Wakatoliki: Bikra Maria utuombee kwa mwanao Yesu. Je, bado yu hai?

Hili ndio tatizo la kuwa na akili kisoda, wewe ndio hujanielewa.
Biblia uliyonayo ni kazi ya Kanisa Katoliki, Vitabu viko vingi sana, hizo injili zipo zaidi ya 20 ila hapo unaona nne tu kwasababu ni maamuzi ya Kanisa, na usibeze mapokeo maana baada ya mambo kupita, na kusemwa mengi basi watu ndio waliandika.

Luka 1
Kwa kuwa watu wengi wameweza kuandika kwa utaratibu habari za mambo yaliyotimizwa katikati yetu, 2 kama walivyotuhadithia wale waliokuwa mashahidi wenye kuyaona, na watumishi wa lile neno tokea mwanzo, 3 nimeona vema mimi nami, kwa kuwa nimejitafutia usahihi wa mambo hayo yote tangu mwanzo, kukuandikia kwa taratibu,
Injili zipo nne tuu
Izo zingine hazikukidhi uhaliisia wa maisha ya Yesu kristo
 
tpaul
Hili ni swali zuri linalohusiana na mafundisho na imani ya Kanisa Katoliki kuhusu Bikira Maria. Hapa nitakueleza kwa ufupi na kwa uwazi:

1. Kuhusu Bikira Maria kuwa hai:
Kanisa Katoliki linaamini kuwa Bikira Maria, mama wa Yesu, baada ya maisha yake hapa duniani, alichukuliwa mbinguni mwili na roho (imani ya Kupaa kwa Bikira Maria). Hii haimaanishi kuwa yupo hai duniani kama sisi, bali ana nafasi ya pekee mbinguni kama mama wa Yesu na mshirika wa karibu wa Mungu. Kwa sababu hiyo, Wakatoliki wanaamini anaweza kuwaombea waamini kama mama anavyowaombea watoto wake.

2. Kwa nini kumuomba Bikira Maria badala ya moja kwa moja kwa Yesu?
Wakatoliki hawaombi kwa Bikira Maria badala ya Yesu, bali wanamwomba awe mshirika wa sala yao (waombezi). Wanamtambua Yesu Kristo kama mpatanishi mkuu kati ya Mungu na mwanadamu (1 Timotheo 2:5), lakini pia wanaamini kuwa watu watakatifu wanaweza kuwaombea wengine mbele za Mungu. Hii inatokana na imani ya kwamba familia ya Mungu inaunganishwa na upendo, na kwamba waamini walioko mbinguni wanaweza kuwaombea waamini walioko duniani.

Kwa mfano, kama unavyoweza kumwomba rafiki au ndugu akusaidie kukuombea, ndivyo Wakatoliki wanavyomuona Bikira Maria kama mshirika wa sala zao, si kama mbadala wa Yesu.

3. Nyimbo na sala kwa Bikira Maria:
Nyimbo na sala zinazomuhusisha Bikira Maria haziishii kwake peke yake, bali huwa zinamwelekeza Yesu Kristo. Maria anaheshimiwa kama mama wa Mungu (Yesu ni Mungu), na heshima hiyo si ibada inayochukua nafasi ya Yesu, bali ni ishara ya shukrani kwa nafasi yake ya kipekee katika mpango wa wokovu.

4. Je, lazima kila Mkatoliki amuombe Bikira Maria?
Hapana, si lazima. Wakatoliki wanaweza kumuomba moja kwa moja Yesu bila kupitia kwa Bikira Maria. Sala zote zinakubalika mbele za Mungu mradi mtu ana imani ya dhati.

Kwa ufupi, kumuomba Bikira Maria si kumwondoa Yesu, bali ni kumshirikisha mama wa Yesu katika safari ya imani. Hii ni sehemu ya utamaduni na mafundisho ya Kanisa Katoliki, lakini waamini wana uhuru wa kuchagua namna ya kusali kadri wanavyos
ukumwa na imani yao.
© Jackson94
Mungu hana mama hana baba
Hana mshirika.
Hakuna alie nanafasi ya upendeleo mbele ya Mungu
Mariamu alifunga na kuomba moaka siku aliposhukiwa na roho mtakatifu na alionekana kama kichaa
Hayupo sehem nyingine isipokuwa walipo manabii na mitume
 
Siku zote nimekuwa nikiwasikia wakatoliki katika sara zao wakimuomba bikra Maria, mama yake Yesu, awaombee. Hata katika nyimbo nyingi wanazotunga, wanamtaja bikra Maria na kumsihi awaombee kwa Yesu. Je, kwani huyu mama bado yu hai? Je, imani ya dini yao haihuruhusu muumini kumuomba Yesu moja kwa moja bila kupitia kwa mama yake?

