Bado hujajibu swali kwamba kwa nini uongee lugha ambayo wewe huielewi na wala anayekusikia haielewi, wakati imeandikwa mitume walinena lugha ambayo watu wengine wa kutoka nchi mbalimbali waliielewa kila mtu kwa lugha yake. Sasa unasema unashindwa kuielezea hali inavyokuwa, tukisema ni illusion tutakosea?
Wakatoliki tunafuata maandiko matakatifu kwamba Roho Mtakatifu yupo popote na kwa yeyote, hahitaji kumjaza mtu. Ni kwa wato wote.
Yoeli 2:28
28 Hata itakuwa, baada ya hayo, ya kwamba nitamimina roho yangu juu ya wote wenye mwili; na wana wenu, waume kwa wake, watatabiri, wazee wenu wataota ndoto, na vijana wenu wataona maono;