Wakatoliki kwa kwaya na ufundi wa vinanda ni sawa na samaki na maji

Wakatoliki kwa kwaya na ufundi wa vinanda ni sawa na samaki na maji

Hawa wakatoliki kwaya na ufundi wa upigaji vinanda kwao ni sawa na samaki na maji ni ngumu kuwatenganisha.

Kwa kweli RC ni mafundi haswa katika upande huu wa uburudishaji kwa nyimbo zao za gospel ukichanganya na vinanda vyao.

Ukikutana na mpiga kinanda fundi wa RC mpaka kichwa anatikisa huwa nafurahi sana😁

Nyimbo zao zimetulia sauti zimepangika kuanzia ya kwanza mpaka ya nne ukichanganya na ufundi wa vinanda ni mwendo wa kuburudika tu.

R.C mnatisha balaa
View attachment 2743834
Tahadhari: Huu uzi sio wa mashindano ya kidini
Mhhh, mkuu kwaya ya parokia gani hiyo? Kwa kweli wimbo umetulia. Kama ipo karibu, kesho natinga ibada ya kwanza!
 
Kanisa Katoliki limejaliwa hazina ya watunzi bora kabisa wa nyimbo za Kanisa, na pia wapiga kinanda mahiri kabisa!!

Siku hizi kuna vijana wadogo kabisa kama akina Ray Ufunguo, Tumaini Swai, Credo Mbogoye, Thomas Mashibe (huyu kinanda kinamheshimu sana), Mushobozi (huyu anatumia miguu yote miwili kwenye pedal) na wengineo wengi wakali!! Wanafanya vizuri sana.

Miaka hiyo wakali wa kinanda walikuwa ni akina John Mgandu, Mkude Sekulu, John Maja, nk.
Wamesheheni mafundi haswa kwenye kukanyaga vinanda
 
Hapa nimepata mwalimu wa Catholic ananifundisha kinanda.

Karibuni.

Years is just a numbers,

They're good.
Ukitaka safari yako ya mafunzo iwe nyepesi, hakikisha pia una uelewa wa elimu ya muziki!

Yaani uwe na uwezo wa kuzichambua zile nota za do re mi fa so la si dooo!! Do si la so fa mi re dooo!! Do mi fa re do mi so so, do mi fa re so soo doo!!!
 
Hawa Wakatoliki kwaya na ufundi wa upigaji vinanda kwao ni sawa na samaki na maji ni ngumu kuwatenganisha.

Kwa kweli RC ni mafundi haswa katika upande huu wa uburudishaji kwa nyimbo zao za gospel ukichanganya na vinanda vyao.

Ukikutana na mpiga kinanda fundi wa RC mpaka kichwa anatikisa huwa nafurahi sana😁

Nyimbo zao zimetulia sauti zimepangika kuanzia ya kwanza mpaka ya nne ukichanganya na ufundi wa vinanda ni mwendo wa kuburudika tu.

R.C mnatisha balaa.

View attachment 2743834

Tahadhari: Huu uzi sio wa mashindano ya kidini.
Not a Catholic but a good follower of Saint Francis of Assisi ... and I love inspirational songs!
🙏🙏🙏❣️
 
Dah,eti mama wa Mungu!!..halafu walokole wakisema yesu Mungu wakatoliki mnapinga,yaani hamna uhakika mnaabudu nini
Tahadhari: Huu uzi sio wa mashindano ya kidini.

Ungezingatia hilo katazo toka mwanzo wa huu uzi usingefikia hii level ya ujinga uliyo onesha.
 
Back
Top Bottom