajiuliza kwanini
 
K
Shida yako ndiyo hiyo unatumia ushabiki tu, kutotambuliwa na wayahudi si sababu lakini hata hivyo hao hao wayahudi hawamtambui Yesu wala agano jipya.
Mitume mpaka wanakufa hakukuwa na Biblia bali nyaraka tu ambazo zilikuwa nyingi sana, zingine hata kwenye hiyo Biblia unayotumia hakuna, lakini kwavile kichwani ni nmweupe hutajiuliza kwanini
Kwani biblia ni nini kaka??
Naona kama unadhani ni iko kitabu chenye rangi nyekundu ya karatasi
Biblia ni uo muunganiko
Na ulianza kama scrollings
Moaka tulipofikia sasa kwenye softcopies
 
K

Kwani biblia ni nini kaka??
Naona kama unadhani ni iko kitabu chenye rangi nyekundu ya karatasi
Biblia ni uo muunganiko
Na ulianza kama scrollings
Moaka tulipofikia sasa kwenye softcopies
Hili ndio tatizo la kuwa na akili kisoda, wewe ndio hujanielewa.
Biblia uliyonayo ni kazi ya Kanisa Katoliki, Vitabu viko vingi sana, hizo injili zipo zaidi ya 20 ila hapo unaona nne tu kwasababu ni maamuzi ya Kanisa, na usibeze mapokeo maana baada ya mambo kupita, na kusemwa mengi basi watu ndio waliandika.

Luka 1
Kwa kuwa watu wengi wameweza kuandika kwa utaratibu habari za mambo yaliyotimizwa katikati yetu, 2 kama walivyotuhadithia wale waliokuwa mashahidi wenye kuyaona, na watumishi wa lile neno tokea mwanzo, 3 nimeona vema mimi nami, kwa kuwa nimejitafutia usahihi wa mambo hayo yote tangu mwanzo, kukuandikia kwa taratibu,
 
tpaul
Hili ni swali zuri linalohusiana na mafundisho na imani ya Kanisa Katoliki kuhusu Bikira Maria. Hapa nitakueleza kwa ufupi na kwa uwazi:

1. Kuhusu Bikira Maria kuwa hai:
Kanisa Katoliki linaamini kuwa Bikira Maria, mama wa Yesu, baada ya maisha yake hapa duniani, alichukuliwa mbinguni mwili na roho (imani ya Kupaa kwa Bikira Maria). Hii haimaanishi kuwa yupo hai duniani kama sisi, bali ana nafasi ya pekee mbinguni kama mama wa Yesu na mshirika wa karibu wa Mungu. Kwa sababu hiyo, Wakatoliki wanaamini anaweza kuwaombea waamini kama mama anavyowaombea watoto wake.


2. Kwa nini kumuomba Bikira Maria badala ya moja kwa moja kwa Yesu?
Wakatoliki hawaombi kwa Bikira Maria badala ya Yesu, bali wanamwomba awe mshirika wa sala yao (waombezi). Wanamtambua Yesu Kristo kama mpatanishi mkuu kati ya Mungu na mwanadamu (1 Timotheo 2:5), lakini pia wanaamini kuwa watu watakatifu wanaweza kuwaombea wengine mbele za Mungu. Hii inatokana na imani ya kwamba familia ya Mungu inaunganishwa na upendo, na kwamba waamini walioko mbinguni wanaweza kuwaombea waamini walioko duniani.

Kwa mfano, kama unavyoweza kumwomba rafiki au ndugu akusaidie kukuombea, ndivyo Wakatoliki wanavyomuona Bikira Maria kama mshirika wa sala zao, si kama mbadala wa Yesu.


3. Nyimbo na sala kwa Bikira Maria:
Nyimbo na sala zinazomuhusisha Bikira Maria haziishii kwake peke yake, bali huwa zinamwelekeza Yesu Kristo. Maria anaheshimiwa kama mama wa Mungu (Yesu ni Mungu), na heshima hiyo si ibada inayochukua nafasi ya Yesu, bali ni ishara ya shukrani kwa nafasi yake ya kipekee katika mpango wa wokovu.


4. Je, lazima kila Mkatoliki amuombe Bikira Maria?
Hapana, si lazima. Wakatoliki wanaweza kumuomba moja kwa moja Yesu bila kupitia kwa Bikira Maria. Sala zote zinakubalika mbele za Mungu mradi mtu ana imani ya dhati.



Kwa ufupi, kumuomba Bikira Maria si kumwondoa Yesu, bali ni kumshirikisha mama wa Yesu katika safari ya imani. Hii ni sehemu ya utamaduni na mafundisho ya Kanisa Katoliki, lakini waamini wana uhuru wa kuchagua namna ya kusali kadri wanavyos
ukumwa na imani yao.
© Jackson94
 
Back
Top Bottom