Mwanamwana
Platinum Member
- Aug 1, 2011
- 9,604
- 22,722
Waumini wa kanisa katoliki wameeleza kusikitishwa na kauli zilizotolewa na Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padri Dkt. Charles Kitima, wakionyesha kushangazwa namna alivyopuuza sakata la mmoja wa waumini hao kuvamiwa na kupigwa.
Wamemtaka Padri Kitima kuchagua upande kati ya siasa na dini, huku wakimtuhumu kuhusika katika kupanga matukio ya uvunjifu wa amani yaliyotokea oktoba 29, 2025, ambapo wamesisitiza kuwa wanaushahidi wa kutosha juu na kuhusika kwake.