Wakatoliki huwa wanapenyezaje watu wao kuwa Marais wa Tanzania?

Wakatoliki huwa wanapenyezaje watu wao kuwa Marais wa Tanzania?

Kwa hiyo hata KKKT,ANGLICAN nao ni hivyo hivyo? Mbona nchi nyingi tu za Afrika zinaongozwa na wasio wakatoliki na zina viongozi wenye uwezo mzuri tu.
Waprotestant wa Tanzania ni tofauti na sehemu nyingine duniani.. Wanashindana kubuni vituko. Hata huko wamegawanyika Kuna low church na high church
 
Sijui kama kuna mpango wote, ila Kwa uzoefu wangu at least wakatoliki wako moderate linapokuja socialization. Madhehebu mengine yanaona kama dini/madhehebu mengine ni mashetani,wao ndio wako sahihi,wao ndio wanamfuata Mungu wa kweli,wengine wote wanaendan Motoni na hivyo kuwa kutokuwa tayari kusaidia au kutoa msaada Kwa watu wa dini na madhehebu mengine.

Anyway, kuna lile la Rais kuzaliwa Kijijini au familia maskini hili nalo ni janga Kwa nchi. Uzoefu unaonyesha kuwa wana roho mbaya na kutoujali shida za wananchi huku wakijinadi kuwa wao ndio wakombozi! Unfortunately jamii nayo inawaamini! Na kuwaona mashujaa!
Umeandika vizuri wanawadanganya watu kwamba unyonge ni mtaji
 
The role of Jesuits in Catholic ndilo jambo linalowabeba hawana cha maana zaidi
 
Vipi kuhusu Joe Biden sio mkatoliki?
Mkatoliki mfu. Anajiita devout Catholic huku anaunga mkono mashoga na kutoa mimba! Baraza la Maaskofu Katoliki Marekani walikuwa kwenye debate kali awe excommunicated kwa kuunga mkono vitendo hivyo hadharani.
 
Hiilo lipo kwenye katiba ambayo haijaandikwa!!
Ndo utaratibu kuwa rais atoke Ukatolikini na Bakwata.
Hatuwezi kumpa urais mtu ambaye anasali kanisa mlangoni Lina picha ya mchungaji na mke wake.
Au unampa Urais mfuasi wa Sheikh Ponda au Ustaadhi ILUNGA Kapungu
 
MLETA MADA HASOMI KATIBA? HAKUNA MAHALI PANAPO TAKA MKATOLIKI NDIYE AWE RAIS BALI NI MTZ MWENYE SIFA TOSHELEVU HATA WEWE UKITIA NIA UTAPATA ACHA KULIALIA.
 
Hasa hasa Hawa wa Evangelical au waite KKKT kwa hapa wapo 25% ya population ila protestants wote ni kama 50 ya population.

Catholics ni 20% tu.
Ukichukua dhehebu mojamoja bado wakatoliki ndio wengi. Hawa protestants wamekuwa denominated sana. Waanglican kwa US wanajiita episcopalians, hawa na hawa wanaojiita evangelicals (sawa na huku tunaowaita walokole) hawako karibu sana kiitikadi.
 
Tena rais muislamu ni lazima kuwa dhehebu la Sunni kwa sababu BAKWATA katiba yake inasema kwa kutamka bayana kuwa kiongozi mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania atatokana na Sunni..
Sasa mkuu, hii katiba ya BAKWATA ni ya wa-sunni, au ya waislam wote nchini! Imekaa kibaguzi sana, hivyo inakosa sifa kuu za kuwa katiba.

Kinachoitwa katiba shurti kiepukane na ubaguzi wa aina yoyote, au upendeleo. Ndio maana mimi mpaka leo naipinga ile rasimu ya tume ya Warioba kwa kuchomeka vipengele vya kibaguzi na upendeleo.
 
Back
Top Bottom