View: https://www.youtube.com/watch?v=V9C1rqOJfxc
Hili ni swali ambalo nimekuwa nikijiuliza kwa muda mrefu bila majibu lakini nikaona leo nilete hili swali mbele ya wanazuoni wa masuala ya dini mliojaa hapa JF mnisaidie kutegua hiki kitendawili. Mtu yeyote anayefahamu hili suala kinagaubaga naomba anifahamishe nipate kuelewa.

Kwa uelewa wangu mdogo, nafahamu kuwa mtu pekee aliyekufa na kufufuka ni Yesu tu. Sasa huyu bikra Maria ina maana yeye hakufa? Kama bado yu hai yupo wapi? Tunaambiwa Yesu baada ya kufufuka alipaa mbinguni na ameketi mkono wa kuume wa Mungu. Je, Maria yeye yu wapi? Au yeye ndiye ameketi mkono wa kushoto?

Maswali ni mengi lakini kwa kuwa humu JF kuna watu wenye uelewa mkubwa wa masuala ya dini, wakiwemo mapdre na maaskofu wa kanisa Katoliki mliomo humu, naomba mnifafanulie kuhusu hili jambo nipate kufunguka macho.

Asanteni sana.
Biblia ya vitabu 66, haikueleza chochote kuhusu kifo cha Mariam. Na kwa maelekezo ya Biblia watu wote wakifa hurudi mavumbini/kaburini. Yohana 5:28-29. Na Yesu alisema anaenda kutuandalia makao na atarudi kutuchukua mbinguni Yohana 14:1-3.
 
Siku zote nimekuwa nikiwasikia wakatoliki katika sara zao wakimuomba bikra Maria, mama yake Yesu, awaombee. Hata katika nyimbo nyingi wanazotunga, wanamtaja bikra Maria na kumsihi awaombee kwa Yesu. Je, kwani huyu mama bado yu hai? Je, imani ya dini yao haihuruhusu muumini kumuomba Yesu moja kwa moja bila kupitia kwa mama yake?

View: https://www.youtube.com/watch?v=V9C1rqOJfxc
Hili ni swali ambalo nimekuwa nikijiuliza kwa muda mrefu bila majibu lakini nikaona leo nilete hili swali mbele ya wanazuoni wa masuala ya dini mliojaa hapa JF mnisaidie kutegua hiki kitendawili. Mtu yeyote anayefahamu hili suala kinagaubaga naomba anifahamishe nipate kuelewa.

Kwa uelewa wangu mdogo, nafahamu kuwa mtu pekee aliyekufa na kufufuka ni Yesu tu. Sasa huyu bikra Maria ina maana yeye hakufa? Kama bado yu hai yupo wapi? Tunaambiwa Yesu baada ya kufufuka alipaa mbinguni na ameketi mkono wa kuume wa Mungu. Je, Maria yeye yu wapi? Au yeye ndiye ameketi mkono wa kushoto?

Maswali ni mengi lakini kwa kuwa humu JF kuna watu wenye uelewa mkubwa wa masuala ya dini, wakiwemo mapdre na maaskofu wa kanisa Katoliki mliomo humu, naomba mnifafanulie kuhusu hili jambo nipate kufunguka macho.

Asanteni sana.

Biblia haikueleza chochote kuhusu kifo cha Mariam. Na Yesu mwenyewe alisema watu wote wakifa wanaenda kaburi/ mavumbini. Yohana 5;28-29. Na pia Yesu kabla hajafa msalani aliaga kwamba atarudi kutuchukua mbinguni. Ukweli wa maandiko, ni makosa kudhani, Mariam yuko mbinguni. Kila mtu siku ya mwisho atafufuka.
 
Injili zipo nne tuu
Izo zingine hazikukidhi uhaliisia wa maisha ya Yesu kristo
Ulikuwepo wakati wanaziweka hizo nne au ndio unasikiliza kazi ya wakatoliki ambayo iliagizwa na Papa Damasus I
 
Siku zote nimekuwa nikiwasikia wakatoliki katika sara zao wakimuomba bikra Maria, mama yake Yesu, awaombee. Hata katika nyimbo nyingi wanazotunga, wanamtaja bikra Maria na kumsihi awaombee kwa Yesu. Je, kwani huyu mama bado yu hai? Je, imani ya dini yao haihuruhusu muumini kumuomba Yesu moja kwa moja bila kupitia kwa mama yake?

View: https://www.youtube.com/watch?v=V9C1rqOJfxc
Hili ni swali ambalo nimekuwa nikijiuliza kwa muda mrefu bila majibu lakini nikaona leo nilete hili swali mbele ya wanazuoni wa masuala ya dini mliojaa hapa JF mnisaidie kutegua hiki kitendawili. Mtu yeyote anayefahamu hili suala kinagaubaga naomba anifahamishe nipate kuelewa.

Kwa uelewa wangu mdogo, nafahamu kuwa mtu pekee aliyekufa na kufufuka ni Yesu tu. Sasa huyu bikra Maria ina maana yeye hakufa? Kama bado yu hai yupo wapi? Tunaambiwa Yesu baada ya kufufuka alipaa mbinguni na ameketi mkono wa kuume wa Mungu. Je, Maria yeye yu wapi? Au yeye ndiye ameketi mkono wa kushoto?

Maswali ni mengi lakini kwa kuwa humu JF kuna watu wenye uelewa mkubwa wa masuala ya dini, wakiwemo mapdre na maaskofu wa kanisa Katoliki mliomo humu, naomba mnifafanulie kuhusu hili jambo nipate kufunguka macho.

Asanteni sana.

Unataka kufunguka macho ya nini kwa imani isiyo yako?
 
Hii ni sehemu ya utamaduni na mafundisho ya Kanisa Katoliki
Hapa nimekuelewa vema sana mkuu. Kumbe hili jambo ni utamaduni tu wa kanisa katoliki kama wadau wengine walivyochangia hapo juu? Ni kama vile wakatoliki walipotuletea suala la Krismas, eti kwamba Yesu alizaliwa tarehe 25 Desemba! Mambo mengi ya wakatoliki ni ya kimapokeo zaidi kuliko ya kiroho. Kwa mfano, hili la Krismas limekaa kipagani zaidi.
 
Hii ni fumbo la imani Maana yake , Kristo alikufa, Kristo,alifufuka na Tena atarudi Duniani, kuwahukumu wazima na wafu
 
K

Kwani biblia ni nini kaka??
Naona kama unadhani ni iko kitabu chenye rangi nyekundu ya karatasi
Biblia ni uo muunganiko
Na ulianza kama scrollings
Moaka tulipofikia sasa kwenye softcopies
Huo muunganiko nani aliunganisha na ni nani aliamua kitabu flani kiwepo au kisiwepo? Mnadhani imetokea angani? Waprotestanti mmepotoka sana na hamjijui kama mmefeli.
 
Mimi kwenye bible yangu hakuna Mathayo bali Mathew.Sijajua kama Maria si Mariamu/Mariam/Maryamu/Maria/Mary au vinginevyo.Je,nimeuziwa "baibl" fekero?
Kwa hiyo shida hapa ni nini mkuu? Hebu rejea kwenye mada.
 
Siku zote nimekuwa nikiwasikia wakatoliki katika sara zao wakimuomba bikra Maria, mama yake Yesu, awaombee. Hata katika nyimbo nyingi wanazotunga, wanamtaja bikra Maria na kumsihi awaombee kwa Yesu. Je, kwani huyu mama bado yu hai? Je, imani ya dini yao haihuruhusu muumini kumuomba Yesu moja kwa moja bila kupitia kwa mama yake?

View: https://www.youtube.com/watch?v=V9C1rqOJfxc
Hili ni swali ambalo nimekuwa nikijiuliza kwa muda mrefu bila majibu lakini nikaona leo nilete hili swali mbele ya wanazuoni wa masuala ya dini mliojaa hapa JF mnisaidie kutegua hiki kitendawili. Mtu yeyote anayefahamu hili suala kinagaubaga naomba anifahamishe nipate kuelewa.

Kwa uelewa wangu mdogo, nafahamu kuwa mtu pekee aliyekufa na kufufuka ni Yesu tu. Sasa huyu bikra Maria ina maana yeye hakufa? Kama bado yu hai yupo wapi? Tunaambiwa Yesu baada ya kufufuka alipaa mbinguni na ameketi mkono wa kuume wa Mungu. Je, Maria yeye yu wapi? Au yeye ndiye ameketi mkono wa kushoto?

Maswali ni mengi lakini kwa kuwa humu JF kuna watu wenye uelewa mkubwa wa masuala ya dini, wakiwemo mapdre na maaskofu wa kanisa Katoliki mliomo humu, naomba mnifafanulie kuhusu hili jambo nipate kufunguka macho.

Asanteni sana.

Mbali na Bikira Maria, kuna wale watakatifu, je na wenyewe wapo hai?! Ili kupata uhondo wa ngoma ingia ucheze!!
 
Back
Top Bottom